Mimi naishi huko, kuna taitizo kubwa la kiusalama, tena kuna wizi hata ule wa kutumia silaha achilia mbali vibaka na wakabaji!
Moja ya chanzo cha tatizo hili ni ukosefu wa vituo vidogo vya polisi maeneo hayo zaidi ya cha Kigambo hapa feri, pili hakuna doria ya maana usiku kiasi kwamba ikifika usiku vibaka hushangilia!
Na zaidi polisi wanahusika kwa matukio ya kupora kwa kutumia silaha, mfano polisi wanatoa taarifa kwa majambazi kuwa mtu fulani anamiliki silaha, hivyo majambazi wakifika chakwanza kabisa wanahitaji silaha kisha shughuli nyingine zinaendelea!
Serikali iimarishe uadilifu wa polisi wetu na wananchi tuanzishe ulinzi shirikishi (sungusungu), viwekwe vituo vya polisi kibada, vijibweni,kimbiji na cha mji mwema kiboreshwe!