GE2025 TCRA: Masuala ya uchaguzi siyo kama kutangaza mpira, waandishi hakikisha hujatia chumvi au kusisitiza vitu ambavyo havipo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, amewataka watangazaji na waandishi wa habari nchini kuepuka kuonesha mitazamo yao binafsi au kuongeza “chumvi” wakati wa kuripoti Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza tarehe 16 Agosti 2025 katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Kaskazini uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Kisaka alieleza kuwa uripoti unaopindishwa au kuakisi mtazamo binafsi wa mwandishi unaweza kupotosha umma na kudhoofisha imani kwa vyombo vya habari.

“Katika kipindi chote cha uripoti wa matangazo ya uchaguzi, mtangazaji haruhusiwi kuonesha mtazamo wake binafsi. Kuongeza chumvi ni jambo ambalo linatupata sana. Kumbuka, masuala ya uchaguzi siyo kama kutangaza mpira. Hakikisha hujatia chumvi au kusisitiza vitu ambavyo havipo,” alisema Kisaka.

Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano wa TCRA, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB). Pia uliambatana na mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo wahariri, watangazaji na maafisa wa polisi kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara. Mada kuu zilihusu pamoja na zingine, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa za mwaka 2020.

Chanzo: Jambo
 
Daaah tayaariii!!!😔😔😢
 
Tutaona kama TBCCM mtaiambia hivyo.
 
Ila Kuna waandishi wapuuzi tcra haiwaoni

Screenshot_20250801-225228~2.jpg
 
Back
Top Bottom