Tazara Flyover...!

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
57,754
Reaction score
129,487
Jana kwa mara ya kwanza nimepita Tazara junction wakati flyover imekamilika. Kusema ukweli im impressed. Flyover ile ukiiona kwa macho ni tofauti na picha mitandaoni, iko vizuri sana.

Kingine nimeona wameacha nafasi kubwa katikati ni wazi wamezingatia BRT lanes zitakazokuja baadae, ningeshauri pale junction ya Nyerere/Kawawa napo waweke flyover kama hii hali itakuwa nzuri zaidi.

Imenikumbusha Chiswick Roundabout Flyover ya London ambayo iko kwenye barabara inaitwa A4 East bound. Muundo wake unafafana na wenye lugha yao wanaiita FLYOVER.
 
Nilitegemea angalau kwa kuanzia kitu kama hiki pale Tazara lakini .. hapa Ni Bangkok ndiyo walikuwa wanaanza baada ya magari kuwa mengi.
Swali, kweli daraja hili litapunguza msongamano Tazara?
 
Attachments

  • upload_2018-7-22_7-12-54.jpeg
    13.3 KB · Views: 142
Nilitegemea angalau kwa kuanzia kitu kama hiki pale Tazara lakini .. hapa Ni Bangkok ndiyo walikuwa wanaanza baada ya magari kuwa mengi.
Swali, kweli daraja hili litapunguza msongamano Tazara?
Wingi wa magari yetu ni sawa na Bangkok? Uzuri wa flyover zinajengeka kirahisi bila kuathiri barabara iliopo.
 
Wingi wa magari yetu ni sawa na Bangkok? Uzuri wa flyover zinajengeka kirahisi bila kuathiri barabara iliopo.
Yes, kwa ufinyu wa barabara zetu you can equate it to Bangkok. Hivi magari yanayotoka Buguruni/Mbagala msongamano utapunguaje maana hiyo flyover ni along Nyrere road! Nieleweshe please
 
Nilitegemea angalau kwa kuanzia kitu kama hiki pale Tazara lakini .. hapa Ni Bangkok ndiyo walikuwa wanaanza baada ya magari kuwa mengi.
Swali, kweli daraja hili litapunguza msongamano Tazara?
Hatuna uwezo huo kwa sasa. Na katikati ya jiji space ni ndogo. Itabidi wabomoe nyumba na magorofa kadhaa ili iwekwe hii barabara
 
Yes, kwa ufinyu wa barabara zetu you can equate it to Bangkok. Hivi magari yanayotoka Buguruni/Mbagala msongamano utapunguaje maana hiyo flyover ni along Nyrere road! Nieleweshe please
Yatapungua kwasababu wamekata muda wa kusubiri yatokayo mjini kwenda airport. Yaani sasa hivi hawatasubiri sana kwasababu ya town-jnia yanapita juu.
Hivi unajua traffic police anaweza kuzuia nusu saa ili upande mmoja upite? Hio nusu saa yanakuwa yamepita magari mengi sana
 
Hii fly over inaweza kuwa msaada kimawazo,ila katika uhalisia tatizo la foleni kitabaki palepale....mana magari yatakuwa yanaumana sana upande wa kushukia,mfano kuelekea uwanja wa ndege sehem ya kushukia pale magari yatakuwa yanakutana kwa wingi halaf mita chache mbele kuna msongamano,unatarajia nini?.....
 
Haya pia uyasemayo ni mawazo yako tu. Sababu kuu ya foleni ni junction hio ya Tazara kwasababu zinakutana barabara kuu mbili.
Pale Veta/Vingunguti polisi huwa wana-prioritize Nyerere road traffic hivyo wanauwezo wa kuhakikisha hicho unachowaza hakiwezi kutokea.
 
Junction ya Jet Lumo,unasemaje? japokuwa iko.mbali na sio kubwa coz inaungana na feeder road ila kiasi chake inaweza kueleta shida...
 
Junction ya Jet Lumo,unasemaje? japokuwa iko.mbali na sio kubwa coz inaungana na feeder road ila kiasi chake inaweza kueleta shida...
Jet pia ni junction ndogo, polisi anatoa kipaumbele kwa Nyerere road traffic. Hawezi kufanya hivi Tazara kwasababu ni junction ya barabara kuu mbili.

Junction za barabara kuu mbili zote zinahitaji flyover sema umaskini wetu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…