Masulupwete
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 2,366
- 2,435
Unanunua bando la wiki nzima la kifurushi cha internet labda bando la shilingi 3,000 unapewa 400MB (kwa mtandao naotumia mimi).
1. Mosi, hilo bando uliloambiwa ni la wiki litadumu kwa siku 6 kamili, badala ya kudumu kwa siku 7. Wenzetu hawa sijui wiki ina siku 6, au hizi siku wao wanazihesabu kwa staili gani, sielewi.
2. Pili, ukishanunua hilo bando sasa, ndo mziki unaanza sasa. Wanazikatakata/gawanya hizo bando; kuna MB wanazipeleka watsap (bila kujali kama wewe unatumia hiyo watsap au hutumii), zingine fesibuku (hivohivo hawajali upo huko fesibuku au haupo), zinazobaki ndio unaingiziwa bando la kawaida la kutumia kwenye internet.
Matokeo yake unapata mb chache sana kwa ajili ya internet na unatumia kwa siku hizo 6 badala ya 7.
Huu ni uzulumati wa mchana kweupe. Hivi TCRA mnayaona haya au hadi tuje huko maofisini kwenu kupanga foleni kuwaelezea haya?
Nyinyi sio watumiaji wa huduma hizi hamuoni upuuzi huu unaofanywa kwa watumiaji au mnasubiri jpm awatumbue?