POSHO MAVYEO
JF-Expert Member
- Jun 28, 2011
- 371
- 112
Namnukuu Dr Mgimwa waziri wa fedha
Kwanza nahisi kausoma huu uzi, lakini kwa nini anataka kuua mawasiliano kwa kujenga barabara? kwenye document aliyoweka mkuu EMT inaonyesha kwamba telecoms ukuza GDP in Afrika kwa karibi 10% yeye alikuwa wapi sasa anaanza kudata hivyo
WAZIRI wa Fedha, Dk.William Mgimwa, amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya Sh 1,000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu ya kiganjani. Alisema serikali inaendelea kupokea maoni kuhusiana na suala hilo.
Dk. Mgimwa alisema jana kuwa tangu itolewe kauli hiyo yamekuwapo manung'uniko mengi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo watumiaji wa mitandao ya simu.
Alisema serikali haikuwa na nia mbaya isipokuwa ililenga kuboresha na kuongeza ukusanyaji wa kodi na kukuza uchumi nchini.
"Watumiaji watakuwa wanakatwa Sh33.35 kwa kutwa nzima ambayo ni sawa na Sh 100 kwa siku tatu, hatua itakayosaidia kuboresha maeneo mengine ya kukuza uchumi," alisema.
Alisema tozo hiyo ililenga kupatikana Sh bilioni 160 kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha miundombinu ya barabara vijijini, maji na umeme. http://www.mtanzania.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=8340:dk-mgimwa-zungumzia-tozo-ya-sh-1000-simu-za-mkononi&catid=8:siasa&Itemid=57
Kwanza nahisi kausoma huu uzi, lakini kwa nini anataka kuua mawasiliano kwa kujenga barabara? kwenye document aliyoweka mkuu EMT inaonyesha kwamba telecoms ukuza GDP in Afrika kwa karibi 10% yeye alikuwa wapi sasa anaanza kudata hivyo
Last edited by a moderator: