Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
Habari za uhakika ambazo zimetoka sio UKAWA bali ndani ya CCM wakati wakipanga mikakati yao ya namna watakavyokampeni ,wamefikia hatua ya kusema ni lazima wafanye kampeni usiku na mchana, kwani habari au ripoti walizo nazo kutoka kwa vyanzo vyao vya habari ni kuwa, katika mikoa 23 hali ya CCM ni mbaya na inaupinzani mkali sana, kwani wakazi wa mikoa hiyo hawana imani na CCM, avumae huko ni UKAWA na Lowassa.
Pia wamegusia upande wa pili ambako ni Zanzibar, wamedai CCM Zanzibar imewaharibia mazingira kwa kuwakamata Mashehe kwa muda mrefu bila ya kuhitimisha hata ingebidi kuwaachia.
Zanzibar kuna mtihani mgumu sana alisikika mmoja wao akisema, kubwa linalotegemewa kuwashawishi wananchi ni kutumia miradi iliyokwisha na waepuke kabisa kuweka ahadi au kugusia mambo ambayo waliyawekea ahadi lakini hayakutekelezwa.