Tatizo ni Balozi Ngemera ama Wizara ya Membe?

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
Kwa muda wa miaka sasa Ubalozi wetu Ujerumani umekuwa kama boma la mmasai kuanzia jengo na hata watumishi wake .Ubalozi huu ni mmoja kati ya Balozi kubwa lakini ukifika utadhani si Ubalozi wenye hadhi .Jumba liko kia ajabu na watanzania hapa Ujerumani tumepiga kelele sana lakini alikuwa hapa Karume yeye ilikuwa safari tu hadi amekuja Ngemera sasa ni balaa mtu huyu .

Ujerumani tuna bahati mbaya sana kupata mabalozo vichwa maji ama hawajali ama hawajui wanacho kifanya .Ninajiuliza kwamba hata wakiwa mawaziri hapo Ubalozini sijui hawaoni hali hali halisi ya jengo lao hilo ama wao huwa wanawa perdiem yao na kuabudiwa na watumishi wa Ubalozi ila mazingira ya watumishi si kazi yao .

Majuzi mkewe Karume alikuwa ana vinjari hapo , waziri wa Utalii na hata Matilda katoka Ujerumani juzi lakini wote wana acha hali ikiwa duni kabisa .

Sasa kaja Ngemera kila mara yeye yuko kama mlevi .Mambo yake hayaeleweki hata kukaa akaona namna tunavyo ona aibu hap Ubalozini tukienda haangalii.Ukimuona anatembea utadhani ni balozi kweli kaa naye uone .Anatoa amri kama Mhindi na hata hamalizi kazi moja anarukia nyingine .Nina wasi wasi mkubwa na huyu Mzee sijajua kabla ya kuwa Balozi alikuwa na huko utawala wake ulikiuwaje .Kwa kuwa na watu vichwa maji wa aina yake ndiyo maana Ubalozi unakosa hadhi kwa kuwa anaye uongoza hana hadhi .

Membe na kundi lako kama ulikuwa hujui Ujerumani kuna matatizi basi anza upya kuutafuta ukweli utaupata ni aibu kuanzia nje hadi ndani .
 
Basi mie naomba mwenye kumjua huyu mzee atupe data maana kaelezwa na ndugu Mugisha kwamba dikteta anatoa ma amri tu bila ya kujali .Yeye na u boss kwisha kazi ukichanganya na Uhaya .

Kwani Ngemera kabla ya kuwa balozi alikuwa nani ?
 
Huyu Jamaa alikuwa Afrika Mashariki Head wa Finance na administration kama sikosei, sasa kutokana na wa Jumui kwamba hivi vyeo tunapokezana hasa hasa ukitilialia ,maanani kwa Mwapachu ni secretary General ilibidi wamtafutie mahali . Sasa sijui uwezo wake wa kazi unamuwezesha kuwa hapo alipo au nguvu ya ziada ni ndio inamuweka hapo.
 
Ujerumani tuna bahati mbaya sana kupata mabalozo vichwa maji ama hawajali ama hawajui wanacho kifanya .

Mimi sijaona ambae katulia, sehemu nyingine yeyote.

Kuna mtu anaweza kututajia Balozi ambae anajua anachokifanya?
 
balozi anateuliwa na rais kwa hiyo aulizwe yeye. waziri na wizara
wanaweza toa mapendekezo lakini sio lazima yakubaliwe na rais.

kuhusu kuchoka kwa jengo ni vyema hali halisi ya kipesa ya
balozi zetu izingatiwe. je wizara inatuma pesa za ukarabati wa
majengo? kama haitumi ni kwa nini? kwani hata maafisa mara nyingi
inakuwa taabu kuwalipa mishahara yao.

tujiulize je wizara ya ujenzi inahusikaje? kwani nafahamu wanahusika pale ambapo majengo ya ubalozi yanamilikiwa na serikali, jee hali ikoje inapokuwa majengo ya ubalozi yamekuwa yamepangishwa? tusijekuwa tunawalalamikia
mambo ya nje wakati mhusika mkuu ni ujenzi.
 
Kwa muda wa miaka sasa Ubalozi wetu Ujerumani umekuwa kama boma la mmasai kuanzia jengo na hata watumishi wake .Ubalozi huu ni mmoja kati ya Balozi kubwa lakini ukifika utadhani si Ubalozi wenye hadhi .Jumba liko kia ajabu na watanzania hapa Ujerumani tumepiga kelele sana lakini alikuwa hapa Karume yeye ilikuwa safari tu hadi amekuja Ngemera sasa ni balaa mtu huyu .

Ujerumani tuna bahati mbaya sana kupata mabalozo vichwa maji ama hawajali ama hawajui wanacho kifanya .Ninajiuliza kwamba hata wakiwa mawaziri hapo Ubalozini sijui hawaoni hali hali halisi ya jengo lao hilo ama wao huwa wanawa perdiem yao na kuabudiwa na watumishi wa Ubalozi ila mazingira ya watumishi si kazi yao .

Majuzi mkewe Karume alikuwa ana vinjari hapo , waziri wa Utalii na hata Matilda katoka Ujerumani juzi lakini wote wana acha hali ikiwa duni kabisa .

Sasa kaja Ngemera kila mara yeye yuko kama mlevi .Mambo yake hayaeleweki hata kukaa akaona namna tunavyo ona aibu hap Ubalozini tukienda haangalii.Ukimuona anatembea utadhani ni balozi kweli kaa naye uone .Anatoa amri kama Mhindi na hata hamalizi kazi moja anarukia nyingine .Nina wasi wasi mkubwa na huyu Mzee sijajua kabla ya kuwa Balozi alikuwa na huko utawala wake ulikiuwaje .Kwa kuwa na watu vichwa maji wa aina yake ndiyo maana Ubalozi unakosa hadhi kwa kuwa anaye uongoza hana hadhi .

Membe na kundi lako kama ulikuwa hujui Ujerumani kuna matatizi basi anza upya kuutafuta ukweli utaupata ni aibu kuanzia nje hadi ndani .
Ni nini hasa tatizo lililopo hapo ubalozini? nyumba? hudumu? uchafu? Tafadhali be more specific!!!!!
 
Ni nini hasa tatizo lililopo hapo ubalozini? nyumba? hudumu? uchafu? Tafadhali be more specific!!!!!

Kwa kweli labda nimsaidie mtoa hoja .Kuna wakati mwaka huu nimetembelea hapo ubalozini katika shughuli zangu za kawaida nikawa naona watumishi walivyo achilia mbali jengo chakavu na wakubwa wanafika hapo bila kujali nimemsikia mjerumani secretary anateta kwamba balozi ni mtu wa ajabu .anakurupuka na anaweza kukufokea hata mbele za watu .

So nikagundua stress za wale watumishi kumbe si maisha magumu ya kazi pekee kumbe hata boss wao anaonyesha uhaya hadi huko Ulaya .Nadhani wale watu wana kabiliwa na matatizo mazito .Sikuweza kupata wa kusema naye ila kwa sasa nitafanya kazi ya ziada .Mugisha umesema uko Ujerumani ? basi tuwasiliane pembeni nikupe kazi .Lazima tujue kwamba kwanza ubalozi unaendeshwa kama familia ya Ngemera na si Ofisi ya Serikali .

Wengine mnaweza kusema pia ili tupate ukweli maana JF si haba kwa kufuatilia .Mliyoko Majuu umulikeni Ubalozi huo hautoi huduma kwa kuwa watumishi wana ogopa kuchukua majukumu .JK hawa ndiyo washikaji zako ambao umewaleta huku wanavuruga wala hawajengi .
 
Mimi sijaona ambae katulia, sehemu nyingine yeyote.

Kuna mtu anaweza kututajia Balozi ambae anajua anachokifanya?

Mahiga nafikiri anafanya kazi nzuri hapo NYC maana wengi wanamsifia, ingawa sijui kama yeye tusimueite balozi kwa vile ni wa UN au vipi. Ila sielewi kwa nini hadi hivi sasa hawa wa TZ-UN bado wanahama-hama majengo ya kupanga badala ya kununua jengo au kujenga la kwao kama walivyofanya Uganda, Nigeria n.k.

Iddi Amini alikuwa mjinga lakini alikuwa na watu waliomshauri vema akajenga ubalozi enzi zile ilipokuwa rahisi. Hivi sasa nafikiri itabidi labda wahamie Queens, NJ au Harlem kama watataka jengo lao wenyewe.
 
Bora rubega akili ya balozi haina akili anakurupuka tu katikla utendaji wake kwa watendaji wenzake .

Mugishagwe hapo Ujerumani mnaishi vipi kama huyo Murangira ndiyo analeta mambo ya nshomire nk kazini ?JK hawa maswahiba andhani wanajenga Nchi ama wana bomoa ? Membe vipi kuu tupe majibu watumishi wa Ubalozi huu Mugisha anasema wana wakati mgumu kutenda kazi zao na hata jengo ni gofu una habari ama uko bize na mambo ya Zimb baada ya Anjoun ?
 
Mahiga nafikiri anafanya kazi nzuri hapo NYC maana wengi wanamsifia, ingawa sijui kama yeye tusimueite balozi kwa vile ni wa UN au vipi.

Pale United Nations anafanya kazi nzuri, inavyooneka, lakini nina dukuduku zangu na Mahiga anavyo run ubalozi (administratively, that is).
 
Vipi, ana"tawala" kama nyumbani kwake??!!

Hapana, ila ofisi yake haiwi run professionally enough. Na sikupenda alivyo handle zoezi la ubadilishaji passport ambalo Foreign Ministry na Ubalozi wa DC wamemtwika mpaka leo. Nadhani angepewa ubalozi wa kawaida na wenyewe ungezembea.

Ubalozi wa DC uliaandaa siku maalum ya Watanzania kuja kutoa pasi miaka miwili iliyopita. Kazi ikapangwa kufanyika kwenye ukumbi wa kanisa la Mtanzania mmoja, Mchungaji Mama Perusi Muganda, ambae alijitoea, kule Hollis, Queens, New York. Mahiga ambae ameipokea kazi hii (mpaka leo), hakuja, akatuma deputies wake na maofisa kutoka DC.

Ilikuwa ni moja ya siku niliyoshuhudia uozo wa Serikali, ukiritimba – na mazingira yanayofanana na ufisadi – mbaya kuliko zote nilizo pata ona.

Jamaa walikuja hawana fomu za kutosha za application. Wakaenda sijui kutafuta photocopy uswahilini, Hollis, Queens ndani, madongo kuinama, kwa kina LL CooL J na Senti 50 walikozaliwa huko. Na zile fomu huwa hazitolewi copy sasa za nyongeza sijui walizipata wapi. Kazi ikaanza saa saba. Saa nane wakapumzika, wakaenda kula. Saa tisa, mstari ni mrefu kuliko wa foleni ya unga wa yanga wa Reagan.

Moja ya tatu ya raia waliojaa holini ni Wahindi. Sileti urangi na ubaguzi, nivumilie kidogo. Maofisa mabosi mabosi wakaanza kuita Wahindi waje mbele ya mstari. Maofisa wakisha mhudumia Mhindi, Mhindi anasindikizwa nje. Naandika kwa kiapo cha ukweli tupu hapa.

Maofisa wengine wa ngazi za chini wakaanza kuwalalamikia wale vibosile. Kwa sababu wao (maofisa wadogo) ndio walikuwa kama security sasa, wana organize mistari na wanaungurumiwa na watu waliokuwa frustrated. Kikatokea ki-bifu cha nje nje kati ya mabosi na na hawa wengine. By the time kinapoa, Wahindi wote wamesha hudumiwa.

Mambo yakaenda shaghala bagala. Kuna foleni ya kuchukua namba na kuna foleni yenyewe haswa ya kupeleka application itiwe saini na muhuri. Vile vinamba vimeandikwa kwa mkono kwenye vikaratasi vilivyo chanwa chanywa. Navyo eti vikaisha! Lakini wengine waliofika baada yako unaona wanapewa vinamba. Watu wakiuliza kulikoni, unaambiwa alishikiwa namba. Mtu kaja saa nane! Ha ha aaaa! Unbelievable. Kwa hiyo ule mstari wa vinamba ukavunjwa, ikachukua masaa kama mawili kuchana chana kikaratasi vingine. Mstari ukaanza tena upya bila kujali nani alikuwa mbele au nyuma. Mimi nikaondoka saa kumi na moja, na foleni ilikuwa inaendelea.

Sasa hii ilikuwa ni kazi iliyoshirikisha ofisi ya Mahiga. Kwa kujitolea au kwa majukumu. Ningekuwa mimi Mahiga ningekuja ukumbini siku ile. Siku ya Jumamosi, sidhani kama alikuwa na mikutano UN. Na kama alikuwa nayo, ange schedule muda ambao hana mikutano UN.

Na mpaka leo, UN mission ya TZ, New York, bado wanaendelea kutoa pasi. Lakini wanaoenda pale wanalalamika ukiritimba mtupu. Kuna kina dada wako pale huwa wanasambaza a word of mouth "mwambieni Juma passport yake imefika." Tena ukitaka, kama unamjua, unaweza kupewa umpelekee bila Juma kuidhinisha.

Kwa hiyo, ufanisi wa ule ubalozi wa Mahiga nao ungeweza kuwa improved, hauwi run vizuri. Labda wengine we are asking too much. Tunalalamika mno. Tumeharibika kwa kukaa nje. Tumezoe mno professionalism kwenye maofisi. Lakini mimi sijuti hata kidogo kuwa spoiled kwa namna hii. Matatizo makubwa ya nchi yanaanzia kwenye madogo madogo huku chini chini. Ndio haya ya kuyarekebisha.

Niliyoshuhudia hapo juu sikuwepo peke yangu ukumbini pale. Walioona vinginevyo wanikamate uongo. If you saw this debacle that day you know what I'm talking about.

Wale maofisa waliokuwa wanaita Wahindi mbele ya mstari ni wafanyakazi wa foreign affairs. Walitokea ile idara inayotoa maofisa wengi wa ubalozi. Ni kinyume cha sheria za nchi kuanika majina ya maofisa wa hiyo idara, kama unawajua. Vinginevyo ningewataja majina hapa. Na wanitafute na wenzao waniue. Kuna wengine niliwakoromea na walinimaindi. Lakini kuna mambo ya nchi ambayo hayawezi kubadilika bila watu kukubali kufa.

Yani inauma ile kinoma yani!
 
...Niliyoshuhudia hapo juu sikuwepo peke yangu ukumbini pale. Walioona vinginevyo wanikamate uongo. If you saw this debacle that day you know what I'm talking about.

Wale maofisa waliokuwa wanaita Wahindi mbele ya mstari ni wafanyakazi wa foreign affairs. Walitokea ile idara inayotoa maofisa wengi wa ubalozi. Ni kinyume cha sheria za nchi kuanika majina ya maofisa wa hiyo idara, kama unawajua. Vinginevyo ningewataja majina hapa. Na wanitafute na wenzao waniue. Kuna wengine niliwakoromea na walinimaindi. Lakini kuna mambo ya nchi ambayo hayawezi kubadilika bila watu kukubali kufa.

Yani inauma ile kinoma yani!

mkuu poleni kwa yaliyowakuta.
hao maofisa nadhani ni wale ambao wanapita tu foreign lakini
wanatokea ile ofisi nyingine. kama kweli ni hao basi kaaazi kweli
kweli!
 
...hao maofisa nadhani ni wale ambao wanapita tu foreign lakini wanatokea ile ofisi nyingine. kama kweli ni hao basi kaaazi kweli
kweli!

Ni kweli wanapita. Hawapo tena DC.

Baadhi nawajua kwa 100%.
 
Mkuu mimi nilikuwepo huko NYC wakati zoezi hili la kubadilisha pass linaanza, nakumbuka waliambiwa waende kanisani, nikaenda kujionea hakukuwa na tatizo lolote, waliowahi ndio waliopewa kwanza, aliyesimamia alikuwa ofisa toka bongo, ambaye hakuwa na mchezo,

Balozi wa Tanzania UN, ambaye at the time alikuwa Rais wa Baraza la Usalama La Umoja Wa Mataifa, yaani dunia nzima inamsubiri kwa maamuzi makubwa ya kiusalama, mpaka ailibdi serikali yetu imtafutie apartment karibu na ofisi za UN, ala aweze kuwepo pale karibu masaa yote 24 kama kazi hiyo ya dunai inavyodai, leo akaache kazi hizo aje kusimamia ubadilishwaji wa passport? Are you serious?

Mijitu mi-Tanzania inakwenda ofisini na kudai haijua kiswahili na kuanza kuwasumbua maofisa pale wakati hata hiyo English haijui, wakilulizwa umeishi muda gani kule eti miaka mitatu tu yamesahau kiswahili? Yakiambiwa lete affidavit au cheti cha kuzaliwa yanauliza what is that? Halafu unasema makosa ya maofisa wa ubalozi?

Ebo! zoezi lilipofanyika Queens, ilikuwa ni mara ya pili kwa sababu kila walipotakiwa kwenda mahali, majitu huishia kwenda saa mbili za usiku kwa sababu ya kuwa kazini, sasa maofisa wake siku nzima wasiende UN kwenye kutuwakilisha kwa sababu ya kazi za wananchi? Wahindi walifika kwenye foleni mapema na hawakuwa na matatizo, wengine walikuwepo kwenye kituo kingine the day before au juzi yake fomu zikaisha wakaambiwa waende tena siku nyingine, sasa ni lazima watangulie kwanza maana walikuwepo kabla,

Huko ofisini ubalozini hakuna ofisa anayekaa tu kusubiri kumtengenezea mtu passport hiyo ni kazi ya ubalozi DC, kule NY wanasaidia tu wawakilishi wetu USA ni DC, ndio wanaotakiwa kuhusika na hili zoezi 100%, sio NY ambapo kuna shughuli za kimataifa 24 hours a day, viongozi na maofisa wa serikali wanashuka Airport JFK 24 hours kila siku, wanahitaji kupokelewa kutayarishiwa mambo ya mikutano, I mean mtu unapaswa kushukur kama umeweza kupewa passport pale,

Mkuu unless una matatizo mengine, lakini kwenye hili huna ukweli kwa sababu hukuwa peke yako, kama ni jnego liko njiani kununuliwa tena kule mjini kabisaa karibu na 44Th Street, ambako sio mbali na UN, mkuu mnyonge mnyongeni, kama ile ofisi ilikuwa mbovu ilikuwa ni wakati wa balozi aliyeondoka kbala ya Mahiga lakini sio sasa, magazeti mengi sana tumeyona kuhusu ofisi ya sasa na kazi nzito waliyoifanya kutuwakilisha Tanzania kwenye Security Council, ndio imezaa mpaka Mama Migiro kupewa kazi ya kusaidia kuongoza dunia!

Msema Ukweli Siku Zote huwa ni Mpenzi wa Mungu, mkuu sema ukweli acha dhambi za bure bila sababu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom