Taxation of mobile communications: The case of Turkey

Namnukuu Dr Mgimwa waziri wa fedha
WAZIRI wa Fedha, Dk.William Mgimwa, amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya Sh 1,000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu ya kiganjani. Alisema serikali inaendelea kupokea maoni kuhusiana na suala hilo.

Dk. Mgimwa alisema jana kuwa tangu itolewe kauli hiyo yamekuwapo manung'uniko mengi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo watumiaji wa mitandao ya simu.

Alisema serikali haikuwa na nia mbaya isipokuwa ililenga kuboresha na kuongeza ukusanyaji wa kodi na kukuza uchumi nchini.

"Watumiaji watakuwa wanakatwa Sh33.35 kwa kutwa nzima ambayo ni sawa na Sh 100 kwa siku tatu, hatua itakayosaidia kuboresha maeneo mengine ya kukuza uchumi," alisema.

Alisema tozo hiyo ililenga kupatikana Sh bilioni 160 kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha miundombinu ya barabara vijijini, maji na umeme. http://www.mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=8340:dk-mgimwa-zungumzia-tozo-ya-sh-1000-simu-za-mkononi&catid=8:siasa&Itemid=57

Kwanza nahisi kausoma huu uzi, lakini kwa nini anataka kuua mawasiliano kwa kujenga barabara? kwenye document aliyoweka mkuu EMT inaonyesha kwamba telecoms ukuza GDP in Afrika kwa karibi 10% yeye alikuwa wapi sasa anaanza kudata hivyo
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Siyo elfu 36 tuu. Ukitumia M-Pesa au benki yako kuhamisha zaidi ya sh. 30,000 utakatwa kodi pia: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/489275-kodi-mpya-barua-ya-tra-kwenda-kwa-mabenki.html

mkuu jana nimetoa m-pesa 50000 nikashaangaa nimebakiwa 447800 kwasababu nilikua na sh 500000 ktk m-pesa yangu, kwa mantiki hiyo sh 50000 inakatwa 2200 kitu ambacho before hakikua hivyo cuz gharama yake ingekuwa ni sh 1000 tu, sasa hivi wameamua kutumaliza watu wa chini kabisa, hizi m-pesa, tigo-pesa nk zimeshakuwa ni mzigo tena, sijui tunaelekea wapi na hii sekta yetu ya mawasiliano?sijui kama wamefanya ka utafiti lau kadogo kutizama impact ya kitu walichokianzisha au wamekurupuka as usual
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mbona wanachukuwa pesa nyingi sana ?!! hiyo hela ni ndefu kweli wanachukuwa ya nini? haya mambo ya kibank sio kufanya hivyo

mkuu ata mimi nimeshangaa sana nafikiri kuanza kutumia tena mfumo wa kibenki kama zamani cuz hizi gharama siwezi kuzimudu kwa sasa, maisha yatazidi kuwa magumu sana huku tunakoelekea cuz wanaotakiwa kulipa kodi stahiki hawalipi wanazidi kukimbiza na sisi mafukara.
 
EMT

Mchango mzuri sana. Umenipa mawazo mapya ya kuishauri Serikali sababu ambazo zinaifanya kodi hii kupingwa kabla ya hata mwezi mmoja kuisha tangu ianzishishwe.

Mkuu, mawazo mapya ya kuishauri serikali? Serikali ipi?
 
Last edited by a moderator:
Mbona wanachukuwa pesa nyingi sana ?!! hiyo hela ni ndefu kweli wanachukuwa ya nini? haya mambo ya kibank sio kufanya hivyo

Mkuu, serikali imeamua kutumaliza. Jana nimechukuwa 20000 tiGO pesa, nikakatwa 1350.Hii kodi ni sawa na 6.75%!
 
mkuu ata mimi nimeshangaa sana nafikiri kuanza kutumia tena mfumo wa kibenki kama zamani cuz hizi gharama siwezi kuzimudu kwa sasa, maisha yatazidi kuwa magumu sana huku tunakoelekea cuz wanaotakiwa kulipa kodi stahiki hawalipi wanazidi kukimbiza na sisi mafukara.

Kuna baadhi ya watu wanadai kuwa hizo kodi ni kulamizimisha watu waanze tena kutumia benk za kawaida.

Inadaiwa kuwa mpesa imefanya watu wengi waache kutumia mfumo wa kawaida wa kibenki
 
Soma hapa chini mkuu...

Wamiliki wa simu kutozwa 14.5%

Hiyo ndio habari nilikua nimeigusia pale awali...
WAMILIKI WA SIMU KUTOZWA 14.5% KUCHANGIA ELIMU TANZANIA. JE MDAU HII IMEKAA SAWA?

WAKATI hali ya maisha ikizidi kupanda kila kukicha,Serikali imepanga kuwatoza watumiaji wa simu za mkononi ili kupata fedha za kugarimia elimu. Wamiliki wa siku za mkononi nchini Tanzania watatozwa asilimia 14.5.

Akizungumza Bungeni jana Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema kwamba tozo hiyo itakuwa chanzo kipya cha mapato ya Serikali, Dk Mgimwa alisema Serikali inakusudia kutoza gharama hizo kwa watumiaji wa simu zote za mkononi kuanzia mwezi ujao ikiwa ni pamoja na kutoza ushuru wa bidhaa zote za kiwango hicho kwenye huduma zote za simu za kiganjani, badala ya muda wa maongezi peke yake.

"Katika ushuru huu, asilimia 2.5 zitatumika kugharimia elimu hapa nchini... Hatua hii imezingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali," alisema Dk Mgimwa.

Mwandishi wa Habarimpya.com akiwa Bungeni Dodoma anaripoti kwamba Kama vile haitoshi, Waziri Mgimwa alitangaza kuongeza wigo wa kutoza ushuru wa bidhaa kwenye huduma za simu za mezani (TTCL) na zisizokuwa na waya.

Pia waziri alitangaza kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi.

Katika hatua nyingi Waziri Dk Mgimwa alisema kwamba Mapendekezo hayo ya ni utekelezaji wa ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, (CAG)Ludovick Utouh.

Katika Ushauri huyo CAG aliwai kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itafute vyanzo vipya vya kodi ili kuongeza mapato ya Serikali katika mwaka wa fedha wa 2013/14.

Miongoni mwa maeneo ambayo Ripoti ya CAG iliyoishia Juni 30, mwaka jana ilishauri kuangaliwa, ni pamoja na huduma za kuhamisha fedha kwa njia ya simu za kiganjani maarufu kama M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Easy Pesa.

CAG alishauri kuwa kampuni za simu kulipa kodi ya zuio ya malipo ya kamisheni inayolipwa kwa wanaofanya biashara hiyo na kodi hiyo ya zuio ipunguzwe kutoka katika kodi ya mwisho itakayotakiwa kulipwa na kampuni za simu.

SOURCE: HABARIMPYA
 
kwahio it means hio ya vifurushi kupanda kwa kiasi cha tshs 100 na bundles kupanda kwenye net ni kodi walizopigwa wenye makampuni nao hawakufanya ajizi bali kumsukumia mtumiaji ?, Duh all in all mi naona ni vema tukapata clarification zaidi juu ya hizo kodi nyingine pia, kama ni kweli vifurushi vimepanda sababu ya hizi kodi au hizi kampuni nazo zimepata fursa ya kutukamua

Labda inahusiana na hii: FAHARI YA KUSINI MWA TANZANIA: WAMILIKI WA SIMU KUTOZWA 14.5% KUCHANGIA ELIMU TANZANIA. JE MDAU HII IMEKAA SAWA?
 
Hiyo ni kodi tofauti na hiyo ya bank kwneye barua

Mkuu unawezafafanua?

Ina kuna aina ya kodi tatu hapa?

  1. Kodi ya sh. 1000 kwa mwezi kwa simkadi moja
  2. Kodi ya asilimia 14.5?
  3. kodi iliyosemwa kwenye ile barua ya TRA
Mie zimenichanganya.
 
huenda ikawa ni hio lakini zile bundles lets say kifurushi cha tshs 500/= (14.5% ingebidi iwe tshs 72.5 na sio kupanda kwa tshs 100) na zile bundle za net zilizopanda buku tano sijui justification ipo wapi I mean je hio yote buku tano na tshs 100/= inakwenda kwenye elimu ?

Mi naona hapa serikali imamua kuwakamua wananchi wake na hizi kampuni zimeona fursa ya kujiongezea chenji kwa mgongo wa kodi na kusukumia lawama kwamba sio sisi ni nchi yenu na kodi zenu (wakati wote ni wale wale tu).
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu unawezafafanua?

Ina kuna aina ya kodi tatu hapa?

  1. Kodi ya sh. 1000 kwa mwezi kwa simkadi moja

  1. Kodi ya asilimia 14.5?
  2. kodi iliyosemwa kwenye ile barua ya TRA
Mie zimenichanganya.

1. Kodi ya sh. 1000 kwa mwezi kwa simkadi moja
HII ITAKATWA KWENYE KILA LAINI YA SIMU YA MKONONI NCHINI [ kumbuka simu za mkononi yaani simu kadi] kila mwezi.

2. Kodi ya sh. 1000 kwa mwezi kwa simkadi moja
Pamoja na makato mengine, kila mtumiji wa internet nchi basi zili ghalama za internet unazolipa kutakuwa na 14.5% kama kodi, hiii itachomekwa kwenye ma-bundle bundle za internet zitapanda uku kupunguzwa ukubwa ili kuingiza hiyo 14.5% itakayokwenda serikalini

3. kodi iliyosemwa kwenye ile barua ya TRA
Hii itakatwa kwa kila mtu anayetumia huduma kama mpesa kila unapotumia, [ sasa sijui ina max cap au wanatakata tu kwamba hata kama umetoa 20milion bado wanakata kwa asilimia iliyosemwa kwenye kodi]
katika kodi mbaya kuliko zote ni hii, maana wanakula pesa ndefu sana, hii huduma ya mobile money itakuwa very soon

HAPO kuna VAT na mikodi mingine kwenye huduma zinazokatwa kodi ya kwanza na ya pili
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hii Kodi inapingwa sana kwasababu sio Progressive. We huwezi kumchaji mtu anayetumia millioni 2 kwenye simu ya mkononi Tshs 1000 na ukamchaji anayetumia Tzs 1000 Tzs 1000. Ni kichaa tu ndo anaweza kukubali hii.

Kama wangeweka kwa kiwango cha utumiaji bado wangepata even more. Mfano:

Ukitumia kuanzia Tzs 0 mpaka Tzs 1000 kwa mwezi kodi inakua 0 Tzs
ukitumia kuanzia Tzs 1001 Mpka Tzs 5000 kwa mwezi kodi ni Tzs 50
Ukitumia kuanzia Tzs 5001 mpaka Tzs 10000 kwa mwezi unalipa Tzs 100
Ukitumia kuanzia Tzs 10,001 Mpaka Tzs 15,000 kwa mwezi kodi unalipa Tzs 300
Ukitumia kuanzia Tzs 15,001 Mpaka Tzs 30,000 kwa mwezi unalipa Tzs 500
Ukitumia kuanzia Tzs 30,001 Mpaka Tzs 100,000 kwa mwezi unalipa Tzs 1000
Ukitumia kuanzia tzs 100,001 mpaka tzs 500,000 kwa mwezi unalipa tzs 2,000
Ukitumia above Tzs 500,001 unalipia Tzs 10, 000

Naamini wangezidi target yao ya Billion 8 TZS.

Ahuitaji kufika darasa la pili kuona hili.
 
Potelea kando hata kama wangewachaji wanaotumia zaidi ya laki tano Tzs 30,000 bado wangetoa tu bila malalamiko na hapo bado wangeingiza billion kadhaa
 
Hii Kodi inapingwa sana kwasababu sio Progressive. We huwezi kumchaji mtu anayetumia millioni 2 kwenye simu ya mkononi Tshs 1000 na ukamchaji anayetumia Tzs 1000 Tzs 1000. Ni kichaa tu ndo anaweza kukubali hii.

Kama wangeweka kwa kiwango cha utumiaji bado wangepata even more. Mfano:

Ukitumia kuanzia Tzs 0 mpaka Tzs 1000 kwa mwezi kodi inakua 0 Tzs
ukitumia kuanzia Tzs 1001 Mpka Tzs 5000 kwa mwezi kodi ni Tzs 50
Ukitumia kuanzia Tzs 5001 mpaka Tzs 10000 kwa mwezi unalipa Tzs 100
Ukitumia kuanzia Tzs 10,001 Mpaka Tzs 15,000 kwa mwezi kodi unalipa Tzs 300
Ukitumia kuanzia Tzs 15,001 Mpaka Tzs 30,000 kwa mwezi unalipa Tzs 500
Ukitumia kuanzia Tzs 30,001 Mpaka Tzs 100,000 kwa mwezi unalipa Tzs 1000
Ukitumia kuanzia tzs 100,001 mpaka tzs 500,000 kwa mwezi unalipa tzs 2,000
Ukitumia above Tzs 500,001 unalipia Tzs 10, 000

Naamini wangezidi target yao ya Billion 8 TZS.

Ahuitaji kufika darasa la pili kuona hili.

Nakubaliana na wewe japo kwenye RED ni hela nyingi sana kwa kodi ya mawasiliani tungetumia kiwango cha 1.1% kama wanavyofanya NEVADA
 
Back
Top Bottom