Tatizo la moyo

Tatizo la moyo

Big Dy

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2015
Posts
496
Reaction score
615
Habari za muda huu wajenzi wa taifa hili,
Leo asubuh nimeamua kuanza mazoezi ila baada ya kukimbia umbali mrefu kidogo nikaanza sikia maumivu makali ya moyo, je hili linaweza kuwa ni tatizo kwa afya?
IMG_20201012_133322.jpg
 
Nakushauri ukapimwe vipimo vya ECG na ECHO kujua kama una tatizo la moyo.
 
Mimi sio Dr ila nimewahi kumsikia prof Janabi kwenye TV kwamba ni vizuri kabla hujaamua kufanya mazoezi ya kukimbia ukacheck afya ya moyo kama inaruhusu ufanye mazoezi ya mbio, na alitoa mfano wa mtu aliyeanguka na kupoteza maisha wakati akifanya mazoezi yakukimbia kwa kutumia machine za kukimbilia zile za gym, anasema huyu mtu alikuwa na matatizo ya moyo na alikuwa hafahamu, ndio maana mara nyingi unashauriwa ufanye mazoezi ya kutembea tu, hadi uwe na uhakika moyo wako upo vizuri kufanya mazoezi ya mbio
 
Nakushauri ukapimwe vipimo vya ECG na ECHO kujua kama una tatizo la moyo.
Hana tatizo la Moyoo ilaa Amefanya Overworking ya Heart muscles...!! Na short supply ya Oxygen lazima Utapata Muscles cramps specifically muscles za moyo ambapo hutokea kama maumivu flani ya kifua na Ukiacha kukimbia muda huo huo maumivu yanaacha. Shida huwa kama maumivu yataendelea kwa muda wa masaa kadhaa zaidi baada ya kuacha kukimbia. Ni jambo la kawaida sawa na muscles cramps za misuli ya miguu..
 
Back
Top Bottom