TCRA, mtafuteni aliyechomekea picha hii ashitakiwe kwa upotoshaji!. Watu wataaibika na kuonekana hawana maana!.

Wanabodi,

Kwa vile kuposti picha ya uongo kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kupotosha jamii, ni kosa la jinai,

Natoa wito kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, kumtafuta mtu aliyepost picha hii na kueleza ni moja ya vilivyomo ndani ya makontena ya Makonda, kitu ambacho sii kweli.
View attachment 854767
Kufuatia picha hii, kuna wengi wamehadai ka kwa kudhani ni kweli sofa ni miongoni mwa vitu vilivyomo kwenye Makontena ya Makonda, hali iliyopelekea hata rais wa Jamhuri ya Muungano, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kushangaa kama waalimu wamehitaji sofa?!, na kueleza inawezekana ni makontena mawili matatu tuu ndiyo yatapelekwa shule, halafu mengine yakaishia shopping malls.


Kufuatia baadhi ya matamshi ya rais wetu, yanathibitisha baadhi ya wasaidizi wa rais, hawamsaidii rais wetu kwenye public, kunakopelekea kumwacha rais kutamka baadhi ya vitu ambavyo haviko sahihi, kitu ambacho kwa namna moja au nyingine, ama kunaifedhehesha taasisi ya urais, au kumfedhehesha rais wetu kuonekana ni mtu anayesema lolote bila kuwa na uhakika, kitu ambachho sio kizuri kwa rais wetu.

Rais wetu anategemewa kuwa very perfect, truthful na very accurate, ndio maana amewekewa wasaidizi wa kila namna, ili chochote ambacho rais anakizungumza, lazima kiwe cha kweli na cha uhakika na jambo lolote rais analosema ni tamko, linafuatiwa na utekelezaji tuu, ndio maana rais wetu tumemuwekea kinga ya kutokushitakiwa kwa mimaajili kuwa rais wetu hawezi kufanya kosa, na rais kuhusu kitu chochote, jicho kitu ni lazima kiwe cha kweli, truthful na accurate, hivyo alipozungumza tuu kuhusu sofa, kukapelekea watu wote kuamini alichokisema rais ni ukweli mtupu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuonekana sio mwaminifu na wengi wakataka atumbuliwe!.

Baada tuu ya kuibuka kwa kashfa hii ya makontena na TRA kuweka kodi kubwa ya milioni 60 kila kontena, kukajenga picha, kilichomo ndani ya makontena hayo ni vitu vya thamani kubwa sana, hivyo ilitegemewa kabla rais wetu, hajazungumza lolote, ilmbidi kwanza ajiridhishe kwanza, jee yote yanayosemwa ni kweli?, kwake ni simple, rais ana jicho refu linaloona kila kona, hivyo kupitia jicho lake ndani ya TRA, lilipaswa liwasilishe hayo makisio ya kodi mezani kwake, na jicho lake ndani ya Mamlaka ya Bandari, TPA, kumfikishia rais wetu taarifa za the bills of landing sambamba na kile halisi kilichokutwa ndani ya makontena yale kabla hayafunguliwa kupita taarifa za scanner, kisha kufanyiwa verification kwa kuyafungua na kuweka seal za TRA, na wale "jamaa zetu", kupeleka taarifa makontena ni ya nani haswa, na baada ya kujiridhisha, ndipo rais wetu, angetoa tamko kama lile na mfano wa masofa kwa kuzungumzia vitu halisi, vya ukweli na vya uhakika!.

Jana kwenye mnada, makontena yote 20, yamefunguliwa na kuonyesha vilivyomo ni samani tuu tena used, ambavyo thamani ikizidi milioni 20 kila container, nitashangaa!, kwa sababu containers nyingine zina mazagazaga tuu, hata mtu akilipa milioni ni bahati, lakini TRA wao wamekadiria kodi ya milioni 60 kwa kila container regarless kilichopo ni nini!, tais wetu katutangazia kuna sofa, halafu hali halisi, hakuna sofa!.

Ila hata kwa kuiangalia tuu hii picha ya sofa, huhitaji kuwa na jicho tunduizi kubaini haikupigwa kwenye contena, bali imepigwa dukani!. Sasa rais wetu anapozungumzia vitu vya uongo wa mitandao, kunamshushia hadhi ya umakini mhe. rais wetu, hivyo maofisa responsible watimize wajibu wao na huyu aliyeposti picha hii, atafutwe popote alipo na kufunguliwa sio tuu mashitaka ya kawaida ya kuposti taarifa ya uongo kwenye mitandao, bali na mashitaka ya uchochezi wa kumchonganisha Makonda na rais wetu na wananchi wake just kwa kuposti picha tuu iliyosababisha balaa lote hili hadi rais atoe tamko ambalo limekuja kutokea kuwa sii kweli, hivyo kufanya jambo lolote litakaloweza kumpotosha rais wa JMT, ikiwepo kuposti uongo uliomfanya rais kuuamini huo uongo akidhani ni kweli, ni kosa la jinai!.
Mnunuzi Makontena ya Makonda afunguka "Sijaona Masofa" - Video

Huyu jamaa ni shuhuda wa vilivyomo ndani ya makontena, aliyekagua makontena yote 20 ya Makonda, na hakuona sofa yoyote.
Hitimisho.
Nauendeleza ule ule wito wangu kwa wasaidizi wa rais,
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums

Ili nisichukiwe na wasaidizi wa rais, nawahakikishia kuwa
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila... - JamiiForums

Paskali

Keep it up uDC unakuja km Jerry muro
 
Mr Mayala ##sory mi nina iman kuwa unakumbukumbu nzuri kabisa kuhusu kauli za muheshimiwa sana a.k.a(pombe)hivi hao washauri wake unafikiri hawapendi kuwa washauri pasipo ushauri??🤷🏿‍♂️
 
Kama picha hiyo ilichomekwa tu, mwenye mkoa wake ambaye pia ni mpakwa mafuta angekuwa alishaingiza watu wake kazini kumtafuta huyo mtu na kumshughulikia. Rais wetu mpendwa na makini sana, ambaye amesimika vyombo vyake vya udukuzi kila kona ya Nchi hii alikwambia mule ndani kulikuwa na masofa - most of them meant to end up in shopping malls. Unataka TCRA wapingane nae? Never.
 
Yona wanacheza mchezo why huo
Paskali, hii movie naona unataka kuichokonoa. Hii inaweza kuwa drama aje aseme hakuna masofa. Sidhani kama kuna mtu wa kuthubutu kumdanganya John, ni michezo inachezwa kuwa hapakuwa na masofa. Trekta je? halikuwemo?
Yona wanacheza mchezo mchafu kudanganya jamii, inakuwaje kwa maneno yake mwenyewe yule mama kuwa wayachanganye makontena ya Makonda na makontena ya watu wengine halafu wapige mnada mmoja na je huyo alietoka akasema yeye ameona hayo makontena hayana masofa na vifaa vyengine vyenye thamani alifanya counter check kuona kama namba za containers zinazopigwa mnada zinalingana na namba zilizomo katika Bill of Lading?

Na kuna utata mwengine baadhi ya makontena yanaonekana yana upungufu wa ujazo hasa yale ya HC 40ft. ivi inaingia akilini kuwa mwenye hiyo mizigo na msafirishaji hizo kontena zije na ujazo huo kwa gharama zote hizo? Isitoshe mfano na hivyo vitu vilivyomo havionekani kama ni Ameican products hasa hivyo vitu vya kilimo including Matrekta yanaonekana kabisa kama ni bidhaa za China na sehem nyengine ukifanya zoom ya picha unaona kabisa maandishi ya kichina.

Pascal unakumbuka siku zile Mkulu aliposema wewe una njaa.
Kama una uchungu usiogope nenda kamwambie Mkulu kuwa Makonda is not above the law kama amewaondoa kina Mwigulu na Makonda amwajibishe kwa kumvua madaraka.
 
Back
Top Bottom