chanaga
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 344
- 190
Habari na poleni na msiba wa Mzee Mengi,bila kupoteza muda niende kwenye mada;malipo ya mwezi ya kisumbusi changu kilikwisha jana 8.5.2019 lakini kutokana na usawa bado unabana bado sijapata pesa ya kulipia (subscribe) lakini tangu jana startimes wananiletea message kwenye uso wa runinga yangu kila baada ya dakika 5 yaani hata kwa zile channel za bure unashindwa kuangalia hata taarifa ya habari,naomba tcra uchukue hatua haraka sana dhidi ya hawa startimes hasa kwa hizi channel za bure kama ni kukumbusha wanitumie sms 1 tu kwa njia ya simu,nawakilisha.
