Tazama teknolojia mpya ya Usafirishaji

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
Your browser is not able to display this video.


Video zimesambaa zikionesha usafirishaji wa haraka wa Pizza, ambapo mtu aliyevaa Jet Suit, ameonekana akipokea oda kutoka dukani, na kuipeleka kwa wateja huku akipaa ikiwa ni namna ya kuokoa muda na kuhakikisha ubora wa chakula

Ni baada ya Kampuni ya kutengeza Fast Foods ya Domino's ya Marekani kuungana na Gravity Industries kufanya majaribio ya kwanza duniani ya kusafirisha pizza kwa kutumia vifaa vya kuvaa vinavyoendeshwa na injini za roketi (jet suit) katika tamasha la #Glastonbury nchini Uingereza

Vifaa hivyo ambavyo gharama yake inakadiriwa kuwa zaidi ya Tsh. Milioni 900 vinahakikisha usalama wa rubani na kuhakikisha chakula kinakuwa safi na cha moto wakati wote wa usafirishaji


Chanzo: Mtandao
 
Ukisema tazama, weka na ka kiambata basi😎
 
Aisee nimeipenda hii
Well done👏👏👏
 
Kupaa wamewaiga wachawi.Dark world ipo more advanced kuliko really World vyote uvionavyo dunia kupitia technology wamekopi toka dark World
 
Asijaribu kupita karibu ya nyumba yangu. Hizo manati atakazokula atajuta kuruka ruka juu ya paa za watu
 
Kupaa wamewaiga wachawi.Dark world ipo more advanced kuliko really World vyote uvionavyo dunia kupitia technology wamekopi toka dark World
Wachawi wanaopaa kwenye ungo watakuwa wanajua how to manipilate gravity, yaani antigravity ila ndio hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…