MLA PANYA SWANGA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 5,181
- 5,429
Watanzania wengi tumekuwa tukililia katiba mpya ni kweli kwa sehemu tuko sahihi. Watanzania tumekuwa tunalilia kuwa na viwanda vingi ili kuinua uchumi yaani badala ya kuuza pamba tuuze nguo. Mh. Rais amesimamama kidete kuhakikisha viwanda vinakuwepo.
Nionavyo mimi, huko nyuma vyote vinavyotafutwa leo vilishawahi kuwepo na serikali hii hii ya chama hiki hiki na katiba hiihii.Mwanaume ama mwanamke anayeoa ama kuolewa zaidi ya mara tatu na kuendelea lakini akawa anaachika ama kutodumu na mme ama mke huyu hasitahili kuoa tena Kama hajatambua tatizo la kutodumu na mke ama mkewe ktk ndoa na kupanda kinga yake.
Huwezi kuanza kuwafufua marehemu kabla hujapata kinga ya ugonjwa uliomuua marehemu. Viwanda na ndege zinazozununuliwa leo ziliwahi kuwepo huko nyuma lakini kwa kuwa katiba yetu haina kinga (immunity) kila kiongozi anayeingia anaamua kufanya ajuavyo. Tusishangae rais akafanya mazuri mengi lakini siku akiondoka tu ikulu atapewa taarifa kuwa wale marehemu uliowafufua wamenyongwa na baba mrithi wako naye hatakuwa na nguvu tena juu ya hilo. Tanzania kila mtu anajiona anajua sana.
Tunahitaji kumpata MTU atakayekuwa tayari kuandaa katiba ya wananchi katiba ambayo itakuwa na kinga (immunity) ili watakaokuja nyuma wasiharibu misingi ya maendeleo watakayoikuta. Katiba ambayo haitaegemea kwa chama chochote wala kundi fulani wala kanda fulani wala kabila fulani wala dini hii ama ile.
Tunahitaji MTU atakayekubali kuwa masikini kwa ajili ya taifa hili. MTU huyo ndiye ataileta KATIBA yenye kinga. Katiba hiyo ndiyo itakayobadilisha taifa hili. Ili kudhihirisha kuwa katiba ya nchi hii haina kinga MTU mmoja tu aliamua uchaguzi urudiwe zanzibar japo katiba ilikuwa na mwongozo mzuri juu ya hilo ila alifanikiwa kwa kuwa katiba haina kinga.
Nchini marekani Rais mpya alitoa tamko la kuzuia baadhi ya watu aliowahofia yeye wasiingie marekani lakini katiba ikambana na akatengua kauli yake kwa kuwa katiba yao ina kinga. Kama hatujui kilichoua viwanda vyetu tusihangaike kujenga vipya maana mwisho wa siku vitataifishwa na kufilisiwa na wachache kwa maslahi yao.
Kama rais una nia njema na taifa hili kuwa MTU uandae katiba ya watu siyo ya chama nayo iwe na kinga ya kudumu itakayozuia baba mrithi wako ikulu asiuze wala kubinafsisha hizo ndege na viwanda ulivyoahidi kujenga na kufufua. Nje ya hapo hata wewe ukiondoka ikulu ujue pilato mpya akifika atawatengua wateule wako wote, atavunja misingi yako yote ya uchumi naye atakuwa na santuri jingine.
Kuwa na viwanda ama uchumi mzuri ni hatua moja na kudumu navyo ni hatua nyingine. Hatua hiyo inategemea kinga ya katiba. Hakuna haja ya kuwa na mali kama huwezi kudumu nayo na ukawa na kinga ya Mali yako isiharibiwe. Yanayokiukwa nchini kwenda kinyume na katiba ni mengi tena yanafanywa na viongozi wetu kwa kiburi tu kuwa katiba haina kinga. Katiba haina meno inadharaulika. Huenda rais tuliyenaye akawa MTU akaamua kufanya taifa hili lipate katiba yenye kinga ila kama hawezi hayo asiangaike maana atakuwa anakusanya mali itakayokuja kugawanwa na kundi lake, chama chake, na wanamtandao wake.
Kinga ni bora kuliko tiba. Nakubali kukosolewa lakini kwa hoja.