TBC ovyoo!

chi-boy

Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
98
Reaction score
15
haiwezekani habari ya Vurugu morogoro wasiitangaze hata kuigusia kidogo.

Au ndo kufwata maneno ya Rais kwa vyombo vya habari kuacha kuichafua serikali kwa kukuza habari. TBC naifuta rasmii, haina tofauti na gazeti la Udaku..

Achana na TBC, ni mradi wa kupumbaza wananchi
 

wakati wabunge wako wanaipangia bajeti bungeni..?
 
Horible channel never seen
 
kama mashirika mengine ya serikali yanavyokufa na hili linafwata..
Serikali hii haijifunzi..
 

Ulikuwa unaangalia TBC, kwani leo orijino komedi wameigiza nini?
 
Tbc ccm swala la ulimboka kutekwa hawakusumbuka kabisa,mauaji arusha,songea na leo imetokea morogoro, jaman tbc tambueni nyinyi mnatamba kwa kodi zetu, jaribuni kufungua akili zenu, mkicheza nyote 2015 mtazipoteza kazi zenug,take care
 

Tusiwalaumu sana TBC1 kwa vile maandamano yenyewe yalikuwa batili kwa mujibu wa jeshi la polisi. Sijui sheria inasemaje, mwandishi wa habari akidhuriwa katika mikusanyiko ambayo siyo halali na hasa ukizingatia vyama vya siasa vinakuwa na chuki binafsi na baadhi vya vyombo vinavyomilikiwa na Serikali na hivyo vinakuwa vinaogopa kuafanyia vurugu na mfano mzuri ni mkutano wa CDM pale jangwani mwaka 2010 ambapo Waandishi wa habari wa TBC1 walifanyiwa vurugu.

Halafu jambo lingine Vyombo hivi vya habari vinakosa morari ya kuandika habari kutokana na ukweli kwamba vimekuwa vikitupiwa shutuma kuwa vinaipendelea serikali, sasa vinaona hakuna haja kabisa ya kuandika habari zao, jmbo ambalo binafsi naona viko sahihi kabisa.

Huwezi kuvishtumu halafu ukataka viandike habari zako.
 
kuna wakati nilikuwa nalazimika kuitizama kwa kuwa king'amuzi uchwara hakidaki local chanels kama STAR TIMES na ITV, lakin bora kusimuliwa habari kesho yake na waliongalia channel nyngn...TBC uozo tu
 
Tbc ccm swala la ulimboka kutekwa hawakusumbuka kabisa,mauaji arusha,songea na leo imetokea morogoro,jaman tbc tambueni nyinyi mnatamba kwa kodi zetu,jaribuni kufungua akili zenu,mkicheza nyote 2015 mtazipoteza kazi zenug,take care
Wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hata ukija wewe mkuu na kuwa mwanasheria mkuu wa serikali hiyo mpya huna mamlaka ya kuwafuta kazi. Wanaogpoa kuambiwa wanapendelea Serikali so wanaona bora wapige kimya.

Mimi nafikiri nia fundisho kwa asasi ambazo zinatangulisha hisia z kisiasa na kuanza kuvishutumu vyombo vya habari bila ya kuwa na ushahidi wa shutuma zao.

TBC1 kamwe hawawezi kuwa na morari ya kuandika habri zaCDM kwa vile hata wakijitahidi vipi kuandika kwa ufasaha wataambiwa wanapendelea serikali.
 

Tuambie nani siyo hovyoo badala ya majungu
 
Dhaifu, na kila kitu dhaifu, ... ni dhaifu kwenda mbele !!!!
 

wewe unaonyesha kabisa unakitu na serikali au Tbc yenyewe au unafanya kazi Tbc?ACHA UMAGAMBA SISI TUTAWANG'OA 2015 THEN WAKASHTAKI POPOTE.
 
Sitaki kuamini kuwa kuna watu bado mnaiangalia hiyo channel!!!!!
 
Kwao kipaumbele kwa sasa ni sensa tu! Oneni aibu wafanyakazi wa tbc1. Katika ulimwengu huu wa utandawazi inashangaza kufichaficha habari kwa sababu tu si njema kwa watawala.

Hata watoto wadogo hapa nyumbani hawaitaki, shortly ni channel ambayo inapoteza mvuto kila kukicha, mnachukiza tbc!!!!
 
ITV waliionesha hadi kama live vile.
 
Kuanzia jana mii siangalii taarifa za habari zote za TV za Bongo kwani BBC Swahili kupitia STAR TV inatosha kabisa kwani habari ni za ukweli na uhakika
 

Naanza kuwa na wasisi na wanajf nahisi wanatumiwa na wanasiasa
 
Tusipost vitu kwa interest zetu binafsi, TBC wamefanya mangapi mazuri, wameelimisha jamii mara ngapi, Tutafakari na tuchukue hatua.

TBC ni chombo cha habari kama vyombo vingine na hakina upendeleo wowote. Let us talk the truth & abandon political propaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…