Wanabodi,
Ikumbukwe wakati wa kuzima matangazo ya analogy kwenda digital TCRA waliuambia umma kuwa kwa makampuni ya ving'amuzi lazima yatoe free local channels. Cha kushangaza free ya local channels kwa startimes sasa wameiondoa kwa channels zote za ndani na kubakiza TBC1. Sasa ili kupata channel nyingine za ndani lazima nilipie.
TCRA njoo mtoe ufafanuzi kwa hili ikiwezekana mutangazie umma tena kuwa sasa lazima tulipie hizi channel za ndani yaani; TBC, STAR TV, ITV, EATV, CHANNEL 10, TV 1, CLOUDS TV.
===========
Waziri Nape, hizi kelele za kulipishwa vifurushi kutizama local channel kwenye ving'amuzi huzisikii?
UPDATES..
- JamiiForums imewasiliana na Waziri Nape Nnauye na ameahidi kulifuatilia hili na kulifanyia kazi au kulitolea ufafanuzi
- Hatimaye Serikali yawa sikivu, Local Channels sasa zimerudi hewani

Waziri wa HABARI utamaduni na michezo. Kwa vyovyote hili swala la ving'amuzi lipo chini yako, inakuaje wananchi wanalalamika lakini serikali ipo kimya?
Kwa wale ambao mpaka sasa bado wanaona hizo local channels wajiandae kwani hata mimi nilikua nikisikia tu watu wakilalamika nikawaona kama wapiga kelele kwani mimi nilikua nazipata lakini hatimae nilingia kwenye mkumbo huo hivyo inaonesha ni kama vile kipindi cha uzimaji wa simu feki hazikuzima kwa wakati mmoja.
Watanzania hatutegemei zama hizi za utawala wa awamu ya tano kuona amri halali ya serikali ikipuuzwa na mbaya zaidi inakwenda kuumiza mtanzania wa hali ya chini yaani masikini.
"Serikali yangu inakwenda kulinda na kujali watanzania masikini hasa wanyonge", hapa nimeinukuu kauli ya Rais wa Jamhuri wa Muungano ambayo aliirudia zaidi ya mara 1000 kipindi cha kampeni na hata baada ya kuingia madarakani lakini kauli hii bila ya kuisimamia hasa kwa ninyi watendaji wake itapoteza maana.
Watanzania hatujahama kutoka kwenye analojia kwenda kwenye digiti ili kuwarahisishia mapepari kutunyonya lakini kwa hili la ving'amuzi hii inaweza kua tafsiri yake kwani naona wananchi wanapiga kelele lakini waziri mh Nape kama vile haupo.
Nakumbuka hili swala la wananchi kuona channel za nyumbani bure lilitamkwa bungeni lakini tuliona pale mwanzo walianza kulipuuza ving'amuzi kama AZAM na wengine na hatimae na STAR TIMES nao wamejitoa wakatubakizia TBC tu?
Tumeona STARTIMES wakitoa maelezo yao humu mitandaoni kwamba habari hizi ni za uongo jambo ambalo si kweli, mbona wananchi hatupati channel za nyumbani kwa zaidi ya mwezi sasa?
Hili kama ni tatizo la kiufundi ni tatizo gani lisilorekebishika muda wote huo? Kama hitilafu imetokea kwenye channel za nyumbani imewezekanaje kwa TBC ishindikane kwa zilizobaki?
Tafadhali mh Nape njoo utoe kauli ili kubatilisha ile kauli ya serikali ama uendelee kututetea sisi walala hoi kwani kwako wewe mh waziri 9000 kwa mwezi ni ndogo ila kwa sisi walala hoi hizi gharama zinatuumiza.
UPDATES..
- JamiiForums imewasiliana na Waziri Nape Nnauye na ameahidi kulifuatilia hili na kulifanyia kazi au kulitolea ufafanuzi
- Hatimaye Serikali yawa sikivu, Local Channels sasa zimerudi hewani