TCIB yakoshwa na NEC, yaikabidhi cheti

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797



08 MAY 2012

Na Agnes Mwaijega

KITUO cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), kwa mara ya kwanza kimeikabidhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) cheti cha usimamizi bora wa uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Ofisa Utawala TCIB, Bi.Deborah Mushi, alisema pamoja na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi huo, bado NEC ilijitahidi kusimamia uchaguzi huo vizuri.


Bi. Mushi alisema kwa mujibu wa ripoti yao ya utafiti uliofanyika wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi, NEC iliendesha uchaguzi ambao ulikuwa huru na haki.

"Kwa asilimia 70 NEC ilijitahidi kufanya kazi yake vizuri na ndiyo maana tumeamua kuipa cheti maalumu cha usimamizi mzuri katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki," alisema.

Hata hivyo alitoa mwito kwa tume hiyo kuhakikisha inachukua hatua kali dhidi ya wale wote waliotumia lugha ya matusi katika kampeni za uchaguzi huo.

"Mimi nadhani kwa upande mwingine ni wajibu wa NEC kuhakikisha inaajiri watendaji wengi watakaosimamia suala la maadili katika chaguzi kwa ngazi zote za serikali kuanzia kata hadi taifa," alisema.

Alisema kuna umuhimu wa Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa elimu endelevu kwa wasimamizi wa masuala ya uchaguzi kwa kuanzisha vipindi maalumu kwa ajili ya mafunzo na si kusubiri hadi wakati wa uchaguzi.

Bi. Mushi alitoa mwito kwa Serikali na NEC kuhakikisha zinatoa ruzuku inayostahili kwa vyama vyote vya siasa ili viweze kushiriki kikamilifu katika chaguzi.

Kwa kipindi kirefu NEC imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kusimamia uchaguzi. Hatua ya NEC kupata cheti hicho inatafsiriwa kuwa inachangiwa na uongozi mpya wa tume.










 
Lakini bado tunahitaji tume huru ya Uchaguzi kabla ya Mwaka 2015
 
Baada ya CDM kuwakomalia kisawasawa walifanya kweli. Hata mimi nawapongeza kwa kusalimu amri na kufanya kazi sawasawa Arumeru.
 
Back
Top Bottom