TBS yaamka usingizini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBS yaamka usingizini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Escobar, Jun 21, 2012.

 1. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 60
  SIKU chache baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda kuiagiza Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake Charles Ekelege, shirika hilo limetangaza kampuni zilizopewa kazi ya kukagua magari yanayotoka nje ya nchi.

  Mapema mwezi uliopita Dk Kigoda alitoa agizo hilo la kumsimamisha kazi Ekerege ili kupisha taratibu za kisheria ikiwamo uchunguzi kufanyika dhidi yake kutokana na madai ya TBS kuwa na ofisi hewa za ukaguzi wa magari nje ya nchi.

  Sakata la Ekelege liliibuliwa mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Deo Filikunjombe ilimtuhumu mkurugenzi huyo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye mpango wa TBS wa kukagua bidhaa nje ya nchi. Filikunjombe alieleza kuwa waligundua madudu baada ya kutembelea vituo vya ukaguzi wa magari nchini Singapore na mjini Hong Kong, China ambapo walikuta vituo hewa vya ukaguzi wa magari.

  Lakini jana, shirika hilo kupitia gazeti hili lilitoa tangazo lililotolewa na Kaimu Mkurugenzi wake mkuu, linataja kampuni zilizopewa na zilizopokonywa kazi ya kukagua magari.

  Tangazo hilo limeeleza kuwa tangu Juni 18 mwaka huu TBS imefuta leseni Na 0656 ya ukaguzi wa magari iliyokuwa ikifanywa na gereji ya Jaffar Mohammed Ali iliyopo Dubai ambayo ilikuwa ikikagua magari yanayoingizwa nchini kutoka nchi hiyo.

  "Kutokana na tangazo hili wote wanaoingiza magari kutoka Dubai wanashauriwa kupeleka magari yao kukaguliwa na kampuni ya Jabal Kilimanjaro Auto Elect Mechanical, magari ambayo yataingizwa nchini bila kukaguliwa na kampuni hii hayataruhusiwa kuingizwa katika soko la Tanzania," lilieleza tangazo hilo.

  Pia, lilieleza kuwa limefuta leseni Na 0655 ya kampuni ya WTM Utility Services ya nchini Uingereza kujihusisha na ukaguzi wa magari na badala yake magari yote kutoka nchini humo yanatakiwa kukaguliwa na kampuni ya Vehicle Operator Services Agency (VOSA).

  "Magari yatakayoingizwa nchini kutokea Uingereza bila kukaguliwa na kampuni hii ya VOSA hayataruhusiwa kuingia katika soko la Tanzania" lilieleza tangazo hilo.


  SOURCE; MWANANCHI

  Kampuni hizi zimepatikanaje? Sikuhizi kuna Mlima kilimanjaro Dubai mpaka waarabu kutumia jina lake au ni kutuhadaa tu au tayari wajanja wameshajipenyeza huko kuvuna pesa? Au ni Kilimanjaro ya kwa kina Chami?
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Bado wezi tu hawa
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 12,935
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  [h=1]About VOSA[/h] The Vehicle and Operator Services Agency (VOSA) was formed on 1[SUP]st[/SUP] April 2003 following the merger of the Vehicle Inspectorate and the Traffic Area Network division of the Department for Transport. VOSA provides a range of licensing, testing and enforcement services with the aim of improving the roadworthiness standards of vehicles ensuring the compliance of operators and drivers with road traffic legislation, and supporting the independent Traffic Commissioners…
  Transparency agenda
  Details of the Government's requirement for greater transparency across its operations.
  VOSA's vision
  Information on the agency's current vision, set in the yearly Business Plan.
  VOSA's directing board
  Information on the agency's Directors and current board structure.
  What we do
  An overview of the operational activites the agency currently does on behalf of or with the public.
  Working with the Traffic Commissioners
  Information on the activities VOSA and the Traffic Commissioners currently deliver, to help improve road safety.
  Published Information Charter[​IMG]
  A document containing information about personal data.
   
 4. O

  Original JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WTM utility ni 100% feki. Jamaa anatoa certificate akiwa pub. Hana mitambo ya ukaguzi na wala hataki kuliona gari husika.
   
 5. K

  Kalenga-Iringa JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2013
  Joined: Nov 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmm!
  kumbe,....
   
 6. a

  andrews JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2013
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,682
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  lukosi huna jipya pole sana ulifikiri utapewa wewe ulie tu maji hayapandi mlima utabaki unazunguka na pound kwenye walett
   
 7. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2013
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  sasa kwa kuwataja VOSA ina maana just ukiwa na gari yenye MOT itaruhusiwa kuingia nchini?
   
Loading...