TBC1 wameshusha tena signal za madishi?

TBC1 wameshusha tena signal za madishi?

vamda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
919
Reaction score
598
Salam wana JF. Huwa natumia dishi la futi 6 kupata matangazo ya televisheni. Siku za nyuma nilikuwa napata matangazo mbalimbali ikiwemo TBC1 lakini sasa ni zaidi ya mwezi sipati matangazo yao. Kila nikiwasha TBC1 inaandika 'WEAK SIGNAL' Je ni kweli TBC1 wamepunguza masafa ya matangazo (signal)? Kama jibu ni ndio basi TBC1 haina faida kwa wananchi tulio wengi tunaoishi vijijini ambao hatuna huduma ya ving'amuzi. Madishi ndiyo yanayotuokoa. TBC1 watufikirie sisi wananchi tunaoishi vijijini maana hiyo ni telelvisheni ya Taifa, tuna haki ya kupata matangazo yao. Au kwa sababu wanataka kurusha kombe la dunia, wameamua kutubania sisi wanyonge tunaotumia madishi ili wafanye biashara yao ya ving'amuzi!
 
Yawezekana kweli wamefanya hivyo ili waonekane pekee kupitia VING'AMUZI vyao na StarMedia ambavyo wanaviuza. Mkurugenzi wao Clement Mshana alisema WAPO KIBIASHARA ZAIDI ndio maana wamenunua haki za kurusha WORLD CUP kwa bei ghali (ingawa aligoma kuitaja bei). Sioni ajabu wakawazuia wenye madish maana wanajua MTAONA BURE.
Hio ndio tbc...
 
Salam wana JF. Huwa natumia dishi la futi 6 kupata matangazo ya televisheni. Siku za nyuma nilikuwa napata matangazo mbalimbali ikiwemo TBC1 lakini sasa ni zaidi ya mwezi sipati matangazo yao. Kila nikiwasha TBC1 inaandika 'WEAK SIGNAL' Je ni kweli TBC1 wamepunguza masafa ya matangazo (signal)? Kama jibu ni ndio basi TBC1 haina faida kwa wananchi tulio wengi tunaoishi vijijini ambao hatuna huduma ya ving'amuzi. Madishi ndiyo yanayotuokoa. TBC1 watufikirie sisi wananchi tunaoishi vijijini maana hiyo ni telelvisheni ya Taifa, tuna haki ya kupata matangazo yao. Au kwa sababu wanataka kurusha kombe la dunia, wameamua kutubania sisi wanyonge tunaotumia madishi ili wafanye biashara yao ya ving'amuzi!

Tbc1 siyo television ya taifa, ni kundi la wahuni tu, ndio maana hawahitaji kuonekana nchi nzima. Hata redio yao ya Tbc taifa nayo ni mtihani tu!
 
Ni wapi huko, maana dar ipo poa na ni week ya pili tbc2 ipo hewani fri of chj, ila sijaelewa kama ndo promo ya wc (kombe la dunia) au la!!
 
Kijiji cha Ulowa Kahama
 
Mimi sishangai,inchi{viongoz} imeshindwa kusimamia kila jambo:umeme,wanyama,madin,afya & Elimu++TBC -habari.waizime tu!!
 
Hata kama wanafanya biashara.., wasitumie mbinu za ki-mbwa kuuza ving'amuzi.., si wanakula kodi zetu sasa kwanini watunyanyase..??!
 
Back
Top Bottom