Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,013
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.



Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.




Ushauri, Kinga na Tiba...




Mrejesho/Ushuhuda

 
Una uzito wa 98 Kg, ungetoa na urefu tungeweza jua kama BMI (Body Mass Index) yako ikoje. Manake uzito huenda ndio unakusababishia matatizo ya kuumwa visigino. Ingia hapa BMI (Body Mass Index) Calculator na uingize "data" zinazohitajika utajua BMI yako na pia inatoa majibu kama BMI ni ya kawaida ama una tatizo.

NI VIZURI UWATEMBELEE WATAALAMU WA AFYA (HOSPITALI) ILI KUPATA USHAURI WAO. Na pia MAZOEZI ni muhimu kwa afya yako.
 

Body mass index yangu ni 36,Nahitaji kujua pia ni aina gani ya mazoezi nahitaji kufanya, Kwani physician wamenishauri nisianze mazoezi makali kwanza.

Nimewaona wataalam mbali mbali na dawa nimetumia lakini nafuu haipo kabisa.
 
Dawa zipi umejaribu?Mimi nina ndg alikuwa na case kama ya kwako.Sikuamini,kuna Dr.anaitwa Sharrif yuko MOI(si rahisi-foleni) lkn alikuwa na clinic Hindu Mandal. alipigwa X-ray,na kwa maelezo ya ki lay man tatizo lilikuwa mishipa.

Baada ya X-ray,ikabidi anyukwe sindano za visigino,1 kila kisigino-aaaaah mbona anatembea na viatu vya kuchuchumaa sasa! Nahisi unaweza kuwa na tatizo hilo x 2.
Rakey
 

Fuatilia ushauri wa huyu jamaa naona kama vile utakufaa
 
Timor,
Pole sana kwa matatizo yako,niseme machache kutokana na uelewa wangu tu kuhusu tatizo lako ingawa mie sio daktari ila waweza kuchukua haya na kufanya vipimo.

Miguu kuwaka moto yaweza kuwa ni ugonjwa unaitwa peripheral neuropathy au nerve zako ambazo zinatoka kwenye uti wa mgongo kubanwa(pinched nerves)

Peripheral neuropathy husababishwa mostly na ugonjwa kama kisukari pamoja na aids,ingawa wataalam wanasema hata bakteria wengine pia huweza kusababisha.

Kama ni peripheral neuropathy hiyo kuwaka moto itaendelea mpaka mikononi in a course of time,while pinched nerve ikiwa serious huweza kusababisha uka-paralize.

ushauri:Nenda kacheck kisukari,hiv infections,x-ray ya mgongo/MRI mara moja.Pia kuna mazoezi waweza kufanya yakakusaidia.Check na diet punguza carbohydrate,acha kabisa sigara na pombe kama unatumia,na lastly jaribu kusali sana kwani hata mambo ya ushirikina pia yapo
 
Kwa Tatizo lako la Miguu kuwako Moto na Visigino jaribu kupakaa Hina kwenye nyayo zako inasaidia sana kwa hayo matatizo yako na kwa jambo la Unene jaribu kuwa unatembea kila siku kwa umbali wa kilomita kama tatu au tano kwa kila siku utapunguwa na jaribu pia kuwacha kula vyakula vya Mafuta Mafuta na kila siku jaribu kuwa unakunywa kijiko kimoja cha Siki ya Apple itakuasaidia kupunguza unene wako.
 
Wakuu heshima mbele!wajameni nina shida!naamini kabisa huku jamvini kuna wataalamu waliobobea!mimi kijana wanagu ana umri wa mwaka mmoja na miezi minne!ana uzito wa Kg 11,tatizo lake lipo kama ifuatavyo!

Huwa hana tatizo lolote ila ikifika mida ya usiku miguu yake visigino vinakua vya moto si kawaida!nilimpeleka hospital dokta akasema labda ni UTI au ni malaria,tukachek malaria hana kirus cha malaria hata!na huwa hana homa hata ila ni visigino tu ndio vinakua vya moto!naombeni sana wandugu mnijuze hili ni tatizo gani na dawa yake ni nini?

Asanteni
 
wataalam wa jf nimekuwa napata shida wakati wa usiku ninaposhtuka kutoka usingizini, ninasikia vidole vya mikononi vimekufa ganzi.

Hali hii ikitokea inachukua kama sekunde 30 ndo hali inarudia kawaida.

Nawaomba msaada wenu wa kitabibu. asanteni'
 
Pole sana ngoja wataalamu wakupe ushauri mimi hapa ushauri wangu naomba uwaone wataalamu kwanza maana hapa unaweza usipate mtaalamu haraka!
 
Jaribu kila siku kunywa maji mengi itasaidia hayo maji kusukuma damu ili iweze kufika vidoleni, na pia uwe unafanya Masaji hivyo vidole vyako pia hiyo itasaidia damu kufanya kazi yake vizuri.

Na ikiwa bado hujapata mabadiliko yoyote waweza kwenda kumona Daktari ataweza kukusaidia vizuri.
 
kwanza kabisa tatizo kama hilo linaweza kuwa limesababisha na vitu vitu vingi lakini vifuatavyo vyaweza kuwa sababu

1. yawezakana unafanya kazi saana za ofisini yaani namaanisha muda mda shingo yako inakuwa imeinama so inaweza kusababisha nerve compression

2. kama kupata ganzi kwa vidole kuanaambata na shingo kuwa nguma i mean neck stiffness, na kuwa na ganzi kidogo kwenye miguu hii inaweza kuwa ni spinal cord compression around C1-4 so unatakiwa kwenda kumuona dackari wa mifupa lakini hii ni kama uliwahi kuwa na trauma/ajali siku za nyuma lakini hukuwa na tatizo lolote, kama wewe unapenda kupigana au la kitu ambacho chaweza kusababisa spinal fracture au unadevelop osteoporosis,
unaweza kupata massage kama tatizo siyo serious saana pia upunguze kukaa kwa muda mrefu kama unafanya kazi ofisi au kubeba vitu vizito

mwisho kamuone daktari atakupa ushauri zaidi.
NB MRI IS BEST WAY OF DIAGNOSIS
 
wataalam wa jf nimekuwa napata shida wakati wa usiku ninaposhtuka kutoka usingizini, ninasikia vidole vya mikononi vimekufa ganzi. Hali hii ikitokea inachukua kama sekunde 30 ndo hali inarudia kawaida.
Nawaomba msaada wenu wa kitabibu. asanteni'

una vidonda vya tumbo?
 


kazi yangu fundi wa kushona nguo. Mda mwingi nautumia nikiwa nimeinamisha shingo! Nayo yaweza kuwa sababu?
 
Aisee kwenu wataalam wa afya nina tatizo la kufa ganzi vidole vya mikono mara nyingi asubuh nikitoka kuamka najikuta niko kwenye hali iyo nyakat zingine hata nikiwa ktk mazingira ya kawaida.

Je hali iyo inasababishwa na nini? Na kama kuna suluhisho naomba tuambiane.
 
Sijui umri wako ila naomba unifahamishe yafutayo.uliwahi kupata ajali au ugonjwa wa muda mrefu,malaria kali ,ugonjwa wa uti wa mgongo,kuumia kichwa?

hali ya lishe iko vipi?nini shughuli zako?je kuna magonjwa yoyote ya kurithi?una kaa kwenye eneo gani(baridi ,joto).ni vizuri tukaanzia hapo ili tuendelee na ushauri mzuri.
 

pole sana ndugu,kuna sababu zaidi ya mia moja ambazo zinaweza kusababbisha mikono kufa ganzi.

Muone mganga kwa vipimo ili ujua tatizo linasababishwa na nn zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…