Tatizo la TV kujibadili rangi naomba msaada

Tatizo la TV kujibadili rangi naomba msaada

KAMJUS

Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
83
Reaction score
16
Wanajamvi tv yangu ya hitach kichogo inazingua rangi mara inakuwa normal mda mwingine inajibadili kuwa ya urujuani au kwa lugha nyingine zambarau picha hazionekani vizuri. Sijui tatzo ni nini wataalamu nipe maujuzi
 
Mmmh wacha waje wajuvi wa hayo mambo, ila umeniacha na hiyo urujuani mkuu, ndo nini?
 
yaani sio rangi za spika maana za spika zinakuwa pembeni. yaani inachange rangi kama vile umeichange kuwa black& white. lakn ynyw inajibadili kuwa ya zambarau
 
Hapana marefu yasiyo na ncha. Imeshafikia mwisho wa muda wake wa matumizi. Ni mwisho wa uhai wa luninga yako. Badilisha kanunue mpya ya kisasa achana na luninga za chogo.
 
Ni mtundu wa vitu hivyo nikuelekeze upo mkoa gani msaada zaidi 0713666725
 
yaani sio rangi za spika maana za spika zinakuwa pembeni. yaani inachange rangi kama vile umeichange kuwa black& white. lakn ynyw inajibadili kuwa ya zambarau

Mkuu ebu weka picha tuione.
 
Attachments

  • IMG10730.jpg
    IMG10730.jpg
    9.1 KB · Views: 161
peleka kwa fundi tv yeyote mwambie arudishie risasi(soldering) kwenye transistor zilizo kwenye CRT,kama ni fundi ataelewa kirahisi
 
mimi nina ya kwangu huwa kuna wakati inatoa picha nzuri ila mda mwingi picha inakuwa na unjano yaani sehemu kama ina maandishi mekundu yanaonekana kama meusi
 
Hiyo ni loose connection 2 kweny CRT,,,fany soldrng kweny hiyo circuit ya CRT kama huwez mpelekee fundi akufanyie espcially kweny hzo resistor & transistor.
 
Hapana marefu yasiyo na ncha. Imeshafikia mwisho wa muda wake wa matumizi. Ni mwisho wa uhai wa luninga yako. Badilisha kanunue mpya ya kisasa achana na luninga za chogo.

Haijachoka ya kwangu miaka mitano tangu nimeirekebisha na haijasumbua tena. Kuna switch iko kwa ndani imeandikwa colour hiyo ndio inayozungushwa inakaa majali pake.Fundi atakudanganya kuchomeachomea uongo kisha anapaswitch unadhani ni kule kuchomea kumbe wapi. Kama wewe mtundu fungua kama huwezi fundi asijifanye kuchomea solda.
 
Siwezi kataa kwa sababu siwezi kujua. Mimi kwa upande wangu sijawahi kupeleka luninga kwa fundi itengenezwe.
 
Haijachoka ya kwangu miaka mitano tangu nimeirekebisha na haijasumbua tena. Kuna switch iko kwa ndani imeandikwa colour hiyo ndio inayozungushwa inakaa majali pake.Fundi atakudanganya kuchomeachomea uongo kisha anapaswitch unadhani ni kule kuchomea kumbe wapi. Kama wewe mtundu fungua kama huwezi fundi asijifanye kuchomea solda.

Ushauri mzuri. Pia aangalie capacitor ambazo zipo karibu na output ya transformer (rectifier) kama zipo lose or zimevimba. Hizo pia huwa zinaweza kuwa sababu japo kazi yake ni kuondoa ripples ili dc supply iwe constant. Sometimes zikiwa zimevimba ama loose huwa zinasababisha hilo tatizo. Nimewahi kutana na hilo tatizo.
 
Kitu kama hicho kimeshawahi kutokea kwenye Tv yetu na chanzo chake kilikuwa ni speaker zilizokuwa karibu na tv.
Hivyo kama walivyoshauri wadau wengine, tafuta fundi ambaye sio mzushi akurekebishie kisha ondoa spika karibu na tv yako.
 
Back
Top Bottom