TCRA, mtafuteni aliyechomekea picha hii ashitakiwe kwa upotoshaji!. Watu wataaibika na kuonekana hawana maana!.

Mbona watu wazima na akili zenu mnajadili kitu kidogo mnaacha hoja yenyewe?
Swala hapa sio kuna nini ndani bali kuna mhuni mmoja kaleta makasha yake bila kufata sheria na akawa analazimisha kuyatoa bila kulipia ushuru.
Kwanini mjadili sijui ndani kulikuwa na nini na kutaka kumsafisha Makonda? Tujadili kwanini aliamua kuleta makasha 20 kwa jina lake na kutaka kuyatoa kwa kisingizio ni msaada ambao kwa mujibu wa sheria zetu yeye sio miongoni mwa watu wanaoweza kupata msamaha wa kile kinachoitwa msaada.
Kwanini mnatumia nguvu nyingi sana kumsafisha Makonda wakati Rais ashasema kodi ilipwe.
Mnataka kumuona Rais mjinga wakati yeye hakuwa akizungumzia yaliyomo ndani ila alizungumza kama mfano tu wa vitu ambavyo vikiachwa viende kimazoea kuna wafanyabiashara watatumia mwanya huo kujiingizia bidhaa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Kwa vile kuposti picha ya uongo kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kupotosha jamii, ni kosa la jinai,

Natoa wito kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, kumtafuta mtu aliyepost picha hii na kueleza ni moja ya vilivyomo ndani ya makontena ya Makonda, kitu ambacho sii kweli.
View attachment 854767
Kufuatia picha hii, kuna wengi wamehadai ka kwa kudhani ni kweli sofa ni miongoni mwa vitu vilivyomo kwenye Makontena ya Makonda, hali iliyopelekea hata rais wa Jamhuri ya Muungano, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kushangaa kama waalimu wamehitaji sofa?!, na kueleza inawezekana ni makontena mawili matatu tuu ndiyo yatapelekwa shule, halafu mengine yakaishia shopping malls.

Kufuatia baadhi ya matamshi ya rais wetu, yanathibitisha baadhi ya wasaidizi wa rais, hawamsaidii rais wetu kwenye public, kunakopelekea kumwacha rais kutamka baadhi ya vitu ambavyo haviko sahihi, kitu ambacho kwa namna moja au nyingine, ama kunaifedhehesha taasisi ya urais, au kumfedhehesha rais wetu kuonekana ni mtu anayesema lolote bila kuwa na uhakika, kitu ambachho sio kizuri kwa rais wetu.

Rais wetu anategemewa kuwa very perfect, ndio maana amewekewa wasaidizi wa kila namna, ili chochote ambacho rais anakizungumza, lazima kiwe cha kweli na cha uhakika na jambo lolote rais analosema ni tamko, linafuatiwa na utekelezaji tuu, ndio maana rais alipozungumza tuu kuhusu sofa, kukapelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuonekana sio mwaminifu na wengi wakataka atumbuliwe!.

Baada tuu ya kuibuka kwa kashfa hii ya makontena na TRA kuweka kodi kubwa ya milioni 60 kila kontena, kukajenga picha, kilichomo ndani ya makontena hayo ni vitu vya thamani kubwa sana, hivyo ilitegemewa kabla rais wetu, hajazungumza lolote, ilmbidi kwanza ajiridhishe kwanza, kupitia jicho lake ndani ya TRA, liwasilishe hayo makisio ya kodi mezani kwake, na jicho lake ndani ya Mamlaka ya Bandari, TPA, kumfikishia rais wetu taarifa za the bills of landing sambamba na kile halisi kilichokutwa ndani ya makontena yale, na wale jamaa zetu, kupeleka taarifa makontena ni ya nani haswa, na baada ya kujiridhisha, ndipo rais wetu, angetoa tamko kama lile na mfano wa masofa kwa kuzungumzia vitu halisi na vya uhakika.

Jana kwenye mnada, makontena yote 20, yamefunguliwa na kuonyesha vilivyomo ni samani tuu tena used, ambavyo thamani ilizidi milioni 20 kila container, nitashangaa, TRA wao wanataka milioni 60 kwa kila container na hakuna sofa!.

Ila hata kwa kuiangalia tuu hii picha ya sofa, huhitaji kuwa na jicho tunduizi kubaini haikupigwa kwenye contena, bali imepigwa dukani!. Sasa rais wetu anapozungumzia vitu vya uongo wa mitandao, kunamshushia hadhi ya umakini mhe. rais wetu, hivyo maofisa responsible watimize wajibu wao na huyu aliyeposti picha hii, atafutwe popote alipo na kufunguliwa sio tuu mashitaka ya kawaida ya kuposti taarifa ya uongo kwenye mitandao, bali na mashitaka ya uchochezi wa kumchonganisha Makonda na rais wetu na wananchi wake just kwa kuposti picha tuu iliyosababisha balaa lote hili hadi rais atoe tamko ambalo limekuja kutokea kuwa sii kweli, hivyo kufanya jambo lolote litakaloweza kumpotosha rais wa JMT, ikiwepo kuposti uongo uliomfanya rais kuuamini huo uongo akidhani ni kweli, ni kosa la jinai!.
Mnunuzi Makontena ya Makonda afunguka "Sijaona Masofa" - Video

Hitimisho.
Nauendeleza ule ule wito wangu kwa wasaidizi wa rais,
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums

Ili nisichukiwe na wasaidizi wa rais, nawahakikishia kuwa
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila... - JamiiForums

Paskali

Kaka Paskali kuna mambo kadhaa ambayo naamini umeacha kuyajadili kwa makusudi ktk bandiko lako.
1. Mh. Rais alipata wapi taarifa za uwepo was sofa ndani ya makontena?. Ni kutoka ktk scanner za bandari, taarifa toka ktk taasisi maalum au taarifa za mitaani?
2. Kama taarifa za mitandaoni zimempotosha mkuu, nani awe wakwanza kuchukuliwa hatua, wasaidizi wake au alieweka picha za sofa za show room?
3. Uwiano wa Ujazo wa bidhaa ndani ya makontena na uhalisia wa upakiaji (kwa uzoefu wa wasafirishaji)
4. Idadi ya makontena iliyotajwa mwanzo (zaidi ya 20), na yale yaliyotajwa kuhusika na mnada uliotangazwa na tra.
.............
Kwa uchache!...
 
Maana picha zinaonesha makasha yako na mizigo nusu nusu. Kweli dayasupora ndio wasio juu kubana matumizi hivyo? Wakati fedha yao wanaipata kwa mbinde kwelikweli hata kwa kubeba boxes wakati mwingine. Walete mzigo wa kutosha makasha 4 katika makasha 20? Haingii akilini. Mbaya zaidi mkuu wa dola anataka kuvuliwa nguo hadharani kuwa ni muongo. Huu mchezo ni hatari sana jamani, oowi!!
 
Ngoma ikivuma sana......!!
 
Wanabodi,

Kwa vile kuposti picha ya uongo kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kupotosha jamii, ni kosa la jinai,

Natoa wito kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, kumtafuta mtu aliyepost picha hii na kueleza ni moja ya vilivyomo ndani ya makontena ya Makonda, kitu ambacho sii kweli.
View attachment 854767
Kufuatia picha hii, kuna wengi wamehadai ka kwa kudhani ni kweli sofa ni miongoni mwa vitu vilivyomo kwenye Makontena ya Makonda, hali iliyopelekea hata rais wa Jamhuri ya Muungano, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kushangaa kama waalimu wamehitaji sofa?!, na kueleza inawezekana ni makontena mawili matatu tuu ndiyo yatapelekwa shule, halafu mengine yakaishia shopping malls.

Kufuatia baadhi ya matamshi ya rais wetu, yanathibitisha baadhi ya wasaidizi wa rais, hawamsaidii rais wetu kwenye public, kunakopelekea kumwacha rais kutamka baadhi ya vitu ambavyo haviko sahihi, kitu ambacho kwa namna moja au nyingine, ama kunaifedhehesha taasisi ya urais, au kumfedhehesha rais wetu kuonekana ni mtu anayesema lolote bila kuwa na uhakika, kitu ambachho sio kizuri kwa rais wetu.

Rais wetu anategemewa kuwa very perfect, ndio maana amewekewa wasaidizi wa kila namna, ili chochote ambacho rais anakizungumza, lazima kiwe cha kweli na cha uhakika na jambo lolote rais analosema ni tamko, linafuatiwa na utekelezaji tuu, ndio maana rais alipozungumza tuu kuhusu sofa, kukapelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuonekana sio mwaminifu na wengi wakataka atumbuliwe!.

Baada tuu ya kuibuka kwa kashfa hii ya makontena na TRA kuweka kodi kubwa ya milioni 60 kila kontena, kukajenga picha, kilichomo ndani ya makontena hayo ni vitu vya thamani kubwa sana, hivyo ilitegemewa kabla rais wetu, hajazungumza lolote, ilmbidi kwanza ajiridhishe kwanza, kupitia jicho lake ndani ya TRA, liwasilishe hayo makisio ya kodi mezani kwake, na jicho lake ndani ya Mamlaka ya Bandari, TPA, kumfikishia rais wetu taarifa za the bills of landing sambamba na kile halisi kilichokutwa ndani ya makontena yale, na wale jamaa zetu, kupeleka taarifa makontena ni ya nani haswa, na baada ya kujiridhisha, ndipo rais wetu, angetoa tamko kama lile na mfano wa masofa kwa kuzungumzia vitu halisi na vya uhakika.

Jana kwenye mnada, makontena yote 20, yamefunguliwa na kuonyesha vilivyomo ni samani tuu tena used, ambavyo thamani ilizidi milioni 20 kila container, nitashangaa, TRA wao wanataka milioni 60 kwa kila container na hakuna sofa!.

Ila hata kwa kuiangalia tuu hii picha ya sofa, huhitaji kuwa na jicho tunduizi kubaini haikupigwa kwenye contena, bali imepigwa dukani!. Sasa rais wetu anapozungumzia vitu vya uongo wa mitandao, kunamshushia hadhi ya umakini mhe. rais wetu, hivyo maofisa responsible watimize wajibu wao na huyu aliyeposti picha hii, atafutwe popote alipo na kufunguliwa sio tuu mashitaka ya kawaida ya kuposti taarifa ya uongo kwenye mitandao, bali na mashitaka ya uchochezi wa kumchonganisha Makonda na rais wetu na wananchi wake just kwa kuposti picha tuu iliyosababisha balaa lote hili hadi rais atoe tamko ambalo limekuja kutokea kuwa sii kweli, hivyo kufanya jambo lolote litakaloweza kumpotosha rais wa JMT, ikiwepo kuposti uongo uliomfanya rais kuuamini huo uongo akidhani ni kweli, ni kosa la jinai!.
Mnunuzi Makontena ya Makonda afunguka "Sijaona Masofa" - Video

Hitimisho.
Nauendeleza ule ule wito wangu kwa wasaidizi wa rais,
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums

Ili nisichukiwe na wasaidizi wa rais, nawahakikishia kuwa
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila... - JamiiForums

Paskali

Kwa sasa, Paskali mwananzengo hakuna taasisi ya urais Tanzania kuna Magufuli ndiyo kila kitu period. Kwa hiyo si rahisi na hakuna sheria ya kumshauri Magufuli asije akapangiwa mpakwa mafuta haguswi. Imebaki kwetu kuchagua mbivu na mbichi.
 
Ndio hivyo mkuu, hii sinema bado mbichi ,
Mkwepa Kodi ni mhujumu uchumi
Tatizo braza ake anambeba mno
FB_IMG_1535809388103.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
In politics,malaika anaweza kugeuzwa shetani na shetani anaweza kupambwa akafanana na malaika! Ila ukweli halisi ni kuwa hii issue inashadadiwa zaiidi na maadui wa makonda kuliko uhalisia wa issue yenyewe. Makonda aliomba tax exemption, issue ilikuwa ni kumkatalia tu basi, lkn imefanywa kisiasa zaidi.

Mchukieni makonda kwa mabaya yake BT kumbukeni na mazuri yake pia
 
Pascal mkorofi, kwa ujumbe wako uliojificha, kama kawaida yako utawafikia/utamfikia.ila hawata jali kwa sababu wengi bado hakujakucha.
 
In politics,malaika anaweza kugeuzwa shetani na shetani anaweza kupambwa akafanana na malaika! Ila ukweli halisi ni kuwa hii issue inashadadiwa zaiidi na maadui wa makonda kuliko uhalisia wa issue yenyewe. Makonda aliomba tax exemption, issue ilikuwa ni kumkatalia tu basi, lkn imefanywa kisiasa zaidi.

Mchukieni makonda kwa mabaya yake BT kumbukeni na mazuri yake pia
Kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona watu wazima na akili zenu mnajadili kitu kidogo mnaacha hoja yenyewe?
Swala hapa sio kuna nini ndani bali kuna mhuni mmoja kaleta makasha yake bila kufata sheria na akawa analazimisha kuyatoa bila kulipia ushuru.
Kwanini mjadili sijui ndani kulikuwa na nini na kutaka kumsafisha Makonda? Tujadili kwanini aliamua kuleta makasha 20 kwa jina lake na kutaka kuyatoa kwa kisingizio ni msaada ambao kwa mujibu wa sheria zetu yeye sio miongoni mwa watu wanaoweza kupata msamaha wa kile kinachoitwa msaada.
Kwanini mnatumia nguvu nyingi sana kumsafisha Makonda wakati Rais ashasema kodi ilipwe.
Mnataka kumuona Rais mjinga wakati yeye hakuwa akizungumzia yaliyomo ndani ila alizungumza kama mfano tu wa vitu ambavyo vikiachwa viende kimazoea kuna wafanyabiashara watatumia mwanya huo kujiingizia bidhaa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ndilo limenifanya nimshangae Pascal Mayalla...yaani hana tatizo kuwa yupo fisadi moja mhuni kaingiza nchini bidhaa na kakwepa kulipa kodi, anataka TCRA imchukulie hatua aliyeweka picha ya makochi mtandaoni, complete rubbish! Eti picha! Haumii kwamba taifa linakosa mapato, ghadhabu yake ni picha kuwekwa mtandaoni.

Mimi hapa najiuliza ni nani hao huko diaspora fisadi huyo alishirikiana nao kula njama ya kutuibia wananchi na kuhujumu taifa, watu wanahangaika na picha! Kama nilivyosema awali hii ni filamu iliyotengenezwa na wajanja kututoa kwenye maovu tunayotendewa Watanzania katika awamu hii ya tano na watu wanakubali tu maelezo ya kihuni.
 
Huwezi kujua MKUU, huenda hata aliyepost hiyo picha ni sehem ya hii sinema. Lakini ilitakiwa hatua kali zichukuliwe kwa upotoshaji tena iwe funzo kwa wengine pia.
Aliyehutubia Taifa akisema Kuna sofa mmemfanya nini? Mnaanza sarakasi wakati maneno mmeyaanzisha wenyewe? Haya yote kayataka Magufuli hadi mnaanza kupata ujasiri wa kuhoji. Angemtumbua mtu wenu mapema kusingekuwa na vimaneno vya kike kama hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom