TCRA imeyashindwa Makampuni ya Simu?

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
16,359
22,516
Inaonekana makampuni ya simu yana nguvu sana kushinda mamlaka ya mawasiliano.Kwa wale wanaotumia mtandao wa zantel nafikiri watakuwa wanaelewa, jana nimeweka bando la siku saa nne usiku kufika saa tatu leo inaonyesha bando langu lime expire.Nikajaza tena bando saa tatu usiku ikaja ujumbe kuwa kesho saa moja na dakika 44 bando limeisha nikawapigia customer care wa zantel walichonijibu hawaoni kumbukumbu zangu nilivyoweka bando lakini wakashindwa kunieleza kwanini bando lao la siku ni chini ya masaa 24.

Nikaamua niingie kwenye tovuti ya TCRA ili nijaze malalamiko online nilichokutana nacho ni aibu kwani ukifungua fomu haifunguki hii ndio mamlaka ya mawasiliano lakini tovuti yao haifanyi kazi vizuri.
 
Mkuu hayo ni majipu. Pamba na mikasi(ganzi hakuna) vimeshaandaliwa, wako folenini hao!
 
Wasisubiri mpaka watumbuliwe jipu Juzi bosi wao kagusua wakati anazungumza kwenye Uwekaji wa jiwe la msingi la barabara ya Holili-Taveta (EAC ).
Wajirekebishe!
 
Makapuni yote ya sim ya hapa tz ni majambazi
Nili waamini sana Voda lakini sio wale tena loooh! jamaa wame change wanapiga vibaya bila soni, kifurushi cha internet cha siku 30 (25,000/-) kilifutwa ndani ya wiki moja tu,inapo zungumziwa TCRA kwenye mambo kama haya mimi siwaoni kabisa na imani yangu ni haba kwao, maana wakiita ushahidi wa watu walio jeruhiwa na haya makampuni pengine ni mamia na teknoloji ya ufuatiliaji nina imani wanayo ila kuna nini katikati ya huu mchezo ni siri yao.
 
Na ninyi muwe mnaangalia mitandao ya kutumia.....

Mitandao mingine netwek inapatika HQ office za mtandao husika tuu
 
Hata ukiwapigia kwenye simu zao unajibiwa 'Namba hiyo haipo'! Hahaaah!
 
Mamlaka zimeshindwa, labda kampuni zote za simu ni wafadhili wa CCM. Nafikiria kuanzisha kitu kama the Arab Spring. Maandamano ya wananchi kila siku kwenye ofisi zote za haya makampuni. Labda watapata message sent.
 
Vita kama hii mteja mmoja mmoja kushinda ni ngumu sana serikari ya Tanzania inatumia karibu nusu ya makusanyo ya kodi kulipa mishahara na taasisi mojawapo inayofaidika ni hii 'Fair Competition Commission' hawa jamaa sijui wanafaida gani wanapatikana kwenye hii link Fair Competition Commission kwa maelezo ya shughuli zao kwa mujibu wa sheria iliyofanya wawepo in the first place.

Hawa FCC ndio wanaotakiwa kuhakikisha si ubora wa bidhaa tu ata terms za matangazo ya kibiashara zinamlinda mlaji kutokana na kile kinachokuwa offered na anachopewa pamoja na mambo mengi ya consumer protection.

Kila siku watu wanalalama it as if sheria hakuna na kama hazipo kwanini wasifanye copy and paste kama ilivyo desturi zao mtu awezi kukufanya ununue bidhaa kwa matangazo yake halafu asikupe kile ambacho ame ki-express that is just not right na haya malalamiko yamekuwa ya muda mrefu sana sasa bora hiyo taasisi ifutwe kama awawezi kuchukua hatua stahiki na kutoa adhabu kuliko kuvuna tu hela za walipa kodi.

http://www.competition.or.tz/public_notes/Standard_ Form_ CONSUMER CONTRACTS_ Regulations_2014.pdf
 
Jaman TCRA mko wapi yani natumia mtandao wa Tigo yaan ma msg yanajirudia mara kumi kumi kwa muda tofaut tofaut yan msg 1 inajirudia mara kibao had usumbufu jaman wenye mtandao hamuoni haya matatizoo? Hamjui mnaweza kuvunja ndoa za watu n.k? Ashum mchepuko umekutumia msg ukaipata ukaisoma ukaifuta eti umelala usiku ile ile msg inaingia tena na sio mara moja kama mar kumi hiv daah jaman fanyen service haya mambo yaishe bas hapa msg za tang jana zinaingia tu had mda huu na jana nilikwisha zisoma, nadhan ni mpya kumbe zimejirudia aah
 
Mimi nimetumiwa sms asbui mpaka sa hizi za kujirudia zmeshafika 50..
 
Inaonekana makampuni ya simu yana nguvu sana kushinda mamlaka ya mawasiliano.Kwa wale wanaotumia mtandao wa zantel nafikiri watakuwa wanaelewa, jana nimeweka bando la siku saa nne usiku kufika saa tatu leo inaonyesha bando langu lime expire.Nikajaza tena bando saa tatu usiku ikaja ujumbe kuwa kesho saa moja na dakika 44 bando limeisha nikawapigia customer care wa zantel walichonijibu hawaoni kumbukumbu zangu nilivyoweka bando lakini wakashindwa kunieleza kwanini bando lao la siku ni chini ya masaa 24.

Nikaamua niingie kwenye tovuti ya TCRA ili nijaze malalamiko online nilichokutana nacho ni aibu kwani ukifungua fomu haifunguki hii ndio mamlaka ya mawasiliano lakini tovuti yao haifanyi kazi vizuri.
Mkuu na sio Zantel tu huu mchezo upo sana kwenye makampuni yote hasa unapoweka bundle usiku,mimi mwenyewe nimewahi kuweka Airtel bundle hata sijaperuzi ikawa inasema bundle imeisha imetokea zaidi ya mara moja,hata Tigo na Vodacom ni vivyo hivyo
 
Vodacom ndiyo jizi kubwa. Ukiwa na balance ya elfu mbili kamili haikuruhusu kuweka bundle ya elfu mbili. Inasema hela haitoshi. Nia uweke pungufu na hela inayobaki hutajua imeenda wapi
 
Vodacom ndiyo jizi kubwa. Ukiwa na balance ya elfu mbili kamili haikuruhusu kuweka bundle ya elfu mbili. Inasema hela haitoshi. Nia uweke pungufu na hela inayobaki hutajua imeenda wapi
Jana imetokea nikaripoti TCRA unaweza check link hapo juu. Ila jamaa kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea. TCRA siwaelewagi kabisa. Wangefanya kazi yao kwa weledi tungekuwa na raha sana nchi hii
 
Jana imetokea nikaripoti TCRA unaweza check link hapo juu. Ila jamaa kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea. TCRA siwaelewagi kabisa. Wangefanya kazi yao kwa weledi tungekuwa na raha sana nchi hii
Angalau Airtel pamoja na matatizo yao hili hawana. Inauudhi sana salio liko lakini inakataa
 
Nimefurahishwa mno na hii bodi ya TCRA kuvunjwa! Go! Magufuli Go! Tumbua kabisa tutaanza kuheshimiana mtaani sasa
 
Attachments

  • IMG-20160426-WA0013.jpg
    IMG-20160426-WA0013.jpg
    68.8 KB · Views: 49
Back
Top Bottom