Tatizo la sliding Hiatal Hernia with GERD

losiraa

Member
Nov 17, 2018
51
27
Habari za jioni ndugu wadau,

Nahitaji msaada na ushauri wenu kuhusiana na tatizo langu kama nilivyoandika. Nimekuwa nikisumbuliwa na dalili kama za vidonda kwa muda mrefu, lakini leo nilipopimwa daktari akanifahamisha kuwa nasumbuliwa na tatizo la sliding hiatal Hernia with GED,

Jambo lililoniumiza ni namna daktari yule alivyonieleza kuwa itanibidi kutumia dawa Siku zote za maisha yangu na maumivu makali ninayohisi.

Wadau naomba kuuliza
1. Je, hiyo ni kweli itanipada kutumia dawa Siku zote za maisha yangu?
2. Je ni kweli ugonjwa huu hauponi?

Naomba ushauri wenu
 
Kulitakiwa kuwa na majadiliano ya kufahamishana vyema, ni kwa nini amesema hivyo.

Hii inatokana na kwamba yeye ndo ameona aina na kiasi cha sliding hernia yenyewe na stage yake.

Sababu, sliding hernia ni moja ya kisababishi cha GERD. Ingawa huwa ni mhimu pia kufanya mabadiliko kwenye mfumo wako wa maisha ili kukusaidia kuishi na tatizo husika, nategemea mtakuwa mmejadili hayo pia.

Kulingana na tatizo kuwa na mtizamo wa kudumu na uchaguzi wa aina ya tiba hivyo basi tiba itatakiwa kuwa ni ya kudumu pia.

20211006_210351.png
20211006_210257.png


20211006_210105.png


20211006_205944.png


20211006_205905.png


20211006_205838.png
 
Nashukuru sana kwa ushauri ndugu yangu,
Daktari aliyefanya kipimo alisema stage ya hiyo hernia sio kubwa ni ya kutibu na dawa haihitaji operation.

GERD ndio ipo hatua ya pili japo pia alisema nitumie dawa.

Najiuliza kama nikibadili life styele na kutumia dawa Hali ikatulia bado kutakuwa na ulazima wa Kuendelea na dawa?
 
Nashukuru sana kwa ushauri ndugu yangu,
Daktari aliyefanya kipimo alisema stage ya hiyo hernia sio kubwa ni ya kutibu na dawa haihitaji operation,
GERD ndio ipo hatua ya pili japo pia alisema nitumie dawa
Najiuliza kama nikibadili life styele na kutumia dawa Hali ikatulia bado kutakuwa na ulazima wa Kuendelea na dawa?

Ukibadili mfumo wa maisha ukaweza ku-control hernia, likely utaweza kutumia kwa muda dawa ili kuondoa athari zilizosababishwa na GERD kwenye njia ya chakula.

Kama athari za GERD zitakuwa zimeisha na hernia iko-controll hapo unaweza kusitisha dawa na kuendelea very strictly na mwenendo wako wa maisha ili ku-control hernia ili usipate GERD.
 
Ukibadili mfumo wa maisha ukaweza ku-control hernia, likely utaweza kutumia kwa muda dawa ili kuondoa athari zilizosababishwa na GERD kwenye njia ya chakula.

Kama athari za GERD zitakuwa zimeisha na hernia iko-controll hapo unaweza kusitisha dawa na kuendelea very strictly na mwenendo wako wa maisha ili ku-control hernia ili usipate GERD.
Asante sana kwa ushauri wako,najitahidi sana kufuata masharti japo ni magumu ila nimeamua kuyafuata, namuomba Mungu anisaidie
 
To further add and stress on what has been said by others:-

1) Realy more on life style changes/adjustments especially with regards to Foods choices, avoiding unecessary stressful situations if possible,taking your meals on time e.t.c;
2) Be careful with frequent use of the so called PROTON PUMP INHIBITORS such as Omeprazole, Lansoprazole, Pantoprazole .... which are mostly prescibed in GERD condtion as these have been associated with KIDNEY DEMAGE which might go on to be IRREVISCIBLE (though this isn't frequently talked about); BUT rather if possible you may rely on suitable Antacid Preparations (Liquids/Suspensions/Gels.....) some of which may contain ingredients that may help to protect GIT lining (e,g SUCRALFATE.....)

All the best.
 
Unapona kabisa ukipatiwa dawa na ukabadili life style especial cut off all acidity foods.
Pendelea vyakula hivi hapa.
 
Back
Top Bottom