Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,882
- 141,503
Taxify ni ride-hailing company kama ilivyo Uber, Lyft, na zinginezo kama hizo.
Ni kampuni inayotokea/ iliyoanzishwa huko Estonia.
Hapa Tanzania/ Dar nadhani ndo imeingia muda si mrefu uliopita. Nadhani ni mwezi au miezi michache sana iliyopita.
Bei zao zipo chini sana kulinganisha na Uber. Lyft wao bado hawajafika hapa Tanzania.
Kwa wasiojua, Lyft ndo mshindani mkubwa sana wa Uber kwa Marekani, ambapo ndo nyumbani mwa hizo kampuni mbili.
Hawa Taxify bado sijawatumia. Nimejaribu kuangalia kuona kama kuna madereva karibu na eneo ambalo nipo lakini sijaona hata mmoja.
Ningependa kupata maoni juu ya huduma zao kama kuna watu ambao tayari washazitumia.
Jumamosi njema.