Tatizo la umiliki ardhi Tanzania

Tatizo la umiliki ardhi Tanzania

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,692
Reaction score
37,575
March 13, 2019
Dar -es-Salaam, Tanzania

Kumekuwepo na tatizo la nyumba nyingi katika vitongoji vya miji ya Tanzania kubomolewa kutokana na utata wa umiliki ardhi.

Mfano mwezi March 2019, Wananchi wa Kitongoji cha Yangeyange Kata ya Msongola Ilala jijini Dar es salaam wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu baada ya nyumba zao zaidi ya 32 kubomolewa na kampuni moja ya udalali iitwayo, Lumina.

Zoezi la kubomoa nyumba hizo ni baada ya mmiliki Scolastica kushinda kesi ya uvamizi katika viwanja hivyo . Baadaye Dalali / broker Lumila wa mahakama kupewa korti oda kuhakikisha umiliki unarudi mikononi mwa mmiliki halali na hivyo nyumba 32 za wavamivi kubomolewa ktk eneo.

Wana JamiiForums tuwe makini wakati tukitafuta maeneo ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba. Wenye uzoefu mtupie maoni taratibu gani za kufuata katika manunuzi ya viwanja hasa katika vitongoji vya mijini Tanzania ili tusikumbane na bomoa bomoa.


Source: Bongo5
 
Hakikisha unafanya through searching katika ofisi za ardhi na mipango miji.
Kwa usahihi zaidi tafuta mtaalam wa sheria akuongoze katika huo mchakato.

Wanasheria tujuzeni tafadhali. Je kile kipengele cha adverse possesion hapa hakihusiki?
 
Back
Top Bottom