Wakuu habari,
Kama sikosei tangu majuzi kumekuwa na tatizo la thread moja kupostiwa zaidi ya mara moja,mda mwingine hadi mara tano thread hiyo hiyo,mtoa mada huyo huyo,muda huo huo na jukwaa hilo hilo.
Hili tatizo linatokana na mitandao yetu ama maboresho yanayokuwa yanafanyika katika jukwaa letu pendwa ndio huwa yanasababisha hili.?
Maana unapost uzi,unaambiwa something went wrong unaendelea na kuendelea nakuendelea kurudia kupost kumbe uzi ushaenda ila taarifa unayopata inakuambia tofauti.
Si ajabu na huu ukajitokeza zaidi ya mara moja.