TCRA saidieni kutuondolea kero ya matangazo TIGO

TCRA saidieni kutuondolea kero ya matangazo TIGO

Hili ni tatizo kubwa sana. Na linatokana na kuajiri watu wasio na ubunifu. Kuna kazi za kuangalia vyeti na ufaulu darasani na kuna kazi unapokwenda kwa muajiri wako inatakiwa aweke vyeti pembeni kisha akudadisi kichwani umebebelea nini.

Kazi za marketing zinataka watu wenye akili inayofikiria vema kama engine ya rocket. Sio mtu anaiga iga vitu bila kutazama jicho la tatu itakuwaje.

Marketing strategists wa hizi kampuni tajwa wamefeli big time kwenye hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli mtandao huu ni kero kero kubwa sana kutokana na meseji zao za kuhamasisha bahati nasibu. Meseji hizi kwa siku ni zaidi ya ishirini hadi usiku wanatuma, mtu unashindwa hata kulala. TCRA mko wapi? Baadhi wa watu wamediriki hata kuondoa sim card za Tigo kwenye simu zao kuondokana na usumbufu huu na kuhamia mitandao mingine.

TCRA naamini mtachukua hatua!

TIGO ni kero kwa sasa!


Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_2019-03-19-10-21-11.png


Usunbufu mwingine tena wa kitoto kabisa ni kama huu
 
Unajua njia rahisi ni kuchukua hiyo namba inayotuma matangazo ukaweka kwenye block list, message zote zinazokuja haziingiil.
 
Jamani hizi sms na calls toka Tigo ni kero sana je ni mtandao gani hauna huu usumbufu ili wengine tuhamie huko? Ukiblock namba moja wanakupigia mwa namba nyingine, tatizo lipo wapi, tunaomba vyombo vya habari viwaite na kuwahoji ikiwezekana wananchi tuwaulize hao management sababu za kutusumbua wateja namna hii.
nasumbuliwa sana na simu kutoka namba
  • 0713800800
  • 0901656564
  • 0901767676
Na sms kutoka namba
  • 15888
  • 15670
  • 15671
  • 15544
 
Kitu ambachi sielewi, line unanunua, vocha unalipia, huduma zote kwa pesa lakini bado wanatuma matangazo kama vile huduma zao bure!
 
Kitu ambachi sielewi, line unanunua, vocha unalipia, huduma zote kwa pesa lakini bado wanatuma matangazo kama vile huduma zao bure!


Mbaya zaidi mtu upo kazini au kikaoni unakuta simu inaita, unatoka nje kupokea unakuta ni tangazo la biashara, sielewi kwanini wanatulazimisha kusikiliza matangazo yao
 
kama una line ya tigo na voda kuna hizi
KINARA
POLISI
BIKOSPOT
VODACOM TAARIFA
TIGO SMS
Kuna namba za stori za kiseng*seng*
Zinaanzia na 90......
Unaweza pigiwa hata saa kumi usiku
Umesahau BOOMPESA , INSTAMOJA
 
Leo ni wiki sasa sijaona yale matangazo yenye kukera kutoka mtandao wa Tigo. Je inawezekana kuwa hatimaye tatizo limeshapata ufumbuzi? Kama ni hivyo ahsante kwa wote waliowezesha kuondolewa kwa kero hii.
 
Voda nao kero kubwa Sana msg zao wanatuma kwa nzia saa mbili asubui mpaka saa mbili jioni wanaboa Sana
 
Back
Top Bottom