Tatizo sio afya ya mgombea, Ila...

Tatizo sio afya ya mgombea, Ila...

2kimo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,029
Reaction score
2,072
Naona watu wengi wamekuwa wakiongelea afya ya mgombea wa Chadema na wengine wakilalamikia hilo au kuita wenzao mapepo au wanga kwa kutaka au kukuombea mabaya mzee Lowassa!

Kwa upande wangu pia afya ya mgombea wa chadema inanitia shaka, kwa sababu kuu zifuatazo:-

1. Sehemu kubwa ya kampeni zinaathiriwa na afya yake ambapo ameshindwa kuongea katika mikutano na inamlazimu kuwa na dakika chache sana za kuzungumza hivyo kuondoa nafasi ya wananchi kukipima chama cha Chadema na UKAWA kwa ujumla. Hii haimaaanishi kuwa tungependezewa na hoja zake lakini hata kujibu baadhi ya hoja tata dhidi yake na chama chake!

2. Lakini kwa kujiuliza vema, hivi kweli kwa afya ya mgombea wa Chadema hata katika kazi za mkataba katika ofisi yako binafsi unaweza kumpa Lowassa contract hata ya mwaka mmoja!

3. Kusahau na speed ya kureact katika mambo inafanya sehemu kubwa ya kazi zake zifanywe na mtu mwingine. Tazama anavyosaidiwa kupanda jukwaani, anafutwa mate, Sumaye anamsaidia kwa kumuongelea... Hivi hata tukimpitisha 25-10-2015 kweli yeye ndiye ataongoza nchi au atasaidiwa na Sumaye?

Najua kuna umri wa kustaafu na targets katika umri huo, sio kuwa mtu hawezi Fanya kazi lakini likelihood ya watu katika umri huo kuperform katika optimal level ni mdogo!

Lakini aina tofauti za maradhi zinawekewa vigezo katika kuendelea kutoa huduma. Ofisi anayotaka kuingia Lowasa ni ngumu, uimara wa afya yake ni kitu cha msingi sana! Parkinson's disease ni ugonjwa unaoathiri ubongo na kuinterfere sana na uwezo wa kufikiri, kumbukumbu na speed katika maamuzi, vitu ambavyo ni key katika afya ya kiongozi Mkuu wa nchi!

UKAWA na Chadema tambueni, watu hawamcheki Lowassa lakini wanafikiri nyinyi hamkuzingatia umuhimu wa afya ya mgombea wenu! Mmefanya kosa la kiutendaji katika kuchagua mgombea! Tunamuheshimu na kumuombea kiongozi huyu gwiji afya njema, lakini tunamuomba aelewe kuwa afya yake ni concern ya msingi kwetu! Hayuko fit kuwa rais.

Hata vyuo, kazi na maeneo mengi mtu angetakiwa kuleta vielelezo vya daktari juu ya ufit wa afya yake ya akili na mwili. Lowassa na Mbowe na waajiri katika makampuni yao wanajua umuhimu wa kipengele cha afya!
 
Suala siyo Lowassa. Issue hapo ni kufukuza ccm. Kwa namna yoyote ile. ccm out.
 
...
3. Kusahau na speed ya kureact ktk mambo inafanya sehemu kubwa ya kazi zake zifanywe na mtu mwingine. Tazama anavyosaidiwa kupanda jukwaani, anafutwa mate, sumaye anamsaidia kwa kumuongelea... Hivi hata tukimpitisha 25-10-2015 kweli yeye ndiye ataongoza nchi au atasaidiwa na sumaye?

...

Unao ushahidi wa kufutwa mate?!
 
Vigezo vya kitoto sana !, hv umesahau afya ya rais wa kenya ilivyokuwa , na kwa enzi yake rais F. Roosevelt wa USA je unajua alikuwa ktk hali gani kiafya kipindi anagombea ! ?, hujasoma hata historia au tatizo ni nini !?, jaribu kuwa mfuatiliaji kabla ya kuandika ukurasa mrefu wa maelezo !, people are fed up !, muda ukifika umefika hakuna cha msalia mtume !, mtabaki kutumia taasisi za utafiti kuupotosha ukweli usiofichika !
 
Tunataka mabadiliko,tumewachoka watetea matumbo yao!!!
 
Rais wao hatakuwa akikagua magwaride siku za sikukuu au hata akienda nchi za nje ataishia kwenye dhifa tu!
 
Vigezo vya kitoto sana !, hv umesahau afya ya rais wa kenya ilivyokuwa , na kwa enzi yake rais F. Roosevelt wa USA je unajua alikuwa ktk hali gani kiafya kipindi anagombea ! ?, hujasoma hata historia au tatizo ni nini !?, jaribu kuwa mfuatiliaji kabla ya kuandika ukurasa mrefu wa maelezo !, people are fed up !, muda ukifika umefika hakuna cha msalia mtume !, mtabaki kutumia taasisi za utafiti kuupotosha ukweli usiofichika !

Hii ni Tanzania wewe sio Kenya wala USA.
 
Tumechoka ahadi hewa za ccm. Lowassa katuonyesha mabadiliko nchini yanawezekana na hatutorudi nyuma.
 
Back
Top Bottom