Tbc ni wezi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tbc ni wezi!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mtzd, Oct 31, 2012.

 1. mtzd

  mtzd Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wadau wa Jf muhali gani,habari za humu jamvini,Kuna suala ambalo kwa kweli TBC wamelifanya nadhani si la kiungwana ,Kuna mashindano ya mpira wa Kikapu yanayoendelea mkoani Tanga,yalianza tangu tarehe 29/oct na yatamalizika Nov 5.Nasema ni wezi kwa sababu walisema wangeonyesha michezo hii live(online) kupitia mtandao(website),kweli tangu walipoanza nimejaribu kuingia kwenye website yao na kuna linki yenye address hii http://65.182.107.34:8080/tv/index2.html na unapoingia hapa unapata sehemu ambayo inabidi ulipie then unapata PIN,kama ndio njia ya kujitafutia hela kwa kuwaibia wananchi nadhani sio sahiibali ni wizi ,nikiwa kama mdau wa mchezo huu nimejaribu kuingia kwenye hii linki ambayo unachajiwa sh 500 kwa kutuma pesa kwenye mitandao kama unayoiona kwenye picha na wanakwambia utapata PIN ambayo itakuwezesha kuingia na kuweza kuangalia michezo hii live,HUU NI WIZI mtupu kwani hiyo linki haifanyi kazi,unapoingiza PIN ambayo unaipata baada ya kulipa sh 500 inakwambia INVALID PIN,tana chini kabisa wameeandika vigezo na masharti kuzingatiwa.ama kweli nyie TBC mnakera , hii ni njia sahihi kweli ya kujipatia fedha,Kwenye maandalizi ya mwaka huu kwenye ligi ya Kikapu kumekua na matatizo mengi mojawapo ikiwa ni ukata wa fedha za kuweza kuongoza ligi hii,Na taarifa nilizopata kutoka kwenye vyombo husika chama cha mkoa wa dar es salaam cha Basketball (BD) ni kwamba kumekua na shida tangu ligi ilipoanza.TBC mkiwa kama chombo cha Taifa nadhani ilikua ni jukumu lenu, tena kuonyesha michezo hii live kwenye Tv na wala sio kwenye mitandao , nadhani ilikua njia sahihi ili muweza pia kupata na wafadhili,matokeo yake ni kuweka online ambapo pia hakuna chochote zaidi ya kujikusanyia hizo 500 .Kwa hali hii sidhani kama mtaweza kuendeleza michezo kwa njia hii,Angalieni wenzenu hata tusiende mbali ,Kenya wanatushinda ,sembuse Nigeria na Angola wenye Tv ambazo zinaweza kuonyesha michezo yao live na sio kwenye mchezo mmoja tu bali karibu michezo yote.Serikali yetu nayo sijui iko wapi,kila siku ni maelezo ambayo mimi nayaita ni kelele bila kutekeleza lolote.Wadau wanaohusika kwenye masuala ya michezo mko wapi,Kweli kwa hali hii TUTAFIKA,ni bahati tumeweza kumpata Hashim Thabeet NBA je kuna akina Thabeet wengine au tutaishia kuwaona wenzetu wakiwa juu zaidi yetu.
   

  Attached Files:

Loading...