Tatizo si malipo, wananchi hawana imani na Serikali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo si malipo, wananchi hawana imani na Serikali.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mjomba wa taifa, Jul 30, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa ufupi mchambuzi yeyote wa siasa anaweza kusema kuwa migomo ambayo imekuwaikilipuka kila kukicha nchini Tanzania imekuwa ikisababishwa na wananchi kupoteza imani na Serikali iliyopo madarakani wala sio malipo duni.

  Siku zote iwapo viongozi hawakubaliki katika jamii yoyote ile licha ya kutumia kila aina ya mbinu kama vile wizi, ulaghai na hata mabavu hakutakuwepo na amani. Kila siku tutakuwa tanawasingizia CHADEMA kuwa ndio wanaochochea migomo sekta mbalimbali. Ukweli ni kuwa hata hao wanaogoma wanaakili zao timamu ambazo hawahitaji nyongeza ya yoyote. Natumaini migomo ingeweza kuwa mikubwa zaidi ya hapo isipokuwa wale wote walioajiriwa katika sekta binafsi hawana nafasi ya kufanya hivyo kwa kuhofia marungu ya waajiri wao wengi wao katika makampuni ya kibepari yanayopewa jeuri na Serikali.

  Serikali lazima ijitazame katika mbinu ilizotumia kuingia madarakani hususan awamu hii ya nne.

  Madai ya kuongezewa posho au mishahara ni dalili tu za ugonjwa wala sio chanzo.
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,975
  Likes Received: 37,566
  Trophy Points: 280
  Mkuu unachoongea ni kweli kabisa na mawazo yako ndio mawazo yangu.Haya yote yanayotokea ni viashiria tu vya watu kuwa wamechoka na watawala wa sasa na kuwa wazi zaidi ni kuwa watu wameichoka ccm.Hii yote ni kutokana na ufisadi na tofauti kubwa ya kipato iliyopo kati ya wanasiasa(viongozi) na watanzania wengine.Na kibaya zaidi ni hii tabia ya watu kufanya ufisadi na kutokuchukuliwa hatua.

  Watu wanaona anasa inayofanywa na viongozi na jinsi viongozi hao wanavyohujumu nchi.Watu wanaona jinsi rasilimali za nchi zinavyofujwa na watawala.Watu wanaona jinsi nchi inavyopoteza mapato kutokana na mikataba ya kifisadi kwa manufaa ya wachache.Watu wanashuhudia mahekalu ya viongozi wanayoyajenga ambayo hayalingani na vipato vyao.

  Kwa kifupi, kwa mambo kama hayo yanayofanyika ni vigumu kuwaambia watu kuwa umasikini wetu ni kwasababu nchi yetu ni maskini na watu wakakuelewa.Ni vigumu kuwaambia watumishi wa umma serikali haina uwezo wa kuwalipa vizuri nao wakakuelewa.

  Mwisho kabisa nasema hatima ya nchi hii ni machafuko siku si nyingi.Watu watadai haki kwa nguvu na watakuwa tayari kwa lolote.Serikali inachofanya sasa ni kuahirisha tu machafuko kwa siku zijazo na si kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
   
Loading...