TBL inavohujumiwa Moro Mjini

TBL inavohujumiwa Moro Mjini

Miss ferrar

Senior Member
Joined
Apr 7, 2016
Posts
199
Reaction score
172
Ni takribani wiki mbili mkoa wa morogoro bia za Tanzania breweries ltd zinauzwa kwa kusuasua au kuadimika kabisa mtaani,kwa uchunguzi mdogo nliofanya huu mji una maagent 3 ambao ni munishi focus,gasper masid(chuwa) na Asenga.

Nilichokiona ni wao kubadili biashara kinyemela na kuuza kwa rejareja(retailers) kama mastockist kinyume na leseni zao za kuuza jumla(wholesalers),huku wakihodhi vinywaji vyote na kuwanyima wauzaji wafanyao biashara kama stockists hivo kuihujumu kampuni mf.bia za kilimanjaro au safari ndogo agent huuziwa Tsh.25000@crate kiwandani,yeye hutakiwa kuuza Tshs.25600@crate kwa stockist huku kampuni ikiwalipa million 10 ya usambazaji pamoja na pesa kwa wafanyakazi,hali imekua tofauti baada ya kuzihodhi ambapo huuza Tsh. 27000@crate kwa wateja wote stockist na rejareja,hivo kutengeneza faida ya Tsh.2000@crate mbali na pesa wanayolipwa na TBL kwa usambazaji na wafanyakazi wao.

TBL fanyieni kazi hizi hujuma kabla tatizo halijazidi kukua.
 
TBL sijui biashara imewashinda? hata huku Mbeya bia zinasua sua sasa sijui tatizo ni nini.

Market managers wao nao wanapewa mishahara ya bure tu hamna wanachofanya kazi kuzunguka na magari tu.

Sikuhizi biashara ya bia ni ngumu nilishawahi kuwashauri TBL lakini wako kimya tu ni hivi;

Kwa Mbeya mjini wakala ni mmoja tu ambaye ni NDIO UNITED COMPANIES. huyu amekua akirelax sana na kusababisha baadhi ya wafanyakazi wake kufanya kazi watakavyo na kuuza bia kwa rushwa kwa kila storekist anayehitaji aina flani ya bia yenye soko.

TBL wakubali wakatae storekist ndo wanaofanya biashara kwa wingi na wanaenda maeneo mengi (remote areas) zaidi kushinda agent mkuu hivyo wangewawezesha storekist kuboresha biashara yao mfano wangeweza kuweka terms na conditions kwa local storekist wanaofahamika kuweza kuweka dhamana (bond) ya kitu flani mfano asset ili waweze kupewa mzigo wa kutosha ili wafanye biashara na mitaji yao midogo (legal and timeframe) kwaajili ya marejesho wa mzigo anaouchukua storekist) kwasababu biashara nyingi za magrocery zinafunguliwa jioni na mda mwingine storekist wanakua hawana bia za kutosha hivyo kusababisha kukosekana kwa bia.

Pili storekist wanawasaidia kupunguza gharama mbalimbali (running cost) kama mafuta mnayompa agent na mishahara ya wafanyakazi.

huu ni ushauri tu mkiupenda muuchukue mkiona ni takataka muuache ila time will tell.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niendelee na jibapa. Maji ya mende yamekua adimu

Psalm 133:1 "Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."
 
Ukifika Tabora utachoka. Bia za TBL ziletwapo na distributor, zote zenye soko ni order ya agents(huwa wamelipia tayari). Hakuna za kusambazwa kwenye mabaa. Ukizifuata kwa hao agents uwe na cha juu kuanzia sh 2000 kwa crate. Mwokozi ni SBL, hana gogoro ya usambazaji.
 
TBL kina mgogoro mkubwa sana wa kisheria. Wanahisa wakubwa, yaani Msauzi na yule wa Holland wametofautiana vibaya na kupelekana mahakamani/Fair Competition Tribunal. Hali ni mbaya kinaweza kufungwa. Chanzo kikuu ni mwanahisa mmojawapo kumhujumu mwenzie. Tetesi ni kuuzwa kwa hisa nyingi kwenye kiwanda tawi cha TBL cha Konyagi bila kushirikisha mwenzie.
 
Kama ni haramu ni kwako muache ambaye sio haramu akitumie!! Niliwahi kusikia hata pesa inayotoka humo nayo ni haramu?! Sasa serikali integemea pesa kutoka humo kununulia madawa inakuwaje??! Nayo ni haramu kweli mambo ya imani ni magumu.
Watu wengine ni wazinzi mkuu
 
Back
Top Bottom