Lukenwa
New Member
- Jan 30, 2019
- 2
- 2
Hili ni tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likizikumba Simu za aina zote iwe ni Android (Mfano Sumsung, HTC, Nokia, Tecno, Huawei n.k) au IOS (Simu zote za Apple, Iphone 4,Iphone X, Iphone 6+ n.k). Imekuwa ni karaha kubwa sana hasa pale unapokuwa katika matumizi ya simu yako mara ghafla inazima.
Leo tuangalie sababu ambazo mara nyingi zimekuwa zikijitokeza kabla ya kutokea tatizo hilo;
1. Betri kuisha muda wake, hii hasa hutokea mara nyingi ambapo unakuta Pale betri imepungua muda wa kutumika kwa ufasaha, na kupelekea kukosa nguvu za kuweza kufanya kazi kwa kiwango kikubwa na mwishowe hupelekea simu kuzima mara kwa mara
2. Kuharibika njia za kuweka betri (terminal), hii hupelekea simu kushindwa kuchaji/kuingiza moto kwenye simu, ambapo betri linakuwa halina moto.
3. Kuwepo kwa “applications” mbalimbali kwenye simu ambazo hujikuta zinajipakua zenyewe hasa kwenye Simu hizi za Android. Kitendo hicho hupelekea simu kuzidiwa kwenye mfumo wa utendaji wa simu na kupelekea simu kujizima ghafla. Mara nyingi hutokea pale ambapo simu hupata joto jingi sana.
4. Kutokea kwa shoti kwenye saketi, hii hasa ni pale ambapo simu imepata unyevunyevu kwenye saketi ambapo baadhi ya “chip” hupelekea kuungua kabisa. Kitendo ambacho husababisha simu kuzima ghafla.
Tumekuwa tukikutana na Maswali mwengi sana ambapo wengi uuliza simu kuzima ghafla wakati anaitumia, kumbe yawezekana sababu kubwa muhimu ni pale simu inapokuwa na betri ambayo haiwezi kuhimili kazi za simu yako na kupelekea simu kuzima ghafla.
Hivyo unapoona Changamoto hiyo jambo muhimu sana ni kuangalia betri lako kwenye simu yako. Na wengine wamekuwa wakilalamika kwamba betri nimeinunua haina muda mrefu itakuwaje haiwezi kufanya kazi na inazimazima?. Hapa tunapenda kuwashauri kwamba hakikisha unapata betri “ORIGINAL” kwa ajili ya Simu yako. Epuka kununua betri “FAKE” ambazo mara nyingi huuzwa kwa bei ndogo sana. Ni bora ukaingia gharama kubwa na ukapata kilicho bora kuliko kununua betri “fake” na kesho yake imezima.
Naamini kuna jambo umejifunza.