Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Malalamiko mengi yanayojitokeza sasa hv kwenye sekta ya Elimu hasa kwenye hizi Shule binafsi ni ya kujitakia, kwa sababu tulifanya kosa kubwa sana kuruhusu Elimu kuwa Biashara, yaani mtu anafungua Shule kama kitega Uchumi kama vile anajenga hoteli ambayo anategemea imrudishie fedha zake pmj na kumpatia faida, sasa hilo ni kosa kubwa sana na halisameheki hata kwa Mungu, kwani Elimu ni haki ya binadamu, ni huduma kwa jamii na inapaswa kubakia hivyo!
Matokeo yake ndo hayo unaona kama vile zilivyo Biashara nyingine, wenye Shule wanaweka Mihula mitatu badala ya 2 ili wavune fedha zaidi, wazazi kubebeshwa gharama nyingi za nyongeza hata zisizo za lazima ili Wafanyabiashara wapate faida n.k lkn cha ajabu wakati huo huo wenye Shule hawataki kulipa kodi, sasa kwa nini wkt ni biashara kama nyingine tu?
Mlm.Nyerere hatukumuelewa kwenye mambo mengi sana na ndio maana tumevuruga kila kitu, Dunia nzima Elimu ni huduma kwa jamii na siyo Biashara ya kupata faida!