TBC: Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima Azungumzia Umuhimu wa Elimu ya Mpiga Kura

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,649
119,257
Wanabo Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amezungumza live kwenye kipindi cha Jambo Tanzania, kinachorushwa live na Television ya Taifa, TBC.

Bw.Kailima amezungumzia tathmini iliyofanyika kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi wa 2015, ili kubaini sababu za wanaojotokeza kupiga kura ni wachache huku waliojiandikisha ni wengi.

Kailima ameeleza baadhi ya sababu hizo, kubwa ikiwa ni ukosefu wa elimu ya mpiga kura.

Maadam NEC imeisha baini hili la ukosefu wa elimu ya mpiga, ni matumaini yetu uchaguzi wa 2020, things will never be the same again.

Angalizo kwa NEC, baada ya kubaini hilo, wanaweza kuwa wamejikalia na ku relax kwa mategemeo 2020 bado ni mbali sana!. Kwa maoni yangu nikiwa ni mzoefu na utayarishaji wa vipindi elimishi vya Radio na Television, kama next election ni two years to come, time ya kuanza mchakato is now,or never, wakizidi kuchelewa, watakuja kujikuta it's too little too late! .

Paskali
Rejea
Pascal Mayalla aipigia debe NEC Nanenane

TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!
 
utuletee mrejesho wengine hatuna tv visimbusi bei juu!

lkn hiyo elimu ya mpiga kura iendane na uzalendo kwa maana ya uwazi wa kura n.k sio elimu halafu kula zinakuwa zinaibiwa yafaa nini..?
inapoteza maana nzima ya elimu ya mpiga kura.
 
Hivi bado kuna watu wanatazama TBC1? Hata kama Yesu atashuka azunguzie kule siwezi kuangalia!
 
Nikimsikia huyu jamaa na yule Mzee wa upara nahisi kuchanganyikiwa maana naona wanaendelea kutudanganya.
 
Suluhu ni Tume huru tuu.
Mkuu Suluhu, cha muhimu sio tume huru bali ni uchaguzi huru na wa hakI.

Zanzibar inaelezwa ndiko kwenye tume huru kwa sababu wapinzani wameteua wajumbe, angalia kilichotokea! .

As long as uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, then the end justify the means.

Paskali
 
Hakuna cha Elimu hapa shida ni Tume yote ni ya CCM tunataka Tume Huru ya Uchaguzi wewe Kailima usitufanye sisi sote ni bongo lala.
Bila Tume Huru hakuna jipya unatetea Tumbo lako na CCM kiama chaja muda si mrefu ni Tume Huru tu ya uchaguzi tuone mtachakachua wapi maana hamkubaliki zaidi ya kudanganya wananchi na kiini macho.
 
Hakuna cha Elimu hapa shida ni Tume yote ni ya CCM tunataka Tume Huru ya Uchaguzi wewe Kailima usitufanye sisi sote ni bongo lala.
Bila Tume Huru hakuna jipya unatetea Tumbo lako na CCM kiama chaja muda si mrefu ni Tume Huru tu ya uchaguzi tuone mtachakachua wapi maana hamkubaliki zaidi ya kudanganya wananchi na kiini macho.
Mkuu Bridalmask, unaonekana una hasira sana, sasa usikute ni watu kama wewe ndio mlioirudisha CCM madarakani kwa hasira zenu za mkizi! ,hivyo hamkupiga kura kwa kususa.

Waliojiandikisha ni watu milioni 22 halafu waliojotokeza ni watu milioni 8. Watu milioni 12 nzima mlisusa, kati ya waliopiga kura na waliosusa, nani wamesababisha CCM ishinde? !. Usiisingizie Tume! .

Paskali
 
Pole kwa kuhisi kuchanganyikiwa, hutachanganyikiwa tena kwa sababu Mzee ameishapumzika.
Paskali

Mkuu Paskali naomba nisaidie, ni kwanini hizi tume wanachaguliwa viongozi wastaafu? Halafu wanaposema vijana tujiajiri wanamaanisha hizo nafasi ni za wazee wastaafu? Hebu ukikutana na hizo mamlaka wahoji kwani ww una nafasi ya kuongea nao.
 
Mkuu Paskali naomba nisaidie, ni kwanini hizi tume wanachaguliwa viongozi wastaafu? Halafu wanaposema vijana tujiajiri wanamaanisha hizo nafasi ni za wazee wastaafu? Hebu ukikutana na hizo mamlaka wahoji kwani ww una nafasi ya kuongea nao.
Mkuu Tindo, kwanza sifa ya mwenyekiti wa Tume ni lazima awe Jaji wa Mahakama Kuu. Wanateuliwa wastaafu kwa hoja watakuwa ni watu wenye busara.
P.
 
Huyu anataka kututoa kwenye mada ya msingi ya kudai katiba mpya ya warioba na tume huru ya uchaguzi
 
Huyu anataka kututoa kwenye mada ya msingi ya kudai katiba mpya ya warioba na tume huru ya uchaguzi
La katiba liliisha kwisha kilichobaki ni kura ya maoni. Katiba mpya ikipita pia itaambatana na tume huru ya uchaguzi.

Kitu chá muhimu ni kwa sisi Watanzania kwa kauli moja, tuipigie kura ya ndio ipite.

Paskali
Mchakato Huu wa Katiba, ni Umasikini Wetu!, Tujikubali!, Tuukubali, Tuupigie Kura ya Ndio!.

Je Wajua Kuwa Kura ya "Hapana" Kwa Katiba Mpya! Ni Kura ya "Ndiyo!" Kwa Katiba Hii Iliyopo?
 
Back
Top Bottom