TBC na Report za campaign za Uchaguzi Mdogo

Nadu

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
263
212
Wana JF kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikifuatilia taarifa za habari za TBC. Katika kuripoti chaguzi ndogo wamekuwa wakionyesha mikutano ya campaign za CCM tu huku wakitoa maelezo bila picha kuhusu vyama vingine. Kama wakitoa picha ni matukio madogo ambayo sio mktano.

Najiuliza hivi vyama vingine hawafanyi mikutano ya hadhara? Mbona hairipotiwi?

Note: Nalazimika kuangalia TBC maana azamu kanitupa.
 
Wasichokijua ni kwamba kati ya mambo yanayochangia TBC kutopendwa na kuporomoka ni hayo mambo ya kibaguzi na upendeleo kwenye kutoa taarifa.
 
Mkuu aliyekwambia TBC ni televisheni ya Taifa ni nani?,TBC ni televisheni ya ccm na hilo lilishasemwa na nape wakati fulani akiwa waziri hebu jaribu kukumbuka
 
Nipo ktk kampeni za kuwashawishi wakazi wa jimbo la Ukonga wapake rangi za CDM ktk nyumba zao.

Kwa kweli zimepauka na kuchakaa

Chonde TBC nipigeni picha basi nipo Majohe kwa nabii Peter Amos naendelea na kampeni huku.

Pipoz pawaaa!!!
 
Mkuu aliyekwambia TBC ni televisheni ya Taifa ni nani?,TBC ni televisheni ya ccm na hilo lilishasemwa na nape wakati fulani akiwa waziri hebu jaribu kukumbuka
TBC ni TV ya Taifa kwa sheria. kinachofanyika ni matumizi mabaya ya kupendelea chama kimoja ukiachilia mbali kuchuja habari za wananchi na kutangaza zaidi habari za wakubwa. Tunapaswa kupaza sauti zetu ili watupe product tunayotaka sisi wananchi
 
Namshangaa sana Dr. Rioba kuweka pembeni maadili ya uandisha kwa kuripoti kwa upendeleo, tabia hiyo waliianza tangu uchaguzi mdogo wa Buyungu. Wakijitahidi sana walikuwa wanawaripoti ACT, Chadema waliwekwa kando.

Vv
 
Kampen za upinzan hazina hoja ni kulalamika tu wala hawana ilan sasa maendeleo wataleta VP ccm viva viva
 
Kampen za upinzan hazina hoja ni kulalamika tu wala hawana ilan sasa maendeleo wataleta VP ccm viva viva
Hayo unayoyasema ndio wananchi wanatakiwa wayajue halafu waamue siku ya uchaguzi. Kwa nini wengine wawamlie wapiga kura?
 
Hayo unayoyasema ndio wananchi wanatakiwa wayajue halafu waamue siku ya uchaguzi. Kwa nini wengine wawamlie wapiga kura?
Hawawez kutangaza hoja mtoto mdogo kama mgombea wa chadema huko ukongo hana haiba ya ubunge ni chakula cha mbowe tu waache watangaze Sera za serikali yao
 
Back
Top Bottom