Tbc1 na mambo yao ya kale

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,427
Wana Jf 10/09/2011 Jamhuri yetu ya Tanzania ili pata msiba mkubwa,lakini wakati msiba huo unatokea hata baada ya masaa 10 kupita bado TBC1 kituo cha Habari cha walipa kodi cha Taifa hakikuweza kuwaonyesha wadau wake nini kimetokea katika Taifa HILI

Baada ya ajari tu kutokea ni mitandayo ya kijamii ndio iliyokuwa ikitupa habari za ajari hiyo kama vile JF,FACEBOOK na TWEETER na kituo cha ALJAZEELA nacho kiliweza kutupa habari nini kimetokea ktk Taifa letu

Cha ajabu TBC1 wao walikuwa wakionyesha miziki tu na kuwaacha wadau wake wasio na uwezo wa kupitia mitandao kubaki midomo wazi

Sasa inakuwaje TBC1 bado inaleta mambo ya kale katika wakati huu wa utandawazi? wanamficha nani habari ambazo tayari watu walisha zipata kupitia mitandao ya kijamii? Je TBC1 hawana wawakilishi zanzibar kule lilikotokea tukio kama ni kupata uhakika basi wangewasiliana na wawakilishi wao lakini wao mhhhhhhh ni TAARABU na Miziki ya Kikongo


tutafika kweli?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom