Street Hustler
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 2,276
- 4,523
Habarini wandugu?
Katika harakati za kujikomboa kiuchumi kupitia ufugaji kisasa nilipata Wazo zuri na kubwa kwangu katika ufugaji wa nguruwe, nlipita kwenye mabenki na taasisi za serikali na binafsi zinazowawezesha wakulima na wafugaji ikaonekana kikwazo natakiwa niwe na eneo kwanza, nikaona isiwe tabu nliona ni bora nipate eneo LA ufugaji ili niweze kuwa mtu wa kusikilizwa katika project yangu nliangalia mkoa nnaoweza kuufanya ule mradi uwe salama nikaona ni morogoro katika mji wa ifakara hukuhuku nikapata heka mbili za kuanzia ile project 2mil zangu zikaenda hvyo kwenye ardhi nikiamini kwenye ule mradi ulivyokuwa wakati napita serikalini na taasisi zake na mabenki wakaniambia angalau nipate sehemu ya ardhi ntakayoanzia.
Sasa baada ya kununua hilo shamba nkaenda wizarani niwaone wale wadau ili waniunganishe na partners wao ili niweze kudevelop kupitia wao cha ajabu wizarani pale maneno nliyokuwa nayapata nkasema bora hata nisingekuja huku watu wa mifugo hawajui a wala bee ya jinsi ya kunidevelop nikaona isiwe shida nkawatafuta Baraza LA uwezeshaji nako nikaambulia sound tuu nkaenda zile taasisi za kilimo na ufugaji ambazo zinasaidia kuboresha Mawazo na muwezeshaji huko napo nkaambiwa mpaka niwe na nyumba nikaona hee!
Nkaikumbuka ile bank ya kilimo TADB huko mzee ni shidah naambiwa nikatafute wafugaji au wakulima wenzangu tutengeneze kikundi cha watu kisichopungua watu 15, kiwe na katiba Mara taarifa za fedha ziwe zimekaguliwa na mkaguzi wa hesabu za serikali kwa kipindi walau miaka mitatu cha ajabu nlipokuja kuumia ni pale nlipoambiwa eti nguruwe hayupo kwenye mpango wa kufadhili katika benki hyo.
Nkaona isiwe tabu nikaenda ofisi za halmashauri nione wanaweza vipi kunishika mkono nako huku n Yale Yale ukifika baada ya wao waseme njia zipi wanaweza kunishauri ili nifanikiwe kwanza wanaishia kunipongeza tuu ooh n mpango mzuri yan umejitahidi sana hapo ndo mwisho wao wanarudi kule Mara tafuta kikundi au zunguka zunguka tuu unaeza pata mfadhili.
Hivi jamani hawa wenye dhamana ya kujikomboa kiuchumi hili taifa wanafanya NINI pesa nyingi nimeona katika pitapita zangu Hz naona zinaliwa kwenye kuandika taarifa,kukaa vikao na semina elekezi yaan kama pesa inafika kwa walengwa n 20% ya pesa ndo zinafika.
Kama wewe umewahi kukutana na changamoto hizi ebu niambie ulijikwamua nazo kivipi