Tayari nimepanga kutembelea vyombo zaidi vya habari

Status
Not open for further replies.

Tangu nape aende UDOM huku JF hakukaliki tena. Hoja zako hazina mashiko bwana mdogo, watu wote hawa wanaochangia humu usidhani it's just in vein, usidhani watu wanafanya mchezo wa kuigiza humu kama kule facebook. Wana uchungu na nchi yao na wana haki ya kujua hatima ya maisha yao pamoja na taifa lao.

Wengi hamjamwelewa nape kinauye, baada ya kutembelea TBC, pamoja na Habari leo , sasa anataka atembelee ofisi za JF, ukiwa kama nani?

Ushauri wangu kwako nape kinauye ni kwamba kazi za chama endesha huko huko, kwanza nimeshangaa sana nini nilichokupeleka huko TBC na HAbari Leo ilhali ni vyombo na mali ya Wananchi, na wewe wakati huo unawakilisha Chama cha Magamba. Usitake kutisha watu kwa gwanda lako la kijani.
 
Nape nakupngeza kwa usugu uliodevelop pamoja na shuruba tele, nina swali moja tu

Je, unadhani ziara zako na mikutano na vyombo vya habari vimeadd any valkue to CCM na wewe binafsi??

Thanks
 
Nnauye; Wakati upo UVCCM, ukiwachachafya viongozi wa Chama kwa ufisadi na mikataba isiyo na manufaa kwa chama nilikuona kweli wewe ni mzalendo. Ulipoteuliwa kuwa DC kasi yako ikapungua, ukanyamaza kwa kuwa tayari marupurupu kibao yalikuwa mlangoni kwako.

Ila taratibu ukaanza kujipigia kampeni kisiasa, ukautaka ubunge wa Ubungo na nikawa nakufuatilia sana Posts zako za kwenye Facebook, zilionyesha kutokubaliana kwako na baadhi ya mambo ndani ya chama.
Majuzi umepewa tena ulaji ndani ya CCM, from day 1 ulipopata cheo hiki umekuwa kama kinyonga, umebadilika, lakini afadhali kinyonga ambaye anakwenda taratibu.

Wewe kasi yako inatutisha, unachokera watanganyika ni namna ulivyokosa uzalendo. Kuna mambo ya msingi yanazungumzwa hapa JF ambayo hata Rais na viongozi wengine wa CCM hawajathubutu kuyasema. Badala ya kuiona JF kama ni Forum ya kueneza propaganda dhidi yenu ulipaswa kuishukuru kwa kuweka bayana mambo mnayoshindwa kuthubutu kuyazungumza.

Naomba unisaidi kujibu/kueleza hoja chache tu ambazo zimejadiliwa sana hapa JF:

1. HOJA YA POSHO: Ulikiri kwamba hoja ya CDM kuhusu posho ni ya msingi, serikali ya CCM imeitupilia mbali kwa kutoa hoja za kitoto zilizotolewa na fisadi Pinda? Unasemaje katika hili?

2. KUKATIKA KWA UMEME: Suala la umeme limekuwa kero sana kwa wtanzania, kwa sasa zaidi ya 75% ya nchi iko gizani! Hatujasikia kauli ya kiongozi wa serikali kuhusu hili. Wana JF tunapozungumzia hili mnatuita tumetumwa na CDM, au tunaeneza Propaganda dhidi ya Chama chenu! Sasa manadhani watanzania ni wapuuzi? Mnadhani hatulioni hili?

3. KUJIVUA GAMBA: Hadi leo watanzania hatujaelewa vema CCM ilikuwa inamaanisha nini iliposema INAJIVUA GAMBA! Tuliambiwa Edward Lowassa na wenzake walipewa siku 60 (kama sikosei) wajieleze! NADHANI HADI LEO NI ZAIDI YA SIKU 60….Hebu tupe kinachoendelea
 

Mkuu endelea kumwaga cheche. Hapa JF kuna upinzani wa wazi wazi kwa CCM na sera zake , kwa kujua au kuto jua.
Wengi wa wapinzani wako katika fungu la wasio jua na hao utaona wanapindisha maana ya sera za CCM kiwazi wazi, hawa ni wa kuwapuuza.

Kuna wale ambao mimi nawaita wasukuma mikokoteni kwa utani, au macoconut, hawa ni blind followers wa CDM ambao hawana mchango wowote kwa CDM yenyewe wala nchi, utawaona kwa matusi yao.

Vile vile kuna wanaotoa challenge za kikweli kweli kwa chama tawala au kwa kuasa pale inapokosea kimfumo au kiutendaji-pokea lawama hizo na kuzipeleka kunako husika Mkuu.

Katika kazi kama yao usitegemee mpinzani akupe ingalao ka senks kwa kumfunga bao. Lakini kuna wapenzi wa kweli wa CCM humu humu na wanatetea sera na maamuzi yote ingawaje vile vile kunakuwa na ka-ucoconut ndani yake.

Hata hivyo Mkuu usikate tamaa, kwa uzoefu wangu mdogo hapa JF, ukiona uongo, matusi na vingine vinaongezeka ujue umewanminya panapostahili!!!!!

In actual fact kwenye Idara yako you have made the difference, keep it up. Kwa hakika Idara yako ya Uenezi lioanza kujibu tuhuma za CDM na vyama vingine ndo naona upotoshaji ulipokolea.

Again keep it up.

Au kwa msemo wa miaka yetu KIDUMU!
 
UDOM hapo inaingiaje wakati humu jamvini hali ilibadilika sana mara baada ya CCM kuja na sera ya kujivua gamba mnamo mwezi februari, Nape mwenyewe alinda Udom mwezi mei
 
Nape,

Ningependa kujua ni nini hasa lengo la hizo ziara katika vyombo vya habari?

Lengo ni rushwa tu..hujui kaka..... Corruption is not necessarily in monetary terms.... Kuzungukia vyombo vya habari ni mpango wa kuvutia ili vyombo viwe na upendeleo kwa chama fulani...Au mnasemaje wenzangu.
 
 
Nilikuwa napenda msimamo wako hata uwajibikaji wako, nilikuwa nakufatilia hata pale ulipopelekwa kuwa mkuu wa Wilaya huko kusin,i still nilikuwa napenda jua watendaje kazi. Nilwai hata kufuatilia interview yako na clouds (PB). Ila ninahofu sasa wapoteza mwelekeo. Anyway, sijakata tamaa kabisa kwani nasubiri mwisho wa kauli hii ya uvuaji wa gamba, na sidhani ni mie tu. I think tupo wengi waliokuwa au wanaoku-admire. Usiwaangushe, please fanyeni kazi kwa maslai ya TAIFA, Msiangalie klupambana na Chadema, no pambaneni na umasikini unaowakabiri waTZ!

Kazi njema!
 
ccm tupeni umeme acha porojo na majungu , mnaudhi sana mnapojaribu kutetea ujinga miaka hamsini umeme hakuna watu wanalala njaa unaleta lawama hapa jf
 
Kamalizeni kwanza kazi yenu ya kuvuana magamba,msifanye kazi nusu nusu kama magamba yamekuwa magumu,waelezeni watu wajue kwamba nyie hamna lolote mnaloweza zaidi,ya siasa za uongo na unafiki watu siku hizi hawadanganyiki, Salaaam Zao.
 
Nape nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya, ukweli umeleta changamoto na approach mpya ktk ccm,
mi si shabiki wa vyama wala viongozi ila napenda changamoto na hoja zenye mshiko na ukweli.

Hapa JF juzi niliweka thread kukupongeza kama wanavopengezwa wa vyama vingine, lakini mods walidelete haraka haraka.

Anyway kaza buti usichoke, jenga chama maana mi naamini (japo si mwana ccm) TZ tunaitaji kiongozi makini mmoja tu wa kulikomboa taifa
na wala si chama. sijuhi atatokea chama gani, tusubiri.
All the best!
 
nape,

hongera kaka hawa chadema ni vuvuzela tuachie sisi tule nao sahani moja. walibadili jf yao ila sasa tunawakabili.

endelea kumwambia daktari wa wakatoliki akalipe kodi.

mbowe vita ya posho aanze na mwenyekiti wake mwenye posho milioni saba na nusu.

taasisi ya mtei na familia haitubabaishi.

endelea kutuletea mambo mapya. chadema umewashika pabaya ndio maana wanakuandama. endelea kuwaminya sawa sawa.
 
ningekushauri uende uhuru na mzalendo ukawatembelee, siku zote mfa maji haishi kutapatapa.
 
Kazi ni kwako,nyie mnapambana na Cdm,CDM wanachanja mbuga kwa wananchi,endeleeni hivyo hivyo.ila kumbukeni CKU HAZIGANDI!
 
Nape watu Tayari wanakuona wewe ni Yusuph Makamba wa Kizazi Kipya, wewe ni Tabwe Hiza mwingine, Hata huko kwa vyombo vya Habari unaonekana ni mbamgaizaji wa siasa za uvundo, unaonekana Malaika wa Nuru kumbe Malaika wa shetani, unatafuta fursa kwa jaso la umbeya , Majungu Na fitna, Nakuambia kwa moyo mweupe kuwa Mwisho wako hauko Mbali
 
Nape, Magamba wamesha pewa barua?
Alafu mbona umetoa thread nakusepa wakati wana JF wamekuuliza maswali kibao ambayo unatakiwa kujibu.
Angalia cha kuongea usijeukajionesha kuwa uwezo wako wa kufikiri ni Finyo.
 
Labda hapa hakuja kujibu Hoja, bali kuwataarifu kwamba "Amepanga Kutembelea Vyombo zaidi vya Habari"
 
Ziara ya kutembelea vyombo vya habari kwa misingi gani haswa itakayotufanya sisi watanzania tunufaike kimaendeleo.
Kwa sababu kwenda kupandikiza mfumo wa chama chako katika vyombo vya habari ni kinyume na maadili ya uongozi,
Siasa ni muongozo wa serikali, Muhimu ni kupandikiza maendeleo kwani vyombo vya habari ni mojawapo ya elimu isiyo
na mpaka kwa jamii katika maisha ya kila siku. Siasa inajitangaza yenyewe bila kufuatilia vyombo vya habari.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…