tatizo la umeme dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tatizo la umeme dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Darling, Mar 21, 2009.

 1. D

  Darling Member

  #1
  Mar 21, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi niko msasani; je huu ueme kukatikakatika ni kwetu tu au wengine pia?
   
 2. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wala si kwenu tu watu msasani, nafikiri ni Dar nzima. Kwa mfano kwetu ishajulikana kuwa siku za j'mosi na j'pili umeme unazimwa, na kweli leo umezimwa mapema tu. Ukizingatia kuwa kupatikana maji maeneo mengi ya Dar kunategemea umeme, basi imekuwa shida. Usipowahi kabla ya saa 3 asubuhi unaweza kukosa na maji pia. Kazi kweli kweli!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,670
  Trophy Points: 280
  Poleni sana. Hakuna kitu ninachochukia kama kukosa maji na umeme kunakosababishwa na uzembe wa vyombo husika na serikali. Kukosekana hivi vitu kunakosesha raha sana.
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Mar 21, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  uko nchachani uzunguni?hapa nchachani uswazi wamekatakata mara 4!
   
 5. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  usipime si kwenu tu kwetu ni kila siku na kila wakati sisi tumesha zoea hapa ustawi tunashindwa hata kusoma kagenerator kakizimwa basi na inavyo onekana bosi mkuu wa tanesco naona madaraka kuliko hata waziri alisema tutakaa gizani na ndo analolifanya,manake ye waziri alisema hatuwezi kuwa gizani,lkn tupo gizani sasa nani boss hapo?
   
 6. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Mike 1234, sio kuwa nani boss kuliko mwenziwe baina ya Waziri na boss wa Tanesco.

  Tanesco ndio wanaojuwa hali halisi ya umeme walionao. Sasa kama Bunge limepiga stop, basi kwanza tupewe taarifa ya huko kukosekana kwa umeme ili tuweze kutathmini na kujuwa sababu ya kutokuwapo kwa umeme.

  Hayo ni majukumu mazito na nyeti kwa wakuu. Kiurahisi tunaweza kulaumu Tanesco lakini sababu inawezekana ikawa sio wao bali ni Bunge kuingilia kazi za kiutendaji.
   
Loading...