MGONGA ULIMBO
Member
- Jun 25, 2017
- 32
- 51
HUSIKA NA KICHWA HAPO JUU. Naamini hili shirika lipo kwa ajili ya kuhakiki viwango na ubora wa kila bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi au zinazotengenezwa ndani ya nchi.
NIWAPONGEZE KWA BAADHI YA KAZI NZURI WALIZOKWISHA ZIFANYA INGAWA BADO KUNA MAPUNGUFU MAKUBWA SANA.
MAPUNGUFU KATIKA VIWANGO VYA BIDHAA KADHAA: Ni ukweli usiopingika kuwa kuna bidhaa nyingi sana mtaani ambazo hazina viwango na unakuta kabisa kuna nembo ya TBS. Je ni kweli wanakosea bahati mbaya, au ni bora twende tu mapato yaingie?
NIELEKEZE MADA KATIKA BIDHAA KUU MBILI AMBAZO NI KERO KWANGU KULINGANA NA VIWANGO.
MOJA: Helmet za pikipiki zinazoingia kutoka CHINA kila siku na zinapitia shirika la viwango kabisa na wanathibitisha kuwa zinafaa kwa ajili yakuzuia madhara pindi ajali inapotokea. NIMEKUWA NIKISHUHUDIA AJALI ZA PIKIPIKI NYINGI. Kuna ajali nyingi wahanga wangeweza kupona kwa kuwa tu na helmet imara kama wanazotumia nchi za magharibi. Kuna siku nilishuhudia ajali kinondoni watu wawili wakifa mbele yangu kwenye barabara za mwendokasi wakati mabasi hayajaanza huduma. Ziligongana pikipiki mbili moja ikitoka kinondoni studio nyingine ikitoka mkwajuni. Wahanga wa ajali hiyo walikufa kwa kupigiza vichwa chini kwenye zege la barabara ya mwendokasi helmet zilipasuka kama mayai. Nikaokota kipande cha helmet wakati tumezunguka eneo la tukio na kujionea nembo maridhawa ya TBS.
MBILI: Nyembe za kunyolea hapo zamani ilikuwa ukinunua wembe inakubidi usome instruction kabisa maana haukawii kukujeruhi lakini nunua nyembe za sasa hivi..hata karatasi hauwezi kukata kwa makali ya nyembe za awali. Mfano mzuri nyembe za gillete sasa hivi hazifai ni butu. Na ninaimani hawa TBS wanahusika katika kudhibiti ubora lakini bado watumiaji wa bidhaa tunapata bidhaa zenye viwango dhaifu kabisa.
ANGALIZO: TBS amkeni tokeni nje ya ofisi fanyeni tafiti za bidhaa mnazohakiki muone kama uhakiki huo una tija au la. Ningekuwa Rais Magufuli ningeformat hilo shirika lote. Naamini TBS INA NGUVU NA MAMLAKA ya kukataa bidhaa zisizokidhi kiwango.