DOKEZO Tatizo la umeme wilaya ya Chunya

DOKEZO Tatizo la umeme wilaya ya Chunya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

ChunyaBoi

New Member
Joined
Jun 19, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Kuna tatizo kubwa la umeme wilaya ya chunya umeme ni mdogo sana. Hili tatizo limekaa muda sasa zaidi ya miezi miwili.

Mahitaji ya umeme kwenye uendeshaji wa shughuli za kila siku za madini ni makubwa mno. Kukatika kwa umeme eneo hili kunaleta hasara kubwa sana kwa watumiaji.
 
Habari, Ndugu Mteja.

Asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu. Kutokana na changamoto ya muda iliyojitokeza kwenye akaunti yetu, ujumbe wako ulitufikia kwa kuchelewa. Hata hivyo, kwa sasa huduma imerejea katika hali ya kawaida.

Tafadhali, tunaomba kutufahamisha kama changamoto uliyoiwasilisha bado inaendelea au tayari imetatuliwa. Endapo bado unaikabili, tafadhali tujulishe ili tuweze kuifuatilia na kuhakikisha inapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Asante sana kwa uvumilivu na ushirikiano wako. Karibu sana. ^CM
 
0782510235 Meneja Tanesco Chunya!
Muulizeni atawajibu, hali halisi ilivyo,huko Chunya!

Hali ni mbaya ,Mbaya ,mbaya kabisa.
Low voltage mchana hakuna umeme wa kutosha, usiku pia na siku za Alhamis na Jumamosi hakunaga umeme kabisa kwa kila wiki.

Hili ni janga la Taifa
 
Asante, ndugu mteja.

Kufuatia taarifa uliyotupatia, tumebaini kuwa changamoto hiyo bado ipo na tumeipokea kwa ajili ya ufuatiliaji na ofisi ya mkoa husika. Mara baada ya kupata mrejesho rasmi, tutatoa taarifa na mwongozo stahiki kwa wateja wetu wote wa Chunya wanaokabiliwa na changamoto hii.

Tunaomba uvumilivu wako wakati tunapoendelea kufanya ufuatiliaji suala hili ili kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi unaostahili.

Asanteni sana! ^CM
 
Kuna tatizo kubwa la umeme wilaya ya chunya umeme ni mdogo sana. Hili tatizo limekaa muda sasa zaidi ya miezi miwili.

Mahitaji ya umeme kwenye uendeshaji wa shughuli za kila siku za madini ni makubwa mno. Kukatika kwa umeme eneo hili kunaleta hasara kubwa sana kwa watumiaji.
Habari, Ndugu Mteja.

Asante sana kwa kutupa muda wa kufuatilia suala hili.

Baada ya kufanya ufuatiliaji kuhusu changamoto ya umeme mdogo (Low Voltage) katika Wilaya ya Chunya, tunapenda kukufahamisha kuwa tayari hatua za kutatua changamoto hiyo zinaendelea kupitia ratiba ya matengenezo na maboresho ya miundombinu ya umeme yanayotekelezwa kwa awamu.

Kwa mfano, kesho kutakuwa na usitishaji wa huduma katika baadhi ya maeneo ili kutoa fursa kwa wataalamu wetu kuendelea na kazi za maboresho zinazolenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Kwa urahisi wa kufuatilia, tumeambatanisha tangazo lenye ratiba ya matengenezo, linaloonyesha maeneo yatakayoathirika pamoja na vipindi vya usitishaji wa huduma. Matengenezo haya yanalenga kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto ya umeme mdogo katika eneo hilo.

Tunaomba uvumilivu na ushirikiano wenu wakati maboresho haya yakiendelea. Asante sana. ^GK
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2026-07-29 at 10.01.42.jpeg
    WhatsApp Image 2026-07-29 at 10.01.42.jpeg
    46.7 KB · Views: 7
Tanesco uwajibikaji wilaya ya Chunya ni hafifu.. Umeme umekua ni changamoto hasa kwa biashara hii ya madini.. Umeme umekua zaidi ya kero tunaingia gharama kubwa kutumia mafuta na mnaelewa hali ya bei ya mafuta ilivo.. Kwa kweli mnatia hasara na mnakwaza tunakaa siku nzima umeme hakuna na ukirudi ni masaaa kadhaa umekatika tena na hii inaenda wiki nzima.. This is too much
 
Ratiba inaonyesha diku za jumamosi hakuna umeme sawa!
Mbona leo Jumapili, Matundasi,Matondo na Itumbi Watanzania wako gizani tangu asubuhi hadi muda huu?????
 
Habari, ndugu wateja na asante kwa kuwasilisha mrejesho huu. Mategenezo bado yanaendelea, ila ngoja kufuatilie juu ya maeneo tajwa kwa msaada zaidi.

Asante. ^GK
 
Tanesco uwajibikaji wilaya ya Chunya ni hafifu.. Umeme umekua ni changamoto hasa kwa biashara hii ya madini.. Umeme umekua zaidi ya kero tunaingia gharama kubwa kutumia mafuta na mnaelewa hali ya bei ya mafuta ilivo.. Kwa kweli mnatia hasara na mnakwaza tunakaa siku nzima umeme hakuna na ukirudi ni masaaa kadhaa umekatika tena na hii inaenda wiki nzima.. This is too much
Habari, Ndugu Mteja.

Kwanza, tunakuomba radhi kwa changamoto hii na tunakushukuru kwa kutuvumilia ili tuweze kufuatilia na kuchukua hatua stahiki.

Tafadhali fahamu kuwa changamoto hii inafahamika na bado inaendelea kufanyiwa kazi. Pia, tunaambatanisha barua kutoka ofisi yetu ya Chunya inayoeleza kuhusu jitihada zinazoendelea katika utekelezaji wa matengenezo hayo.

Barua hiyo pia inaonesha tarehe ambazo huduma inaweza kusitishwa kwa ajili ya matengenezo. Taarifa za matengenezo yaliyopangwa pia hutolewa kupitia makundi yetu ya WhatsApp.

Iwapo ungependa kujiunga na kundi la WhatsApp la eneo lako ili kupata taarifa hizi kwa wakati, tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp pamoja na Wilaya unayoishi kupitia Inbox, nasi tutakusaidia kuunganishwa.

Asante! ^CM
 
Attachments

  • shared image.jpg
    shared image.jpg
    83.2 KB · Views: 1
Habari, Wateja Wetu.

Tunapenda kutoa mrejesho kuhusu changamoto ya umeme kuwa mdogo (low voltage) inayowakabili baadhi ya wateja wetu katika Wilaya ya Chunya na wilaya ya Mkwajuni.

Tafadhali fahamu kuwa Serikali kupitia TANESCO inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto hii. Leo Septemba 11, 2026, mkataba wa ujenzi wa miundombinu muhimu ya umeme umesainiwa Wilayani Mkwajuni, hatua ambayo inalenga kuongeza upatikanaji wa umeme kwenye wilaya hizo.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 (220kV) kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza, Wilaya ya Mkwajuni, yenye urefu wa takribani kilomita 122, kwa thamani ya TSh bilioni 109. Aidha, mradi unahusisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme chenye uwezo wa 100MVA, sawa na takribani MW 80.

Mradi huu unatarajiwa kuleta kutatua changamoto yote ya upatikanaji wa umeme kwa wateja wote.

Hivyo, tunaomba muendelee kuwa na uvumilivu wakati utekelezaji wake unaendelea.

Tunawashukuru kwa ushirikiano na uvumilivu wenu.

Asante! ^HN
 
Asante kwa taarifa nzuri!
Ninaomba kuuliza, kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza, Wilaya ya Mkwajuni, yenye urefu wa takribani kilomita 122, hii line itapitia chunya mjini, Matundasi hadi Makongorosi? Ua itapitia wapi?
 
Ndiyo, njia ya umeme ya mradi huu itapita katika maeneo uliyoyataja. Mradi unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha takribani miezi 18.

Tunatarajia kuwa kukamilika kwa mradi huu kutaleta unafuu mkubwa katika upatikanaji na ubora wa huduma ya umeme katika maeneo hayo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha huduma kwa wateja wetu.

Tunaomba uendelee kuwa na uvumilivu na uelewa wakati utekelezaji wa mradi ukiendelea.

Asante. ^HN
 
Back
Top Bottom