TBC1 haipendwi na Watanzania

Jana nililazimika kuangalia channels za Kenya kupata habari saa moja na saa tatu usiku. TBC tupa kule!!
 
Iondoe kasoro itapendwa tu,japo Upendo haulazimishwi.
 
Tbc imekosa mafundi mitambo wenye ubunifu,na vifaa duni (camera).Muonekano wake ni wa hali ya chini sana,haina mvuto kabisa,pia ina taarifa za upande moja (ccm).
 
Tutaipendaje TBC wakati yenyewe haitupendi. TBC hawana heshima hata kidogo wanatusukumia habari hata kama hazikubaliki. Wakae waangalie wenyewe bango, cherereko na kumwagiana sifa ambazo hazipo
 
Enzi Za Tido Muhando TBC ilikuwa Nzuri Sana Ilikuwa na Vipindi Vizuri Sana!Watu Tunaichukia Maana Ni Tv Ya Kusifia Sifia Tu Vitu Vya Hovyo Wapinzani tunaiitaga TBCCM
 
Huipendi wewe
 
Hakuna MTU mwenye akili timamu anaweza kutazama huu uchafu hata wafanyakazi WA TBC huangalia taarifa za za Azam2 au Itv
 
Haina tofauti Na KBC ya moi ilikuwa ni kumsifia mtukufu arap moi Kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…