Kichomi ni nini? Husababishwa na nini? Na tiba yake ni ipi?

kilumbi

Member
Oct 9, 2012
24
4
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisumbuliwa na kichomi na nimeshatumia dawa nyingi sana za hospitali lakini bado tatizo liko pale pale. Naomba mnisaidie dawa itakayonisaidia kuondokana na tatizo hili.
 
TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO

VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee

au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.

Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.

    • Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
    • Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?
    • Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
    • Umeinama au umelala
    • Ukishakula chakula
Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa

wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimengenyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.

Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.

Hasa kama hunywi maji.

Kunywa sana Maji ya Uvuguvugu yatakusaidia kuondowa tatizo la kichumi.
 
shosti wangu kanitumia message asubuhi hii kwamba anasumbuliwa na lichomi tangu jana hajalala nimemuuliza hivi kinasabaishwa na nn akaniambia eti vitu vya baridi, naomba wataalamu mtiririke hapa kutusaidia wengi
 
Hivi ndugu, Kichomi husababishwa na nini kitaalamu? Na huduma ya kwanza nini? Na tiba yake kitaalam nini?
 
sababu ziko nyingi sana mfano;
baridi kali
matatizo ya moyo
matatizo ta uzazi
uvimbe kwenye ovari

Hakuna tiba ya moja kwa moja mpaka angalau chanzo kijulikane. Huduma ya kwanza ni kumlaza mgonjwa, kumkanda na maji ya vuguvugu.. kumfunika asipigwe na baridi.
 
pneumonia ndio jina la kitaalamu angalia usiibiwe na waganga wa kienyeji
Mkuu inaonyesha wewe unaropoka ovyo bila ya kujuwa unachokisema. Mkuu.@jajis alichosema yeye anaumwa matatizo ya kichomi wewe unasema pneumonia jina la kitaalamu kisha unawapiga vita Waganga wa kienyeji unasema eti wasimuibie hakuna mganga wa kienyeji atakaye muibia kwanza wewe unachosema tofauti na huyu Mkuu jajis anacholalamika unajuwa hiyo (Pneumonia) ni ugonjwa gani? au unakisia tu?au unapenda na wewe kutoa mchango wako wa pumba? Mshauri au mpe dawa akatumie basi. Kamahuna kitu cha kuchangia bora si unyamaze kuliko kuwatukana waganga wa kienyeji kuwa eti watamuibia? Tumemshauri aende Hospitali kwanza kupimwa huenda ana maradhi ya moyo yeye anahisi kuwa kichomi wewe unamuambia eti ana Maradhi ya (pneumonia)? umejuaje
kama kitu hujuwi ngojea wanaojuwa watakuja kumjibu usiropoke ovyo kuwalaumu watu pasipo kuwa na wewe elimu yoyote ile bora kunyamaza au mpe pole inatosha kuliko kusema maneno ya pumba.
 
MziziMkavu acharuka!!!

Mkuu inaonyesha wewe unaropoka ovyo bila ya kujuwa unachokisema. Mkuu.@jajis alichosema yeye anaumwa matatizo ya kichomi wewe unasema pneumonia jina la kitaalamu kisha unawapiga vita Waganga wakienyeji unasema eti wasimuibie hakuna mganga wa kienyeji atakaye muibia kwanza wewe unachosema tofauti na huyu Mkuu jajis anacholalamika unajuwa hiyo (pneumonia) ni ugonjwa gani? au unakisia tu?au unapenda na wewe kutoa mchango wako wa pumba? Mshauri au mpe dawa akatumie basi. Kamahuna kitu cha kuchangia bora si unyamaze kuliko kuwatukana waganga wa kienyeji kuwa eti watamuibia? Tumemshauri aende Hospitali kwanza kupimwa huenda ana maradhi ya moyo yeye anahisi kuwa kichomi wewe unamuambia eti ana Maradhi ya (pneumonia)? umejuaje
kama kitu hujuwi ngojea wanaojuwa watakuja kumjibu usiropoke ovyo kuwalaumu watu pasipo kuwa na wewe elimu yoyote ile bora kunyamaza au mpe pole inatosha kuliko kusema maneno ya pumba.
 
MziziMkavu acharuka!!!
Mkuu mimi sijacharuka ninamuambia Mkuu.@Freedom tommorrow Maneno ya ukweli kama hana kitu cha kuandika bora asiandike asome Thread na apite kama gari lililojaa mzigo. La kama anacho kitu cha kuandika aandike asiandike maneno ya pumba hapa jukwaani. Tunapoteza muda wetu kuwasaidia kuwapa ushauri watu wenye kutaka ushauri yeye huyu Mkuu Freedom tommorrow anaropoka maneno kama mtu aliye lewa pombe? anasema eti wasimuibie waganga? Kuna mganga gani aliye mwambia huyu aliyeweka Thread kuwa amerogwa? watu wengine vichwa vyao vizito kuelewa na kusoma pia kama vile hawajuwi kile wanacho kisema.
 
Nilipatwa na tatizo kama hili, ila dr. aliniambia niache kula pilipili, vitu vyenye acid mf ndimu, limao, pombe kali, maharage. Pia nile chakula kwa wakati. Nimefuata masharti yote naona vimeacha.
Vilikuwa vinakutokea sehem gan vichomi mkuu
 
TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO

VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee

au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.

Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.

    • Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
    • Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?

    • Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
    • Umeinama au umelala
    • Ukishakula chakula
Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa

wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimengenyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.

Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.

Hasa kama hunywi maji.

Kunywa sana Maji ya Uvuguvugu yatakusaidia kuondowa tatizo la kichumi.
Ahsante mkuu
 
Kunywa maji mafundo saba tena kwa kuhesabu au chukua kipande cha uzi kipake mate halafu bandika katika paji la uso kama sigda hapo itakuwa shwari

Hii ndio tiba ninayotumia mpaka leo tokea nikiwa mdogo nilifundishwa na bibi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom