Tatizo ni elimu yetu au kitu gani?

Tatizo ni elimu yetu au kitu gani?

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,305
Wakuu,mtanisamehe tu kwani mimi siyo mwandishi mzuri hata kidogo.
Wanasema nchi ikiwa na wasomi wengi haitawaliki kirahisi.

Hoja yangu ni huu uhaba wa ajira kwa wahitimu,wengi tunaililia sirikali kushindwa kutuajiri. Najiuliza haya machache,hivi elimu ni nini? Inatusaidia kuyakabili mazingira?

Unazaa mtoto unalea kidogo tu unaanza kupeleka nasare,msingi,mpaka chuo kikuu kwa gharama kubwa na madeni juu.Anahitimu huko,anarudi nyumbani unaendelea kulea.Ajira hana.

Kwa swala la elimu kuna rasmi ya darasani inayozingatia viwango na masharti yake na isiyorasmi inayotegemea uwezo wa kumudu kwako,mfano ni usasi,uhunzi,ususi,na mengineyo. Engineer huyu ana vyeti, huyu kasomea gereji tu.Wote ni wahandisi mmoja ana vyeti wapili anaujuzi.

Huyu mwenye ujuzi ni rahisi kujichanganya hata chini ya mwembe akafungua karakana,huyu mwenye vyeti anasaga lami kusaka ajira.! Duh! Sisemi tusisomeshe vijana,elimu muhimu sana,nawaza tu hapa hivi hatuwezi kufanya kitu kupambana na hii hali? Au hatuna utashi wa kisiasa kuwawezesha vijana wajiajiri!

Kuna hili balaa la utumishi serikalini na uhakiki usioisha,wa vyeti,majina,dini,ndoa mpaka kabila. Ukifanikiwa kubaki na hiyo ajira mateso ni mengi mno,makato yasiyoeleweka ya mwenge,kodi,na kila anachotaka mwajiri,bado mifuko ya hifadhi isiyolipa pesa zako unapozihitaji. Mshahara wenyewe sasa!!ukilalamika kidogo tu wanakula kichwa.

Tunapohangaika na uhuru wa kisiasa nadhani tungeanza kushughulikia uhuru wa kiuchumi kwanza.

Tunadhalilika sana wananchi,tutafakari !
Tunaondokanaje na hili?
 
Ni kitu cha msingi sana umeongea, Na watu pia inabidi wabadili mtazamo kwamba ukisoma lazima uajiriwe na serikali.
 
Juzikati hapa,nimemkuta bwana mmoja ana masters ya sheria eti hajui lakufanya maana hajaajiriwa!duh niliumia lakini nimsaidieje?ametune akili yake hivyo.
 
Wakuu,mtanisamehe tu kwani mimi siyo mwandishi mzuri hata kidogo.
Wanasema nchi ikiwa na wasomi wengi haitawaliki kirahisi.
Hoja yangu ni huu uhaba wa ajira kwa wahitimu,wengi tunaililia sirikali kushindwa kutuajiri. Najiuliza haya machache,hivi elimu ni nini? Inatusaidia kuyakabili mazingira?
Unazaa mtoto unalea kidogo tu unaanza kupeleka nasare,msingi,mpaka chuo kikuu kwa gharama kubwa na madeni juu.Anahitimu huko,anarudi nyumbani unaendelea kulea.Ajira hana.
Kwa swala la elimu kuna rasmi ya darasani inayozingatia viwango na masharti yake na isiyorasmi inayotegemea uwezo wa kumudu kwako,mfano ni usasi,uhunzi,ususi,na mengineyo. Engineer huyu ana vyeti, huyu kasomea gereji tu.Wote ni wahandisi mmoja ana vyeti wapili anaujuzi.
Huyu mwenye ujuzi ni rahisi kujichanganya hata chini ya mwembe akafungua karakana,huyu mwenye vyeti anasaga lami kusaka ajira.! Duh! Sisemi tusisomeshe vijana,elimu muhimu sana,nawaza tu hapa hivi hatuwezi kufanya kitu kupambana na hii hali? Au hatuna utashi wa kisiasa kuwawezesha vijana wajiajiri!
Kuna hili balaa la utumishi serikalini na uhakiki usioisha,wa vyeti,majina,dini,ndoa mpaka kabila. Ukifanikiwa kubaki na hiyo ajira mateso ni mengi mno,makato yasiyoeleweka ya mwenge,kodi,na kila anachotaka mwajiri,bado mifuko ya hifadhi isiyolipa pesa zako unapozihitaji. Mshahara wenyewe sasa!!ukilalamika kidogo tu wanakula kichwa.
Tunapohangaika na uhuru wa kisiasa nadhani tungeanza kushughulikia uhuru wa kiuchumi kwanza.
Tunadhalilika sana wananchi,tutafakari !
Tunaondokanaje na hili?
Tatizo sio kujiajiri bali elimu yetu imemuandaaje mtu kujiajiri labda tuanzie hapo.mfano mtu amesomea ualimu huyu asilimia kubwa lazima ategemee ajira kutoka serikalini au shule binafsi ambazo ni chache kuliko wahitimu,kitu cha msingi mi nafikili serikali ingefanyia marekebisho mitaala ya elimu yetu kwanza ili iwaandae wahitimu kwaajiri ya ajira binafsi,pia serikali ingejaribu kuweka utaratibu kwamba mwanafunzi yeyote akimaliza kidato cha nne kabla hajajiunga na masomo ya advance basi lazima apitie veta mwaka mmoja ndo aendelee na masomo mengine hapo itawasaidia wanafunzi wote wanaoishia form four na wale wanaoendelea kusoma kua na elimu ya ujuzi wa kitu furani hata akimaliza chuo hatokaa tena mtaani kwan atakua anakitu cha ziada kichwani hivyo ataweza kujiajiri mwenyewe.lakini kama tutategemea tu elimu yetu tutasububiri sana kwani haituandai kwa kujiajiri bali kuajiriwa hususani baadhi ya fani.
 
Wazo zuri.Tunahitaji pia ubunifu,uthubutu,na hamasa.
 
Ni kweli lakini vitu kama hivi vinaitaji mjadala wa kitaifa nafikiri kama viongozi wetu wangeweza kusimamia hili malalamiko ya ajira yangekua machache sana uzuri wake kwasasa kila mkoa unachuo cha veta kama serikali ingeweza kuwekeza angalau kila mkoa uwe na vyuo angalau viwili vya veta hili zoezi lingekua zuri sana hata hii kauli mbiu ya tanzania ya viwanda ingekua nyepesi sana.au hata wakijaribu tu kwa vyuo vya veta vilivyopo pia lingewezekana kwa short kozi.
 
Sasa kwa vile hawatafanya hivyo,tufanyeje ?namaanisha huku kwenye ngazi ya jamii kubwa inayoathirika maana hao tunaotamani watusaidie kwao hili siyo mada,mada yao ni kuongeza wapiga kura kwa gharama yoyote na kila wakiwa dhalili kwao ni fursa.Tunatokaje hapa?
 
Ndugu yangu swala la ajira kwa jamii hususani ktk nchi zetu hizi za dunia ya tatu lazima tupambane tu vyovyote iwezekanavyo ingawa maendeleo yatakua ya mzunguko sana kwakua kila unapoitaji kujiajiri lazima ukute unaigusa serikali kwa namna moja au nyingine maana hata nchi za wenzetu wananchi wanaweza kujiajiri kwakua kuna mgongo wa serkali nyuma yao,mfano chukulia mtu unataka kujiajiri ktk kilimo unakuatana na shida ya soko,ukitakabiashara unakutana na shida ya mtaji unafanyaje hapo?
 
Sasa hizo zote ni changa moto ambazo lazima serikali ipambane nazo kwanza mfano chukulia zao la korosho kwasasa serikali walivyolisimamia linavyoleta manufaa kwa wakulima!hapo hapo angalia wakulima wa mbaazi wanavyopata tabu ya soko!sasa kama serikali ikipanga inawezekana tu mkuu
 
Ndugu yangu swala la ajira kwa jamii hususani ktk nchi zetu hizi za dunia ya tatu lazima tupambane tu vyovyote iwezekanavyo ingawa maendeleo yatakua ya mzunguko sana kwakua kila unapoitaji kujiajiri lazima ukute unaigusa serikali kwa namna moja au nyingine maana hata nchi za wenzetu wananchi wanaweza kujiajiri kwakua kuna mgongo wa serkali nyuma yao,mfano chukulia mtu unataka kujiajiri ktk kilimo unakuatana na shida ya soko,ukitakabiashara unakutana na shida ya mtaji unafanyaje hapo?
Tuko pamoja kiongozi,ila sasa tukikaa tusubiri hawa wapanga sera wetu ni dhahiri hawatatusaidia na sisi ndiyo tunaodhalilika na watoto/wazazi wetu. Je huoni kama kulitambua tatizo ni mwanzo wa kulitatua? Sasa tufanye nini kwao hili haliwagusi.
Tunaolilia uhuru wa kiuchumi ni sisi.
 
Ni kweli mkuu unajua mfano mim mwenyewe ni muhanga wa ajira nimehitimu chuo kikuu ktk fani ya elimu tangu 2016 nimejaribu kuomba ajira ktk shule binafsi nimekosa kutona na masomo ya sanaa nimefikilia kufanya biashara nimeshindwa mtaji,nimefikilia kulimo sina shamba pia lazima uwe na mtaji pia kula na matumizibmengine sasa unabaki tu kua kituko mtaani watu wanakunyooshea vidole kua amesoma lakini hana lolote bora asingesoma sasa ndo changamoto zenyewe hizo zinazotukuta.
 
Aisee!pole sana.
 
Ukishafungua karakana utaajiri MBUZI ??

( Hivi kwani watu mmekuwa MBUGILA sana karne hii ? )
 
Back
Top Bottom