Tatizo la ukavu wa uke... Haya nyie Wadada mnaosema naumia wakati wa tendo njoo hapa

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
394
456
Bpharm: Chriss Johny

Tatizo la kuwa na ukavu ukeni hutokea wakati tishu za uke hukosa ute wa kutosha na uke kutokua na afya thabiti.
Kwa kawaida, kuta za uke hukaa zimehifadhiwa na safu nyembamba ya ute maji.

πŸ’Ž
Dalili kuu ni kama vile kukosa hamu ya kuendelea KUSHIRIKI tendo, maumivu makali ukeni, michubuko, na wakati mwingine hupelekea miwasho baada ya tendo

πŸ“š
Hormoni estrojeni husaidia kudumisha uwepo wa ute maji na kuhakikisha uke wako kuwa na afya.
Kupungua kwa viwango vya estrojeni hupunguza kiasi cha unyevu katika uke. Na kupungua kwa homoni kunaweza kutokea wakati wowote kutokana na sababu mbalimbali. Inaweza kuchukuliwa kama masihara. Lakini ukosefu wa unyevu wa ukeni unaweza kuwa na athari kubwa kwenye maisha yako katika tendo la ndoa.

πŸ“š
Kwa bahati nzuri, matibabu kadhaa hupatikana ili kupunguza ukavu wa uke. Moja kama tatizo ni la muda mrefu ni vema kuonana na daktari aweze kukupa matibabu au kukushauri kuhusu matumizi ya estrojeni za uke au matumizi ya vilainishi uke.

πŸ“€
Je, Matibabu mbadala ya ukavu ukeni ni kama yapi?

1. Chembe katika maharagwe ya soya huwa na athari sawa na za estrojeni. Ikiwa unatumia kwa wingi soya kwenye lishe yako, unaweza kupata unafuu wa ukavu wa uke.

2. Ulaji wa mihogo ni kiungo kingine cha ziada ambacho kimeonyesha kusaidia kupunguza ukavu lakini ushahidi kutoka kwa utafiti bado haujafanyika.

3. Pia ulaji wa maparachichi, apples, flaxseeds, na kunywa maji mara kwa mara. Ni njia mbadala yenye afya kwa wale ambao hawapendi soya.

4. Matumizi ya gel za kulainisha na kuongeza uteute yanaweza tumika pia, utayapata pharmacy. Ni mazuri zaidi kuliko matumizi ya mafuta mengine, maana hivo vilainishi vinavyouzwa pharmacy mfano ( KY) huweza kuendana na PH ya uke na vimetengenezwa kwa lengo hilo husika

πŸ“š
Ukavu wa uke na maumivu yanaweza kumfanya mwanamke asipende tendo la ndoa, japokua tendo la ndoa pia ndio dawa ya asili ya ukavu wa uke. Wakati mwanamke anaandaliwa kwa tendo la ndoa, mzunguko wa damu kwa tishu zake za uke huongezeka, ambayo inasisimua uzalishaji wa unyevu, na hivyo hupambana na ukavu.
UMEJIFUNZA NINI LEO ?

.
πŸ™
AHSANTENI MWISHO
sio mimi ni huyu hapa πŸ‘‡ kasema
Bpharm: Chriss Johny
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom