Tatizo la miguu mtoto mdogo kukanyaga pembeni

NITIKE NDOSI

Senior Member
Jan 15, 2013
153
86
Habari wakuu!

Nina mtoto mwwnye umri wa mwaka mmoja sasa ana matatizo ya miguu. Nimeligundua hili baada ya kufikia hatu hatua ya kutaka kusimama, ndipo nikajua hakanyagi saw a!

Anatumia upande wa kidole kikubwa kusimama, huku upande wa vidole vidogo huwa km vimenyanyuka juu na kisigino pia huenda upande!

Hatua nilizochukua ni kumpeleka hospitalini, baada ya kumchunguza wakadai kuna baadhi ya mishipa haiko sawa so akaanzishiwa clinic ya kumnyoosha kila siku. Lkn ni wiki ya tatu sasa sioni mabadiriko yoyote.

So please naomba ushauri mwingine ambao unaweza kunusuru hali ya kijana wangu na kurudi normal!
 
Habari wakuu!
Nina mtoto mwwnye umri wa mwaka mmoja sasa ana matatizo ya miguu. Nimeligundua hili baada ya kufikia hatua ya kutaka kusimama, ndipo nikajua hakanyagi sawa! Anatumia upande wa kidole kikubwa kusimama, huku upande wa vidole vidogo huwa km vimenyanyuka juu na kisigino pia huenda upande!
Hatua nilizochukua ni kumpeleka hospitalini, baada ya kumchunguza wakadai kuna baadhi ya mishipa haiko saw a ko akaanzishiwa clinic ya kumnyoosha kila siku. Lkn ni wiki ya tatu sasa sioni mabadiriko yoyote. So please naomba ushauri mwingine ambao unaweza kunusuru hali ya kijana wangu na kurudi normal!

Pole mkuu..ila usiwe na wasiwasi imeshatokea kwa watoto wangu wawili. Wa kwanza niliogopa kama wewe ila wa pili nikawa tayari na experience na wote wako sawa sasa. Kitu cha kwanza kufahamu ni ngumu kuuyoosha kama hajaanza kutembea. Mana wanapofanya mechanism ya kuunyoosha inabidi akiwa anakanyaga ndo unanyooshwa automatically. Wa kwanza nilimpeleka CCBRT na walimtengenezea viatu special vya kuunyoosha ndani ya miezi miwili akiwa anatembea ukanyooka vizuri, ikiwa bado wanarekebisha kiatu anaendelea kutembelea finally lazima unyoke tu. Mtoto wa pili nilikuwa mkoani hivyo nikampeleka hospitali ya wilaya tu na yeye wakamfungia POP ya kawaida tu kunyoosha kwa wiki 6 akiwa anatembea wakatoa ukawa umenyooka wakaongeza kama wiki 3 na mguu ukawa ok..sasa wako poa kabisa....Kwahiyo mkuu usiogope...ila matokeo mazuri na ya haraka ni pale ambapo mtoto ameanza kutembea.
 
NAshukuru sana kiongozi! Message yako imemifariji sana kiongozi wangu! God bless you!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom