Vipi, ana"tawala" kama nyumbani kwake??!!
Hapana, ila ofisi yake haiwi run professionally enough. Na sikupenda alivyo handle zoezi la ubadilishaji passport ambalo Foreign Ministry na Ubalozi wa DC wamemtwika mpaka leo. Nadhani angepewa ubalozi wa kawaida na wenyewe ungezembea.
Ubalozi wa DC uliaandaa siku maalum ya Watanzania kuja kutoa pasi miaka miwili iliyopita. Kazi ikapangwa kufanyika kwenye ukumbi wa kanisa la Mtanzania mmoja, Mchungaji Mama Perusi Muganda, ambae alijitoea, kule Hollis, Queens, New York. Mahiga ambae ameipokea kazi hii (mpaka leo), hakuja, akatuma deputies wake na maofisa kutoka DC.
Ilikuwa ni moja ya siku niliyoshuhudia uozo wa Serikali, ukiritimba – na mazingira yanayofanana na ufisadi – mbaya kuliko zote nilizo pata ona.
Jamaa walikuja hawana fomu za kutosha za application. Wakaenda sijui kutafuta photocopy uswahilini, Hollis, Queens ndani, madongo kuinama, kwa kina LL CooL J na Senti 50 walikozaliwa huko. Na zile fomu huwa hazitolewi copy sasa za nyongeza sijui walizipata wapi. Kazi ikaanza saa saba. Saa nane wakapumzika, wakaenda kula. Saa tisa, mstari ni mrefu kuliko wa foleni ya unga wa yanga wa Reagan.
Moja ya tatu ya raia waliojaa holini ni Wahindi. Sileti urangi na ubaguzi, nivumilie kidogo. Maofisa mabosi mabosi wakaanza kuita Wahindi waje mbele ya mstari. Maofisa wakisha mhudumia Mhindi, Mhindi anasindikizwa nje. Naandika kwa kiapo cha ukweli tupu hapa.
Maofisa wengine wa ngazi za chini wakaanza kuwalalamikia wale vibosile. Kwa sababu wao (maofisa wadogo) ndio walikuwa kama security sasa, wana organize mistari na wanaungurumiwa na watu waliokuwa frustrated. Kikatokea ki-bifu cha nje nje kati ya mabosi na na hawa wengine. By the time kinapoa, Wahindi wote wamesha hudumiwa.
Mambo yakaenda shaghala bagala. Kuna foleni ya kuchukua namba na kuna foleni yenyewe haswa ya kupeleka application itiwe saini na muhuri. Vile vinamba vimeandikwa kwa mkono kwenye vikaratasi vilivyo chanwa chanywa. Navyo eti vikaisha! Lakini wengine waliofika baada yako unaona wanapewa vinamba. Watu wakiuliza kulikoni, unaambiwa alishikiwa namba. Mtu kaja saa nane! Ha ha aaaa! Unbelievable. Kwa hiyo ule mstari wa vinamba ukavunjwa, ikachukua masaa kama mawili kuchana chana kikaratasi vingine. Mstari ukaanza tena upya bila kujali nani alikuwa mbele au nyuma. Mimi nikaondoka saa kumi na moja, na foleni ilikuwa inaendelea.
Sasa hii ilikuwa ni kazi iliyoshirikisha ofisi ya Mahiga. Kwa kujitolea au kwa majukumu. Ningekuwa mimi Mahiga ningekuja ukumbini siku ile. Siku ya Jumamosi, sidhani kama alikuwa na mikutano UN. Na kama alikuwa nayo, ange schedule muda ambao hana mikutano UN.
Na mpaka leo, UN mission ya TZ, New York, bado wanaendelea kutoa pasi. Lakini wanaoenda pale wanalalamika ukiritimba mtupu. Kuna kina dada wako pale huwa wanasambaza a word of mouth "mwambieni Juma passport yake imefika." Tena ukitaka, kama unamjua, unaweza kupewa umpelekee bila Juma kuidhinisha.
Kwa hiyo, ufanisi wa ule ubalozi wa Mahiga nao ungeweza kuwa improved, hauwi run vizuri. Labda wengine we are asking too much. Tunalalamika mno. Tumeharibika kwa kukaa nje. Tumezoe mno professionalism kwenye maofisi. Lakini mimi sijuti hata kidogo kuwa spoiled kwa namna hii. Matatizo makubwa ya nchi yanaanzia kwenye madogo madogo huku chini chini. Ndio haya ya kuyarekebisha.
Niliyoshuhudia hapo juu sikuwepo peke yangu ukumbini pale. Walioona vinginevyo wanikamate uongo. If you saw this debacle that day you know what I'm talking about.
Wale maofisa waliokuwa wanaita Wahindi mbele ya mstari ni wafanyakazi wa foreign affairs. Walitokea ile idara inayotoa maofisa wengi wa ubalozi. Ni kinyume cha sheria za nchi kuanika majina ya maofisa wa hiyo idara, kama unawajua. Vinginevyo ningewataja majina hapa. Na wanitafute na wenzao waniue. Kuna wengine niliwakoromea na walinimaindi. Lakini kuna mambo ya nchi ambayo hayawezi kubadilika bila watu kukubali kufa.
Yani inauma ile kinoma yani!