Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,601
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua kampeni maalum inayolenga kuwawezesha Watanzania kufikia ndoto zao kwa kuwapatia suluhisho sahihi za kifedha, hatua inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ustawi wa jamii.
Kampeni hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa makundi mbalimbali ya wananchi, hususan wajasiriamali, wakulima na biashara ndogo na za kati, kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kupanua fursa za ajira nchini.
Your browser is not able to display this video.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Machi 18, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TCB Bank, Kaimu Mkurugenzi Jema Msuya, amesema benki hiyo imejipanga kuwa mshirika wa maendeleo kwa wateja wake kwa kuwapatia huduma zinazokidhi mahitaji yao na kusaidia kufanikisha malengo ya kifedha.
“Tunataka kuwa karibu na wateja wetu na kuhakikisha kila Mtanzania anapata msaada wa kifedha unaomwezesha kufikia ndoto zake,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa TCB Bank, Alex Dwashi, amesema kampeni hiyo inalenga kujenga uhusiano wa karibu na wateja kwa kuelewa changamoto zao na kutoa suluhisho mahsusi yatakayosaidia kukuza shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali.
“Kampeni hii inalenga kugusa maisha ya Watanzania moja kwa moja kwa kuwaunga mkono katika safari ya kukuza shughuli zao za kiuchumi,” amesema.
Your browser is not able to display this video.
Naye Meneja Mwandamizi wa TCB Bank, Al-Amin Lwano, amesema benki hiyo itawafikia moja kwa moja wajasiriamali katika maeneo yao ya biashara ili kuwapatia mikopo na huduma nyingine za kifedha zitakazosaidia kuongeza mtaji na kuboresha uzalishaji.
“Tutaenda karibu na wafanyabiashara ili kuwasaidia kukuza biashara zao na kuchochea uchumi wa nchi,” amesema.
Your browser is not able to display this video.
Ameongeza kuwa uwezeshaji wa wananchi kupitia sekta ya fedha ni nyenzo muhimu ya kukuza uchumi endelevu, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kuchangia maendeleo ya taifa kwa ujumla.