TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za muda huu wanajamvi? Pasi shaka mu bukheri wa afya kabisa...lengo la Uzi huu ni hiki kipindi cha tega nikutege cha Chanel ya TV1. Hakika nimekiangalia mara mbili nikasikitika kabisa kwa maudhui ya kipindi kile ambacho kwangu niliweka katika makundi kadhaa
1) Udhalilishaji: hata kama ni utandawazi na kwenda na wakati lakini hii ni too much kwani ni Udhalilishaji mkubwa wa mila, tamaduni na desturi zetu. Yaani kujipeleka pale kwaajili ya kujichukulia mchumba ni Udhalilishaji wa hali ya juu
2) Kuchochea ngono: Yaani bila kupindisha kauli kipindi hiki kinahalalisha ngono kwenye jamii kwani mtu anakuja anajichagulia wake wanaenda kuspend muda "date", hakuna utofauti na madanguro mtu anaenda kujichagulia wake wa kula nae bata
3) Upotoshaji: ukiwasikiliza hao wanaoenda kusaka mwandani wanajinadi kuwa wafanyabiashara, mamodo, wanavyuo au vyovyote, mwandani hapatikani kwa njia za namna ile badala yake ni kuipotosha jamii. Kwangu naona kama maigizo kwani kwa kuanzia inawezekana wanawatafuta watu waje kuigiza kama wanatafuta mwandani na kupata ili kuwavuta mazezeta wajitokeze.
Nilienda kumsalimia shemeji yangu nikasikia mabinti wawili magomeni inaonekana wameshindikana kitabia mtaani kwao, wakawa wanajadili kwamba wataenda kwa lengo la kuonekana wanatafuta mwandani kisha wakipata wanaspend muda na hela za huyo mtu kisha kila mtu aende njia yake.
Kipindi kinavunja miiko ya kitanzania kabisa na kujenga mind za watoto wetu ziharibike tangu wapo wadogo. Utandawazi unazidi kuimomonyoa Tanzania yetu, juhudi za ziada zisipoonekana tutapoteza kila kitu kwa tamaduni za magharibi.

TV1 na TCRA tuondoleeni hiki kipindi.
Kuna kipindi kinaitwa tega nikutege. Kipo TV1. Kinarushwa Jumapili kuanzia saa mbili.
Kwamba wanachukukiwa makahaba wanakuja kugombaniwa na vijana kwa njia ya kujibu maswali. Mshindi anapewa offer ya kwenda kulala na huyo kahaba kwenye hoteli atakayopenda! Kwa hiyo kila wiki vijana watagombania nafasi hii. Tulipofika sasa si sawa! Kwa hiyo TV1 na TCRA mko radhi na huu upuuzi wenye lengo la kutuharibia taifa? Wazazi tutakaaje na watoto wetu kuwafundisha maadili ikiwa taasisi zetu zinakubaliana na huu ukiukwaji wa maadili? Tuungane kwa nguvu kukemea huu upuuzi. TV1 na TCRA ondoeni hicho kipindi!
Tafadhali sambaza ujumbe huu kadiri uwezavyo!
Naanza kwa kuwapa pole wale wote waliopatwa na msiba wa tcra,poleni sana.
Mliopo nn mtakaokuja naamini muwazima wa afya na poleni na hongereni kwa kujenga taifa huru ila linalohitaji kukombolewa.
Hoja yangu ni hii na ninaoma mnisaidie maana yake mimi nimeshindwa kuelewa.
Hiki kipindi cha "Tega ni kutege"kinachorushwa tv 1 kila ijumaa saa 3:30 usiku.
Kinafundisha nini hasa na lengo lake hasa ni nini?nimeshindwa kukielewa nisaidieni wapendwa.
Je kina ulazima kuonyeshwa au kurushwa hewani?