Tatizo la miguu kuwaka moto (neuropathy): Ushauri, Kinga na Tiba

JamiiForums

JamiiForums

Official Robot
6,013
2,000
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.

Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.

Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.

WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.

Mi nina tatizo la miguu kuchemka,yaani nahisi kama nyayo zimelowekwa motoni naomba ushauri tafadhari, pia nina tatizo la kuhisi kama nina baridi kali upande mmoja wa mwili wangu(wa kulia).

Nahisi kama ninakuwa na baridi kali hadi mkono wote wa kulia unakuwa kama umechoka na kulegea.

Msaada please
Habari.

Ndugu wana Jf, kwa takribani zaidi ya mwaka sasa, ninasumbuliwa na tatizo la nyayo za miguu kuwaka moto.

Wakati inaanza nilijua tatizo ni aina ya viatu ninavyo tumia, nikabadirisha na tatizo likabaki pale pale.

Nikaamua kwenda hospitali mara kadhaa bado tatizo halija ondoka,(dawa nilizo tumia, ni multvitamin, neurobine, na neuro support. na siku hizi, nyayo zina uma mda wowote tofauti na mwanzoni ambapo nyayo zilikuwa zinauma wakati wa usiku pekee.

Pia, nyayo zikiuma nnakuwa najisikia hali ya kuchoka sana, na kukosa nguvu.

Hospitali nilizo enda ni za serikali, moja ya wilaya na nyingine ni ya mkoa.

Sasa nnawaomba ndugu zangu, msaada wa mawazo wa jisni ya kupata ufumbuzi wa tatizo langu, eidha kwa kunielekeza hospitali ambayo nnaweza kwenda kupata matibabu kwa gharama yeyote ile nipo tayari.

Na kama kuna mtu aliwahi kupata hili tatizo, na likatatuliwa nnaomba unishirikishe na mimi nipate kupona maana nnateseka.

Asanteni.

Ushauri, Kinga na Tiba...

Pole sana kwa matatizo yako,niseme machache kutokana na uelewa wangu tu kuhusu tatizo lako ingawa mie sio daktari ila waweza kuchukua haya na kufanya vipimo.

Miguu kuwaka moto yaweza kuwa ni ugonjwa unaitwa peripheral neuropathy au nerve zako ambazo zinatoka kwenye uti wa mgongo kubanwa(pinched nerves)

Peripheral neuropathy husababishwa mostly na ugonjwa kama kisukari pamoja na aids,ingawa wataalam wanasema hata bakteria wengine pia huweza kusababisha.

Kama ni peripheral neuropathy hiyo kuwaka moto itaendelea mpaka mikononi in a course of time,while pinched nerve ikiwa serious huweza kusababisha uka-paralize.

Ushauri: Nenda kacheck kisukari,hiv infections,x-ray ya mgongo/MRI mara moja.Pia kuna mazoezi waweza kufanya yakakusaidia.Check na diet punguza carbohydrate,acha kabisa sigara na pombe kama unatumia,na lastly jaribu kusali sana kwani hata mambo ya ushirikina pia yapo
TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO MIGUU

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili

yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na

hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo

1.Mtu kuhisi ganzi

2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.

3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:

1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).

2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi

3.Uzito mkubwa wa mwili,

4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).

5.Shinikizo la damu,

Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa?

Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini? Ukipata majibu wasiliana na mimi kwa Private messege
Magonjwa haya ni upungufu wa vitamini B complex kuwa na matatizo ya kisukari,ulevi,uvivu wa mazoezi,kukaa eneo moja muda mrefu na nk.

Njia za kuepuka ugonjwa huu
- Kufanya mazoezi ya kukimbia na kunyosha miguu
- Usafi wa viatu na sox
Kama umeupata tumia njia hizi utapona kabisa
- Tumbukiza miguu kwenye maji ya uvuguvugu na ikiwemo chumvi kiasi na baada ya hapo paka limao maeneo yote yalio asilika
- Tumia sana vitunguu swaumu kuwa mda wa wiki moja tatizo litakuwa limekwisha.

Na pia kuna dawa ya vidonda vya tumbo ambayo huponya na kuviondoa kabisa na iyo daqa ina faida nyingi sana kam vile
- Kutibu kisukari
- Matatizo ya mgongo
- Nguvu za kiume
- Matatizo ya figo
- Matatizo ya moyo

Na mengine mengi san na pia natoa ushauli bure bila malipo yoyote kulingana na ugonjwa
waweza kunipigia kwenye namba 0752093410 au 0685299621.

Na dawa yangu ninaiuza kwa bei ndogo kuanzia 35000 tu kama uko mbali nitakutumia
MUNGU NA AKUBALIKI.
Asante kwa kusoma makala hii.
Mrejesho/Ushuhuda
Wakuu natumai mu wazima kwa kudra za muumba. Siku chache zilizopita niliweka Uzi hapa jukwaani, nikiomba msaada wa ushauri ili tatizo langu la miguu kuwaka moto nipate namna ya kulitatua kwani ilikuwa ni miezi miwili imepita nikiwa na tatizo hilo na nisingeweza kuvaa viatu kutokana na maumivu niliyokuwa nayo.

Msaada wa mawazo: Miguu inawaka moto

Nashukuru wanajukwaa mlinipa ushauri wa kila aina na niliufanyia kazi na sasa nimerudi kuwashukuru wanajukwaa wote kwa moyo uliojaa upendo kwa kuguswa na hali niliyokuwa nayo. Sasa tatizo nililokuwa nalo limeisha na viatu ninavaa na chuoni ninaenda bila tatizo.

Mungu aibariki JF na Wanajukwaa wote. Upendo wa namna hii udumu milele na milele.

Asanteni sana.

#Mavindozii.
 
M

Mfumwa

JF-Expert Member
1,456
1,195
Una uzito wa 98 Kg, ungetoa na urefu tungeweza jua kama BMI (Body Mass Index) yako ikoje. Manake uzito huenda ndio unakusababishia matatizo ya kuumwa visigino. Ingia hapa BMI (Body Mass Index) Calculator na uingize "data" zinazohitajika utajua BMI yako na pia inatoa majibu kama BMI ni ya kawaida ama una tatizo.

NI VIZURI UWATEMBELEE WATAALAMU WA AFYA (HOSPITALI) ILI KUPATA USHAURI WAO. Na pia MAZOEZI ni muhimu kwa afya yako.
 
Timor

Timor

Member
48
95

Body mass index yangu ni 36,Nahitaji kujua pia ni aina gani ya mazoezi nahitaji kufanya,Kwani physician wamenishauri nisianze mazoezi makali kwanza.Nimewaona wataalam mbali mbali na dawa nimetumia lakini nafuu haipo kabisa.
 
K

Katabazi

JF-Expert Member
355
0
Dawa zipi umejaribu?Mimi nina ndg alikuwa na case kama ya kwako.Sikuamini,kuna Dr.anaitwa Sharrif yuko MOI(si rahisi-foleni) lkn alikuwa na clinic Hindu Mandal. alipigwa X-ray,na kwa maelezo ya ki lay man tatizo lilikuwa mishipa. Baada ya X-ray,ikabidi anyukwe sindano za visigino,1 kila kisigino-aaaaah mbona anatembea na viatu vya kuchuchumaa sasa! Nahisi unaweza kuwa na tatizo hilo x 2.
Rakey
 
Bill

Bill

JF-Expert Member
5,705

Fuatilia ushauri wa huyu jamaa naona kama vile utakufaa
 
M

Mijicho

Senior Member
187
225
Timor,
Pole sana kwa matatizo yako,niseme machache kutokana na uelewa wangu tu kuhusu tatizo lako ingawa mie sio daktari ila waweza kuchukua haya na kufanya vipimo.
Miguu kuwaka moto yaweza kuwa ni ugonjwa unaitwa peripheral neuropathy au nerve zako ambazo zinatoka kwenye uti wa mgongo kubanwa(pinched nerves)

Peripheral neuropathy husababishwa mostly na ugonjwa kama kisukari pamoja na aids,ingawa wataalam wanasema hata bakteria wengine pia huweza kusababisha.

Kama ni peripheral neuropathy hiyo kuwaka moto itaendelea mpaka mikononi in a course of time,while pinched nerve ikiwa serious huweza kusababisha uka-paralize.

ushauri:Nenda kacheck kisukari,hiv infections,x-ray ya mgongo/MRI mara moja.Pia kuna mazoezi waweza kufanya yakakusaidia.Check na diet punguza carbohydrate,acha kabisa sigara na pombe kama unatumia,na lastly jaribu kusali sana kwani hata mambo ya ushirikina pia yapo
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
40,438
2,000
Kwa Tatizo lako la Miguu kuwako Moto na Visigino jaribu kupakaa Hina kwenye nyayo zako inasaidia sana kwa hayo matatizo yako na kwa jambo la Unene jaribu kuwa unatembea kila siku kwa umbali wa kilomita kama tatu au tano kwa kila siku utapunguwa na jaribu pia kuwacha kula vyakula vya Mafuta Mafuta na kila siku jaribu kuwa unakunywa kijiko kimoja cha Siki ya Apple itakuasaidia kupunguza unene wako.
 
M

mande

Member
8
0
Wakuu heshima mbele!wajameni nina shida!naamini kabisa huku jamvini kuna wataalamu waliobobea!mimi kijana wanagu ana umri wa mwaka mmoja na miezi minne!ana uzito wa Kg 11,tatizo lake lipo kama ifuatavyo!

Huwa hana tatizo lolote ila ikifika mida ya usiku miguu yake visigino vinakua vya moto si kawaida!nilimpeleka hospital dokta akasema labda ni UTI au ni malaria,tukachek malaria hana kirus cha malaria hata!na huwa hana homa hata ila ni visigino tu ndio vinakua vya moto!naombeni sana wandugu mnijuze hili ni tatizo gani na dawa yake ni nini?

Asanteni
 
R

Redey

Member
47
0
wataalam wa jf nimekuwa napata shida wakati wa usiku ninaposhtuka kutoka usingizini, ninasikia vidole vya mikononi vimekufa ganzi. Hali hii ikitokea inachukua kama sekunde 30 ndo hali inarudia kawaida.
Nawaomba msaada wenu wa kitabibu. asanteni'
 
Zipuwawa

Zipuwawa

JF-Expert Member
3,058
1,250
Pole sana ngoja wataalamu wakupe ushauri mimi hapa ushauri wangu naomba uwaone wataalamu kwanza maana hapa unaweza usipate mtaalamu haraka!
 
S

seniorita

JF-Expert Member
674
0
Go see a doc, na pia nenda massage....shida ya nerves hizo
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
40,438
2,000
Jaribu kila siku kunywa maji mengi itasaidia hayo maji kusukuma damu ili iweze kufika vidoleni, na pia uwe unafanya Masaji hivyo vidole vyako pia hiyo itasaidia damu kufanya kazi yake vizuri. Na ikiwa bado hujapata mabadiliko yoyote waweza kwenda kumona Daktari ataweza kukusaidia vizuri.
 
Rodcones

Rodcones

JF-Expert Member
402
195
kwanza kabisa tatizo kama hilo linaweza kuwa limesababisha na vitu vitu vingi lakini vifuatavyo vyaweza kuwa sababu
1. yawezakana unafanya kazi saana za ofisini yaani namaanisha muda mda shingo yako inakuwa imeinama so inaweza kusababisha nerve compression
2.kama kupata ganzi kwa vidole kuanaambata na shingo kuwa nguma i mean neck stiffness, na kuwa na ganzi kidogo kwenye miguu hii inaweza kuwa ni spinal cord compression around C1-4 so unatakiwa kwenda kumuona dackari wa mifupa lakini hii ni kama uliwahi kuwa na trauma/ajali siku za nyuma lakini hukuwa na tatizo lolote, kama wewe unapenda kupigana au la kitu ambacho chaweza kusababisa spinal fracture au unadevelop osteoporosis,
unaweza kupata massage kama tatizo siyo serious saana pia upunguze kukaa kwa muda mrefu kama unafanya kazi ofisi au kubeba vitu vizito
mwisho kamuone daktari atakupa ushauri zaidi.
NB MRI IS BEST WAY OF DIAGNOSIS
 
Raia Fulani

Raia Fulani

JF-Expert Member
10,215
1,250
wataalam wa jf nimekuwa napata shida wakati wa usiku ninaposhtuka kutoka usingizini, ninasikia vidole vya mikononi vimekufa ganzi. Hali hii ikitokea inachukua kama sekunde 30 ndo hali inarudia kawaida.
Nawaomba msaada wenu wa kitabibu. asanteni'
una vidonda vya tumbo?
 
R

Redey

Member
47
0
kwanza kabisa tatizo kama hilo linaweza kuwa limesababisha na vitu vitu vingi lakini vifuatavyo vyaweza kuwa sababu
1. yawezakana unafanya kazi saana za ofisini yaani namaanisha muda mda shingo yako inakuwa imeinama so inaweza kusababisha nerve compression
2.kama kupata ganzi kwa vidole kuanaambata na shingo kuwa nguma i mean neck stiffness, na kuwa na ganzi kidogo kwenye miguu hii inaweza kuwa ni spinal cord compression around C1-4 so unatakiwa kwenda kumuona dackari wa mifupa lakini hii ni kama uliwahi kuwa na trauma/ajali siku za nyuma lakini hukuwa na tatizo lolote, kama wewe unapenda kupigana au la kitu ambacho chaweza kusababisa spinal fracture au unadevelop osteoporosis,
unaweza kupata massage kama tatizo siyo serious saana pia upunguze kukaa kwa muda mrefu kama unafanya kazi ofisi au kubeba vitu vizito
mwisho kamuone daktari atakupa ushauri zaidi.
NB MRI IS BEST WAY OF DIAGNOSIS

kazi yangu fundi wa kushona nguo. Mda mwingi nautumia nikiwa nimeinamisha shingo! Nayo yaweza kuwa sababu?
 
M

mataka

JF-Expert Member
286
225
Aisee kwenu wataalam wa afya nina tatizo la kufa ganzi vidole vya mikono mara nyingi asubuh nikitoka kuamka najikuta niko kwenye hali iyo nyakat zingine hata nikiwa ktk mazingira ya kawaida. Je hali iyo inasababishwa na nini? Na kama kuna suluhisho naomba tuambiane.
 
M

mamakunda

JF-Expert Member
370
195
VUTA subira wataalam watakuja tu, hapa ndo penyewe.
 
KAKA A TAIFA

KAKA A TAIFA

JF-Expert Member
564
195
Sijui umri wako ila naomba unifahamishe yafutayo.uliwahi kupata ajali au ugonjwa wa muda mrefu,malaria kali ,ugonjwa wa uti wa mgongo,kuumia kichwa?hali ya lishe iko vipi?nini shughuli zako?je kuna magonjwa yoyote ya kurithi?una kaa kwenye eneo gani(baridi ,joto).ni vizuri tukaanzia hapo ili tuendelee na ushauri mzuri.
 
Mr Kiroboto

Mr Kiroboto

JF-Expert Member
341
225
Aisee kwenu wataalam wa afya nina tatizo la kufa ganzi vidole vya mikono mara nyingi asubuh nikitoka kuamka najikuta niko kwenye hali iyo nyakat zingine hata nikiwa ktk mazingira ya kawaida. Je hali iyo inasababishwa na nini? Na kama kuna suluhisho naomba tuambiane.
pole sana ndugu,kuna sababu zaidi ya mia moja ambazo zinaweza kusababbisha mikono kufa ganzi.Muone mganga kwa vipimo ili ujua tatizo linasababishwa na nn zaidi
 
Forum statistics

Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom